Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 283; Dawa Ya Hofu, Wivu, Chuki Na Hisia Zote Hasi…

By | October 10, 2015

Kuna hisia nyingi sana hasi ambazo zinatuzunguka kila siku. Na hisia hizi ndio zimekuwa zinafanya maisha ya wengi kuwa magumu na ya hovyo. Alama kubwa ya hisia hasi ni hofu kwenye maisha. Hofu imezuia watu wengi kuishi maisha yenye furaha. Hofu imesababisha baadhi ya watu kuishia kupata magonjwa ya akili. (more…)

UKURASA WA 282; Kuwa Makini…

By | October 9, 2015

Kukosa umakini kwenye vitu ambavyo tunafanya kumekuwa chanzo cha matatizo makubwa sana. Watu wengi wamepata hasara kubwa, watu wengi wamepoteza maisha yao, watu wengi wamejikuta kwenye hali ngumu kwa sababu tu kuna mtu hakuwa makini kwenye kutimiza majukumu yake. Na kwa nini watu hawapo makini kwenye kutimiza majukumu yao? Kwa (more…)

UKURASA WA 281; Siyo Kwa Ajili Yako….

By | October 8, 2015

Unapofanya kitu cha tofauti, iwe ni kwenye kazi, biashara na hata maisha ya kawaida, kuna watu wachache watakuelewa na wengi sana hawatakuelewa. Hili sio tatizo kubwa. Tatizo kubwa ni hili, wale wengi ambao hawatakuelewa watatumia nguvu yao ya wingi kukuzuia wewe kuendelea kufanya unachofanya sasa. Watakukatisha tamaa kwa kukuambia haiwezekani (more…)

UKURASA WA 280; Huwezi Kudhibiti Chochote…

By | October 7, 2015

Kila mmoja wetu anapenda kudhibiti vitu. Kuwa na uhakika wa kile anachofanya au anachotarajia kufanya. Kila mmoja angependa kujua na kuwa na uhakika kwamba kinachotokea ni kama alivyopanga au alivyotegemea. Lakini pamoja na kutaka huku kudhibiti, ukweli ni kwamba hatuwezi kudhibiti chochote kilicho nje yetu. Hatuna nguvu hiyo, licha ya (more…)

UKURASA WA 279; Boresha Nembo Yako Kwa Kufanya Hivi….

By | October 6, 2015

Kila mmoja wetu ana nembo yake, na ni nembo ya ubora. Na nembo hii tunaiweka kwenye kila kitu ambacho tunafanya, kila kitu ambacho tunagusa na kila kitu ambacho tunasema au kufikiri. Umewahi kuwa mahali na kukawa kuna kitu kimefanyika na aliyefanya hajulikani lakini watu wakasema huyu atakuwa ni fulani? Kwa (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Kitu Kimoja Ambacho Wanafalsafa Wote Wanakubaliana Ndio Kimekufikisha Hapo Ulipo.

By | October 4, 2015

Habari za leo mwanafalsafa? Unaendelea kujifunza kuhusu falsafa yako mpya ya maisha? Hongera sana. Na je umeshaanza kuyaweka haya unayojifunza kwenye maisha yako? kama ndio hongera sana. Kama sio unasubiri nini? Maisha uliyonayo ndio haya, na wakati huu ulionao ndio una uhakika nao, hivyo ndio wakati wa kuishi yale maisha (more…)

UKURASA WA 277; Acha Kuua Ndoto Za Wengine.

By | October 4, 2015

Jana tulishirikishana kuhusu maadui zetu ambao ni watu wa karibu sana, ndugu na rafiki zetu.(kama hukuisoma bonyeza hapa) Msomaji mwenzetu alitaka twende mbali zaidi, sio kufikiri tu nani ni maadui zetu, bali sisi wenyewe tumekuwa maadui wa wakina nani. Na hii ni sahihi na muhimu sana kufanya kama kweli unataka (more…)

UKURASA WA 276; Ndugu Na Marafiki Zako Ndio Adui Zako Wakubwa.

By | October 3, 2015

Ndugu zako na marafiki zako wa karibu wanakupenda sana. Ndio maana mpaka sasa mpo karibu na mkishirikiana kwenye mambo mengi. Lakini hawa hawa ndugu na marafiki zako wa karibu, ni maadui wakubwa sana kwako. Sio maadui kwamba wanataka kukuua au kukupoteza, hapana. Ni maadui kwa sababu wana nia njema sana (more…)

UKURASA WA 275; Kama Watu Wote Wangekuwa Vipofu…….

By | October 2, 2015

Mara nyingi adui yetu mkubwa sio macho yetu wenyewe, bali macho ya wengine. Kuna watu wengi ambao wamejikuta wakifanya mambo ambayo sio muhimu kwao ila wanafanya tu ili waonekane nao wanafanya au wapo. Sasa hebu jiulize, kama watu wote duniani wangekuwa vipofu, na wewe pekee ndiye unayeona, je ungekuwa na (more…)