Category Archives: SHERIA ZA SIKU

#SheriaYaLeo (356/366); Tumia kifo kuziondoa tofauti.

By | October 22, 2022

#SheriaYaLeo (356/366); Tumia kifo kuziondoa tofauti. Kifo ni moja ya vitu vinavyotuleta mahali pamoja wote. Ni kitu kinachotufanya wote kuwa sawa kwa sababu mwisho wa siku wote tutakufa. Haijalishi tofauti zetu kwenye maisha, wote njia yetu ni moja, kifo. Yote tunayobaguana nayo hayana tofauti kwenye kifo. Kwa kujua hatima hii (more…)

#SheriaYaLeo (355/366); Jua yaliyo muhimu.

By | October 21, 2022

#SheriaYaLeo (355/366); Jua yaliyo muhimu. Tuna malengo ya kufikia, miradi ya kukamilisha na mahusiano ya kuboresha. Chochote tunachofanya kwa wakati wowote ule kinaweza kuwa ndiyo kitu cha mwisho kwetu kufanya. Hivyo tunapaswa kuhakikisha kila tunachofanya ndiyo kilicho muhimu zaidi na kuweka juhudi zetu zote kwenye kitu hicho. Kwa utambuzi huu (more…)

#SheriaYaLeo (354/366); Jichukulie umezaliwa upya.

By | October 20, 2022

#SheriaYaLeo (354/366); Jichukulie umezaliwa upya. Pale unapopitia magumu sana kwenye maisha yako na kuona kama yamefika tamati, ila ukaweza kuyavuka, unapaswa kutumia hali hiyo kuishi kwa tija zaidi. Jichukulie kama mtu uliyezaliwa upya, ambaye umepata nafasi nyingine ya maisha baada ya kushindwa kutumia vizuri nafasi ya awali. Kwa kujichukulia umezaliwa (more…)

#SheriaYaLeo (353/366); Kuwa na haraka na matamanio.

By | October 19, 2022

#SheriaYaLeo (353/366); Kuwa na haraka na matamanio. Unapokuwa na muda mwingi wa kufanya kitu, huwa inakuwa rahisi kuahirisha kufanya kitu hicho, kwa kujiambia utafanya kesho. Tunapokuwa na muda mwingi huwa tunaishia kuupoteza kwa usumbufu na mambo yasiyokuwa na tija kwetu. Inakuwa vigumu kuweka umakini wetu wote kwenye yaliyo muhimu na (more…)

#SheriaYaLeo (352/366); Kuona kitu kwa mara ya mwisho.

By | October 18, 2022

#SheriaYaLeo (352/366); Kuona kitu kwa mara ya mwisho. Kama binadamu tungekuwa tunaishi milele, maisha yangepoteza maana. Ni ufupi wa maisha ndiyo unatufanya tuyathamini na kufanya yale yenye tija. Lakini wakati mwingine huwa tunajisahau na kuzoea vitu, kwa kuona vipo muda wote. Ili kuondoka kwenye mazoea haya na kuvithamini vitu, tunapaswa (more…)

SheriaYaLeo (351/366); Kukikaribia kifo.

By | October 17, 2022

SheriaYaLeo (351/366); Kukikaribia kifo. Watu wengi huendesha maisha yao kwa mazoea na kupoteza muda kwenye mambo yasiyokuwa na tija. Ni mpaka pale wanapokutana na hatari ya kifo ndiyo wanayabadili maisha na kuishi kwa tija. Inaweza kuwa ni kwenye ajali ambayo mtu amenusurika kufa au kupata ugonjwa ambao hawezi kupona. Katika (more…)

#SheriaYaLeo (350/366); Kitambue kifo kwa vitendo.

By | October 16, 2022

#SheriaYaLeo (350/366); Kitambue kifo kwa vitendo. Huwa tunakihofia kifo kwa sababu tunajiweka mbali nacho. Imekuwa ikielezwa kwamba dawa ya hofu ni kufanya kile unachohofia. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye kifo, kama hutaki kukihofia, unapaswa kukitambua kifo kwa vitendo. Kujenga hali inayokukumbusha kifo kila wakati kiasi kwamba hukihofii tena. Moja ya (more…)

#SheriaYaLeo (349/366); Ondoka kwenye mazoea na kuiga.

By | October 15, 2022

#SheriaYaLeo (349/366); Ondoka kwenye mazoea na kuiga. Huwa tunaiangalia dunia kwa kutumia mazoea na kuiga wengine. Tunafanya yale tuliyozoea kufanya au tunayowaona wengine wakifanya. Kuna mengi ambayo tunashindwa kuyang’amua kutokana na mazoea tunayokuwa nayo. Hayo yanatutaka kwenda zaidi ya mazoea na kuiga. Yanatutaka tutumie uwezo mkubwa ulio ndani yetu kuweza (more…)

#SheriaYaLeo (348/366); Jinsi ya kuiangalia dunia.

By | October 14, 2022

#SheriaYaLeo (348/366); Jinsi ya kuiangalia dunia. Watu wengi huwa wanaiangalia dunia kwa mazoea. Wanatumia yale waliyoyazoea kutafsiri yanayotokea na kufanya maamuzi. Wanapenda uhakika wa mazoea, hata kama hayaleti matokeo yaliyo bora. Wewe hupaswi kuwa hivyo, badala yake unapaswa kuiangalia dunia kama mchunguzi. Unapaswa kuiangalia dunia ukiwa tayari kujifunza na kujaribu (more…)

#SheriaYaLeo (347/366); Maisha na kifo.

By | October 13, 2022

#SheriaYaLeo (347/366); Maisha na kifo. Tunaweza kuelezea tofauti kati ya maisha na kifo kwa namna ifuatayo; Kifo ni utulivu kamili, bila ya mwendo au mabadiliko, isipokuwa kuharibika. Kwenye kifo tunatenganishwa na wengine na kuwa wapweke. Kwa upande mwingine, maisha ni mwendo, muunganiko na viumbe wengine na utofauti wa maisha. Kwa (more…)