Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2020; Wakati Ni Huu…

By | July 12, 2020

Ni nadra sana kila kitu kwenda kama unavyotaka kiende. Hivyo kuacha kuchukua hatua mpaka wakati uwe sawa, kama unavyotaka wewe, ni kujichelewesha. Katika kila wakati kuna kitu hakitakuwa sawa, kuna changamoto binafsi utakuwa nazo, kuna changamoto za kimazingira au kiuchumi zinaweza kuibuka. Ukitaka sababu ya kutokufanya kitu chochote kile, utaipata (more…)

2019; Sifa Za Kuangalia Kwa Mtu Wa Kushirikiana Naye…

By | July 11, 2020

Kwenye safari ya mafanikio hakuna jeshi la mtu mmoja, kwamba utafanikiwa kwa kujitegemea wewe peke yako ni kujidanganya. Unahitaji ushirikiano wa watu wengine kwenye maeneo mbalimbali ndiyo uweze kufanikiwa. Kama ni biashara unahitaji kuwa na wabia, unahitaji kuajiri wasaidizi na unahitaji kupata wateja watakaonunua kile unachouza. Lakini kabla hujafika kwa (more…)

2018; Watu Wenye Hofu…

By | July 10, 2020

Watu wenye hofu huwa wanapenda kuzungukwa na watu wenye hofu. Ungeweza kufikiri kwamba watu hao wangependa kuzungukwa na wasio na hofu, wanaojiamini ili nao washinde hofu zao. Lakini hivyo sivyo ilivyo, watu wenye hofu wanapenda kuzungukwa na wengine wenye hofu ili kuhalalisha hofu zao. Wanachotaka kuamini ni kwamba hofu walizonazo (more…)

2017; Urahisi Na Raha Ya Kufanya…

By | July 9, 2020

Kanuni muhimu kabisa ya uchumi ni hii, kadiri kitu kinavyopatikana kwa wingi na urahisi, ndivyo thamani yake inakuwa ndogo na watu kutokuwa tayari kulipa gharama kubwa kukipata. Hii ndiyo kanuni unayopaswa kuendesha nayo maisha yako, kupima kila unachotaka kufanya ili kujua thamani yake. Kama unachofanya kinafanywa na kila mtu, usitegemee (more…)

2016; Kelele Na Kazi Haviendi Pamoja…

By | July 8, 2020

Upo usemi baina ya wawekezaji kwamba ukiona mkurugenzi mkuu (CEO) wa kampuni anaongea sana kwenye vyombo vya habari, basi jua kuna tatizo kwenye kampuni hiyo. Kuna kitu hakipo sawa au mkurugenzi huyo hafanyi kazi yake vizuri. Usemi huo una ukweli ambao ukiujua na kuutumia utakusaidia. Ni kweli kwamba kelele na (more…)

2015; Saa Moja Ya Kufanya Kazi…

By | July 7, 2020

Kama ambavyo mwanafalsafa Seneca amewahi kuandika, tatizo la muda siyo kwamba ni wa uhaba na hautoshi, bali ni mwingi na tunautawanya hovyo. Ndiyo maana swali maarufu la kujiuliza kama leo ingekuwa siku yako ya mwisho hapa duniani ungefanya nini, linatusaidia sana kuweka vipaumbele vyetu sawa. Tunapojua kwamba bado tuna muda, (more…)

2013; Umakini Wako Ndiyo Maisha Yako…

By | July 5, 2020

Mtu mmoja amewahi kusema niambie mambo unayofanya kila siku kwenye muda wako na nitakuambia wewe ni mtu wa aina gani. Kauli hiyo ina maana kubwa sana, kwa sababu kule ambapo unapeleka umakini wako, ndiyo kunakojenga maisha yako. Vitu vinavyochukua muda wako ndiyo vitu vinavyokujenga. Changamoto kubwa tuliyonayo ni kwamba umakini (more…)

2011; Asili Na Soko…

By | July 3, 2020

Hivi ni vitu viwili unavyopaswa kuvifuata, unavyopaswa kujifunza na pale unapohitaji maoni au mrejesho, basi angalia kwenye vitu hivyo viwili. Asili ina sheria zake ambazo huwa hazibadiliki kulingana na eneo au hali. Sheria za asili ni za kudumu. Ukizifuata utanufaika nazo, ukizivunja utaadhibiwa. Asili haijali wala haina huruma, inajua njia (more…)