Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2010; Unahitaji Uchoshi…

By | July 2, 2020

Tunaweza kusema maendeleo ya binadamu yamekuwa yanazaliwa kutokana na uchoshi (boredom). Pale ambapo mtu anakuwa kwenye hali ya kuboreka, akiwa hana cha kufanya ndipo akili yake inakwenda hatua ya ziada na kumwonesha njia za kukabiliana na chochote anachopitia. Na uchoshi huo ni ule ambapo mtu anakuwa mpweke, mawazo yake yanakuwa (more…)

2009; Hapo Ndipo Unapopaswa Kuwa…

By | July 1, 2020

Watu wengi hawaridhiki na pale walipo sasa, Iwe ni kiasi cha kipato wanachotengeneza, kazi au biashara wanayofanya au eneo wanaloishi. Wengi tuna ndoto kubwa zaidi ya pale tulipo sasa. Lakini ukweli ni kwamba, huwezi kufika kokote unakotaka kufika bila kuanzia hapo ulipo sasa. Kazi kubwa unayotaka kufikia, inaanzia kwenye kazi (more…)

2008; Dalili Ya Hofu Isiyoonekana Wazi Wazi…

By | June 30, 2020

Kila mtu huwa ana dalili fulani za hofu, pale anapokuwa na hofu, mwili wake huwa unamsukuma kufanya kitu fulani, hata kama hajui. Kuna ambao hung’ata kucha, kuna ambao mikono hutetemeka na wengine kutokwa jasho, hata kama hakuna joto. Ipo dalili ya kiakili ya hofu, ambayo huwa inawapata walio wengi, lakini (more…)

2007; Fursa Iliyokuwa Inakusubiri Wewe…

By | June 29, 2020

Ukiona watu wanakuna kwako na fursa, wanakuonesha fursa inayokufaa sana na kukushawishi ujiunge na fursa hiyo la sivyo utaikosa basi kuwa na uhakika kwenye jambo hili, wewe ni fursa kwa watu hao. Kama wanachokuambia ni fursa kweli, unafikiri ingekaa muda wote ikusubiri wewe? Unafikiri hao wanaokusisitiza ni fursa wangepoteza muda (more…)

2006; Uhuru Ni Kujitambua…

By | June 28, 2020

Mtoto mdogo akitaka kitu anakitaka kama anavyotaka yeye, hawezi kukubali kitu kingine isipokuwa kile anachotaka yeye. Kupata kile anachotaka anaweza kufikiri ni uhuru, lakini huo siyo uhuru. Uhuru siyo kupata kile ambacho mtu anataka kwa namna anayotaka yeye. Huko ni kuendeshwa na hisia au mihemko na siyo kuwa huru. Uhuru (more…)

2005; Motisha Ni Nyenzo Kwa Watu…

By | June 27, 2020

Mwanahisabati Pythagoras aliwahi kusema nipe nyenzo ndefu na mahali pa kusimama na nitaweza kuisogeza dunia. Hapa alionesha jinsi ambavyo nyenzo ina nguvu ya kufanya makubwa, yale ambayo kwa hali ya kawaida hayawezekani. Chukua mfano wa nyenzo kwenye maisha yetu ya kila siku, kung’oa msumari mahali kwa mikono yako ni zoezi (more…)

2004; Dakika Kumi Zinaweza Kufanya Nini?

By | June 26, 2020

Kitu kimoja ninachokiamini, na nitaendelea kuamini hivyo maisha yangu yote ni kwamba wale wanaosema hawana muda wa kufanya vitu fulani wanavyotaka kufanya huwa wanadanganya. Siyo kweli kwamba hawana muda, ila tu hawataki kufanya, sasa kwa kuwa hawataki kuukabili ukweli, wanatumia kisingizio cha muda. Kwenye siku kuna masaa 24 ambayo ukiyageuza (more…)

2003; Tatizo Siyo Kipaji…

By | June 25, 2020

Wakati tunasoma, somo la hisabati lilikuwa linaonekana ni somo gumu kwa wanafunzi walio wengi. Hivyo wale ambao walikuwa wanaliweza somo hilo walionekana kuwa na kipaji. Kulikuwa na kauli kabisa kwamba ‘hesabu ni kipaji’ Kwenye mafanikio pia, wapo wengi wanaoamini kwamba mafanikio yanahitaji mtu uwe na kipaji fulani. Na hapo wanatumia (more…)

2002; Mchezo Lazima Uendelee…

By | June 24, 2020

Hakuna mtu ambaye kila kitu kinaenda kama alivyopanga kwenye maisha yake. Lakini wapo watu wanaoendelea kufanikiwa licha ya kukutana na vikwazo vingi, huku wengine wakishindwa kwa vikwazo hivyo hivyo. Wale wanaofanikiwa ni wenye mtazamo wa kutoruhusu chochote kiwe kikwazo kwa safari yao. Wanachukulia safari ya mafanikio kama mchezo au onesho (more…)

2001; Halafu Mwisho Wa Siku Unapata Nini?

By | June 23, 2020

Upo usemi kwamba tatizo la mbio za panya ni kwamba hata ukishinda, unabaki kuwa panya. Ni usemi unaohusu zaidi eneo la fedha, hasa pale unapoishi maisha ya mashindano, kwamba hata ukiwashinda wengine, bado unaishia kuwa kama wao. Leo nataka tupeleke usemi huo kwenye eneo jingine la maisha yetu, eneo ambalo (more…)