Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

MEDITATION(TAJUHUDI); Maana Yake, Jinsi ya Kufanya na Faida Zake.

By | April 10, 2016

Karibuni kwenye darasa letu la jumapili ya leo, ambapo tutakwenda kujifunza kuhusu MEDITATION (TAJUHUDI) Kwenye darasa la leo tutashirikiana na Dr Bukaza Chachage ambaye pia ni mmoja wa watu wanaofanya meditation kila siku. Kwa sehemu ya kwanza tutajifunza yafuatayo; 1. Maana ya meditatio, 2. Maandalizi ya kufanya meditation, 3. Jinsi (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Ubinafsi Wa Maisha Na Unavyokuzuia Kuwa Na Maisha Bora.

By | April 10, 2016

Habari za leo rafiki? Karibu tena kwenye kipengele chetu cha falsafa mpya ya maisha ambapo kwa pamoja tunakwenda kujifunza mambo muhimu kuhusu maisha ili kuweza kuyafanya maisha yetu kuwa bora, ya furaha na yenye mafanikio makubwa. maisha ndiyo kitu pekee ambacho hakuna atakayekikwepa, tutayaishi mpaka pale tutakapoacha maisha haya. Leo (more…)

UKURASA WA 466; Maisha Kama Mtihani…

By | April 10, 2016

Kama umeweza kusoma hapa basi nina uhakika umeshawahi kufanya mtihani au unajua mtihani maana yake nini. Na mitihani ipo ya aina nyingi, kulingana na mfumo wa maswali ulivyo kwenye mtihani husika. Kuna mtihani ambao unapewa majibu mengi na kuchagua jibu moja sahihi (multiple questions) na pia kuna mtihani ambao unapewa (more…)

UKURASA WA 465; Siyo Rahisi Kama Inavyoonekana.

By | April 9, 2016

Jamaa ameanza biashara na mtaji wa laki tano ila kwa sasa anamiliki biashara kubwa ya mtaji wa bilioni…. Jamaa amelima matikiti na sasa hivi una utajiri mkubwa sana…. Hadithi kama hizi zimejaa kila kona ya mazungumzo yetu. Na ni hadithi ambazo wengi wanapenda sana kuzisikia, na zinawahamasisha wengi kweli. Na (more…)

UKURASA WA 464; Sehemu Pekee Ya Kusema KAMWE…

By | April 8, 2016

Kuna maeneo mengi sana ya maisha yako ambayo huwezi kutumia neno kamwe. Na hii ni kwa sababu mambo mengi yanaweza kutokea bila ya wewe kuwa na maamuzi ya moja kwa moja. Unaweza kusema kamwe sitofanya kitu fulani, lakini ukajikuta kwenye mazingira ambayo inabidi ufanye. Wazungu wanasema NEVER SAY NEVER. Lakini (more…)

BIASHARA LEO; Makadirio Ya Matumizi Na Faida.

By | April 7, 2016

Unapoweka mipango yako ya kibiashara, ni lazima uwe na makadirio. Na linapokuja swala la fedha kuna makadirio mengi ambayo huwa tunayafanya kama wafanyabiashara. Tunakadiria matumizi yetu ya kibiashara, na pia tunakadiria mapato yetu na faida pia. Kitu kimoja cha kushangaza sana kuhusu makadirio yetu ni kwamba huwa siyo sahihi, karibu (more…)

UKURASA WA 463; Kondoo Na Mbwa Mwitu…

By | April 7, 2016

Kila kitu unachochagua kufanya kwenye maisha yako kina gharama. Kila hali unayochagua kwenye maisha yako ina gharama. Hii ni sheria ya asili, hivyo ni wewe kuchagua ni gharama gani uliyo tayari kuilipa. Katika maisha tunaweza kuwagawa watu kwenye makundi mawili, na makundi haya yanaendana kisifa na aina mbili za wanyama. (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; DIFFICULT CONVERATIONS (Mbinu Za Kujadili Mambo Magumu Na Muhimu Kwako)

By | April 6, 2016

Kuna mazungumzo ambayo ni muhimu sana kwa kila mmoja wetu, ila mazungumzo haya yanakuwa magumu kufanya kutokana na unyeti wake na umuhimu wake pia. Katika hali kama hii watu wengi hushindwa kutoa kile walichonacho mioyoni mwao na hivyo kubaki wanaumia au kuzikosa fursa muhimu kwao. Mazungumzo kati yako na mwenza (more…)

UKURASA WA 462; Rahisi Na Sahihi.

By | April 6, 2016

Hakuna wakati mzuri wa kupima ukuaji wetu, kupima maendeleo yetu binafsi kama wakati ambapo tunapitia changamoto. Mambo yanapokuwa shwari hakuna tatizo, kila kitu kinakwenda kilivyopangwa na hata mtu wa kawaida ataonekana ni bora kwenye nyakati hizo. Lakini mambo yanapokuwa magumu, changamoto zinapoibuka, hapa ndipo tunapowajua wale wa tofauti, wale waliojitoa (more…)

BIASHARA LEO; Usitumie Biashara Mpya Kuua Biashara Yako Ya Zamani.

By | April 5, 2016

Unapoanza na biashara moja na ukaona inafanya vizuri, unapata mawazo ya kukua zaidi kibiashara, na kufikiria kufungua biashara nyingine mpya. Hili ni wazo zuri sana kwa sababu huwezi kubaki pale pale kwa siku zote, kama mfanyabiashara makini ni lazima ukue. Lakini hapa kwenye ukuaji, hasa wa kuanzisha biashara mpya kuna (more…)