Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Tengeneza mfumo bora wa wafanyakazi kwenye biashara yako.

By | April 4, 2016

Kama unaendesha biashara ndogo ambayo unategemea siku moja ikue, basi jambo kubwa la kuzingatia kuanzia sasa ni kutengeneza mfumo bora wa wafanyakazi kwenye biashara yako. na kama tayari biashara yako ni kubwa, unahitaji kuwa na mfumo bora wa ufanyaji kazi kwenye biashara yako. Jambo hili ni muhimu kwa sababu wafanyabiashara (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Hakuna Kisichokuwa Na Mwisho Na Mambo Muhimu Ya Kujifunza Na Kuzingatia.

By | April 3, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Karibu tena kwenye kipengele hiki muhimu sana cha makala za FALSAFA MPYA YA MAISHA, ambapo kwa pamoja tunatengeneza yale maisha ambayo tunapenda kuyaishi na siyo kufuata yale ambayo kila mtu anayaishi. Leo katika makala yetu tunakwenda kuangalia dhana muhimu sana ambayo wote tunatakiwa kuielewa kuhusu (more…)

UKURASA WA 459; Ulaji Na Uzalishaji…

By | April 3, 2016

Katika kila jambo linaloendelea duniani, kuna makundi mawili ya watu. Kuna walaji na kuna wazalishaji. Walaji ni wale ambao wanasubiri kitu kitoke na wao waanze kutumia. Na wazalishaji ni wale ambao wanaangalia kipi kinahitajika na wanakitengeneza kisha kuwapatia walaji. Katika makundi haya mawili wanaonufaika zaidi ni wazalishaji, kwa sababu walaji (more…)

UKURASA WA 458; Tatua Matatizo Yako Kwanza…

By | April 2, 2016

Tunapenda kutatua matatizo ya wengine, kila mmoja wetu ana ndoto kubwa ya kutatua matatizo ya dunia, kuibadili dunia, kuifanya dunia kuwa sehemu bora zaidi ya kuishi. Ila haya yote yanawezekana kama hiki kimoja kitafanyika, kuanza kutatua matatizo yako kwanza. Ni lazima uanze na matatizo yako kwanza, uweze kuyatatua, na baada (more…)

BIASHARA LEO; Unachojifunza Kutoka Biashara Za Wengine.

By | April 1, 2016

Pamoja na kwamba wewe ni mfanyabiashara, bado pia wewe ni mteja kwenye biashara za wengine. Ukianzia na unapopata mahitaji yako muhimu na hata unapopata huduma nyingine muhimu kwako. Usiishie tu kuwa mteja, bali hakikisha kupitia uteja wako unajifunza mbinu za kuboresha biashara yako. Kila unapokwenda kununua kwenye biashara nyingine, jiulize (more…)

UKURASA WA 456; Umekosea…

By | March 31, 2016

Unajisikiaje pale mtu mwingine anapokuambia neno hilo? Kwamba wewe umekosea? Mara nyingi watu wanapoambiwa hivyo kwa haraka sana huanza kupinga, huanza kutafuta kitu cha kujitetea. Kukosea kunauma na hivyo wengi hawapendi kuonekana wamekosea, hata kama ni kweli wamekosea. Badala yake hutafuta kila njia ya kujitetea na kujiondoa kwenye kile ambacho (more…)

BIASHARA LEO; Njia Rahisi Ya Kuua Biashara Yako.

By | March 30, 2016

Kuna njia nyingi sana unazoweza kutumia kuua biashara yako. Kwanza elewa kwamba wewe mwenyewe ndiye utakayeua biashara yako. Siyo mtu mwingine yeyote, ni wewe kwa kufanya au kutokufanya mambo fulani kwenye biashara yako. Sasa turudi kwenye hiki tulichopanga kujadili leo. Njia rahisi sana ya kuua biashara yako ni kuacha kujali (more…)