Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 274; Sio Tatizo Lako, Ni Tatizo Lao Wenyewe…

By | October 1, 2015

Msingi wa kwanza kabisa wa wewe kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako ni kuchukua majukumu yote ya maisha yako. Yaani chochote kitakachotokea kwenye maisha yako ni juu yako mwenyewe. Huna wa kumlaumu au kumlalamikia, ni wewe mwenyewe umesababisha na hivyo unahitaji kufanya kazi kurekebisha, kama ni kosa. Lakini msingi huu (more…)

UKURASA WA 273; Uliza Maswali….

By | September 30, 2015

Tulipokuwa watoto, chochote ambacho tulikuwa hatujui au hatuelewi, tulikuwa tunauliza. Na wala hatukuona aibu kwamba tutaonekana hatujui. Tuliuliza bila ya kuwa na wasi wasi na pale tulipoona majibu hayaridhishi tuliuliza tena na tena. Kuna wakati tulikuwa ving’ang’anizi mpaka aliyekuwa anakataa kitoa jibu anaamua kutoa ili tu kuondokana na kelele za (more…)

UKURASA WA 272; KESHO….

By | September 29, 2015

Kesho ni siku ambayo haijawahi kufikiwa. Kesho ni mwizi wa ndoto kubwa za watu wengi. Kesho ni njia ambayo umekuwa unatumia kutoroka matatizo yako. Kesho ni siku ambayo inapatikana kwenye kalenda ya wajinga, hakuna kalenda yoyote duniani imeandikwa kesho. Lakini tunaipenda kesho, tunaitumia kesho kila mara, na bado hatujawahi kuifikia (more…)

Mambo muhimu ya kuzingatia pale unapoanza biashara na mtaji mdogo.

By | September 28, 2015

Moja ya maswali ambayo huwa napokea sana kutoka kwa watu wanaotaka kuanza biashara huwa ni biashara gani waanze kwa mtaji kidogo wanaokuwa nao. Mfano wa swali huwa, “nina laki tano, naweza kuanza biashara gani kwa kiasi hiki cha fedha?” swali hili huwa linaulizwa mara nyingi sana kwa viwango vidogo na (more…)

UKURASA WA 271; Unachoweza Kufanya Baada Ya Kushindwa.

By | September 28, 2015

Pamoja na malengo na mipango mizuri ambayo unaiweka kabla ya kuanza kufanya jambo lolote, bado huna uhakika wa asilimia 100 kwamba utafanikisha kufanya. Na nafasi ya kushindwa ni kubwa kuliko ya kushindwa. Kwa kifupi utashindwa, katika baadhi ya mambo ambayo utakuwa umepanga kufanya. Sasa kushindwa sio tatizo, ila kinachotokea baada (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Jinsi Ya Kuimarisha Falsafa Yako Mpya Ya Maisha.

By | September 27, 2015

Habari mwanafalsafa? Ndio, wewe ni mwanafalsafa, na wala huhitaji kusubiri mpaka mtu akuite hivyo. Chimbuko la neno falsafa au kwa kiingereza philosophy ni neno la kigiriki filosofia ambalo maana yake ni kupenda busara/hekima. Kwa kifupi ni kupenda kujifunza na kufikiri zaidi juu ya kile kitu unachofanya au vile unavyoishi. Kwa (more…)

UKURASA WA 270; Mafanikio Ya Kushikiza Kwenye Vitu.

By | September 27, 2015

Jamani hii ni vita, Halafu ni safari ndefu sana. Halafu maisha yako ndio haya, huwezi kuyasimamisha uje uyaishi baadae. Mara nyingi tunapozungumzia mafanikio, watu huwa na picha ya vitu vikubwa ambavyo wamevifikia, ni vizuri sana, kwa sababu mafanikio yana maana tofauti kwa watu tofauti. Na mafanikio haya yanaweza kumfanya mwingine (more…)

UKURASA WA 269; Hapa Ndipo Unapojificha.

By | September 26, 2015

Kuna sehemu ambapo umekuwa unajificha. Unajificha sehemu hii sio kwa ajili ya kujilinda bali kwa ajili ya kutoroka kufanikiwa, kwa ajili ya kutoroka kufanya mambo makubwa. Umetafuta sehemu ambayo ukishajificha pale hakuna mtu anayeweza kukulaumu kwamba kwa nini hujafanya mambo makubwa au kwa nini hujatimiza ulichoahidi. Wewe mwenyewe umeshafurahia hapo (more…)

UKURASA WA 268; Hii Ni Vita Kali, Jipange Sana.

By | September 25, 2015

Kuwa bora ni vita kali sana, kwa sababu kila kinachokuzunguka kinakulazimisha kuwa kawaida. Kuwa tofauti ni vita kali sana, kwa sababu kila mtu anategemea uwe kama wengine walivyo. Kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako ni vita kuu kuliko zote utakazokuja kupigana kwenye maisha yako. Vita hii itaanza na wewe binafsi, (more…)

UKURASA WA 267; Wakati Wa Mabadiliko Na Kinachochochea Mabadiliko Ya Kweli.

By | September 24, 2015

Moja; watu hatupendi mabadiliko. Ndio hatupendi kabisa. Hatujui ni kitu gani kitakachotokea baada ya mabadiliko na hivyo hii inatuletea hofu zaidi. Tunapenda kufanya kile ambacho tuna uhakika nacho, “nikifanya kazi mwisho wa mwezi nitapewa mshahara. Nikiingia kwenye biashara sina uhakika kama nitapata wateja”. Hivyo hili linawazuia wengi kubadilika. Mbili; kama (more…)