Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

1999; Hushtuki Tu…

By | June 21, 2020

Ulipata kazi ya kwanza, ikawa hailipi vizuri, ukaicha. Ukapata nyingine, bosi akawa anakunyanyasa, ukaiacha pia. Ukapata nyingine, hiyo ukawa huelewi na wafanyakazi wengine, nayo ukaiacha pia. Na bado unalalamika kwamba hupati kazi nzuri. Hushtuki tu? Umepata mwenza wa kwanza, tabia mkawa hamuendani, mkaachana, ukapata wa pili, tena mkashindwa kuelewana, ukapata (more…)

1998; Cha Kufanya Unapokuwa Huna Uhakika…

By | June 20, 2020

Hakuna jambo lolote ambalo una uhakika nalo kwa asilimia 100 kwenye maisha yako. Lolote linaweza kutokea, na mara nyingi mambo ambayo huwa hatutegemei yatokee, huwa yanatokea kwa wakati ambao hatukutegemea yatokee. Huna uhakika kama kesho utakuwa hai, lakini je hilo linapaswa kukufanya upoteze siku ya leo? Huna uhakika kama wateja (more…)

1997; Kama Una Wasiwasi Na Usahihi Wake, Uko Sahihi…

By | June 19, 2020

Njia sahihi ya kufanikiwa huwa iko wazi na inaeleweka kirahisi na mtu yeyote yule. Ukiona kuna njia ya mafanikio ambayo huielewi, ambayo una wasiwasi na usahihi wake, basi jua uko sahihi, kwamba njia hiyo siyo sahihi. Hii ni kanuni fupi na rahisi sana itakayokuepusha na matatizo mengi kwenye maisha yako. (more…)

1996; Njia Bora Za Kukuza Mtandao Wako…

By | June 18, 2020

Kwenye maisha ya mafanikio, unamjua nani ni muhimu kama ilivyo unajua nini. Mtandao wa wale unaowajua na wanaokujua una mchango mkubwa sana kwenye mafanikio yako. Wengi wamekuwa wanahangaika kukuza mitandao yao kwa njia ambazo huwa naita ni za kujipendekeza. Njia za kuhangaika ili uonekane na wewe upo, lakini mtandao unaotengeneza (more…)

1995; Hatua Tatu Za Kutengeneza Wateja Kwenye Biashara…

By | June 17, 2020

Iko wazi kwamba kuendesha biashara ni kugumu na kuna changamoto nyingi. Lakini ugumu na changamoto nyingine tumekuwa tunaziongeza wenyewe, kwa yale tunayofanya au kushindwa kufanya. Na moja ya maeneo ambayo tumekuwa tunaongeza changamoto kwenye biashara zetu ni kushindwa kutengeneza wateja wa biashara zetu. Hii ni kwa sababu wengi huingia kwenye (more…)

1994; Sikiliza Ukimya…

By | June 16, 2020

Tunaishi kwenye zama za usumbufu, zama ambazo ni vigumu sana kukaa kwenye ukimya na utulivu. Kifaa tunachotembelea nacho kila mahali, yaani simu janja, hua hakitupi kabisa nafasi ya kuwa na ukimya na utulivu. Kila wakati kinatuletea taarifa kwamba kuna watu wanatutafuta, kuna mambo yanaendelea mitandaoni na kadhalika. Hivyo kila wakati (more…)

1993; Kuhusu Kufanya Kila Kitu…

By | June 15, 2020

Tukiwa tunaendelea na msisitizo kwenye ufanyaji badala ya kupanga na kusubiri, kuna changamoto nyingine ambayo wengi wanaikaribisha. Watu wengi huwa wanataka wafanye kila kitu wao peke yao, na hilo siyo tu linawakwamisha kuanza, bali pia linawafanya washindwe kuzalisha kitu bora na cha kipekee. Huwezi kufanya kila kitu, huna muda wala (more…)

1992; Tumia Zana Zinazokuzunguka…

By | June 14, 2020

Kwenye ukurasa wa 1991 nimekuambia uko tayari kuanza, huhitaji kusubiri mpaka uwe mkamilifu, anzia hapo ulipo sasa na endelea kujifunza kadiri unavyokwenda. Lakini najua unaweza kuacha kuanza kwa kisingizio kwamba huna zana za kuanza kufanya, kwamba inahitaji gharama kupata zana hizo na huwezi kumudu gharama hizo kwa sasa. Niendelee kukuambia (more…)

1991; Uko Tayari Kuanza…

By | June 13, 2020

Moja ya vitu vinavyowazuia wengi kuanza yale waliyopanga kuanza, ni kuona bado hawajawa tayari. Wengi wamekuwa wakiona bado hawajajifunza vya kutosha, au kuna kitu bado hawajajua, hivyo wanasubiri mpaka wajue kila kitu ndiyo waanze. Huku ni kujidanganya na kuficha ukweli kwamba haujawa tayari kuanza. Ukweli ni kwamba, tayari unajua kiasi (more…)