Category Archives: SHERIA ZA SIKU

#SheriaYaLeo (346/366); Mtazamo Wa Utoto.

By | October 12, 2022

#SheriaYaLeo (346/366); Mtazamo Wa Utoto. Kama tutakuwa wa kweli kuhusu maisha yetu, wengi wetu tutakubali kwamba hakuna jipya kwenye maisha yetu. Kila kitu kinaonekana cha kawaida na hakuna kinachotushangaza. Kuna kitu kikubwa tunajua kinakosekana kwenye maisha yetu, lakini ni vigumu kujua ni kipi hasa. Kujaribu kuondokana na hali hiyo, huwa (more…)

#SheriaYaLeo (345/366); Ona kwa ujumla.

By | October 11, 2022

#SheriaYaLeo (345/366); Ona kwa ujumla. Sisi binadamu huwa tuna tabia ya kuona vitu kwa utengano. Tunajiona sisi na wengine kama watu binafsi na waliojitenga badala ya kujiona kama kitu kimoja ambacho kimeungana. Huwa tunaiangalia dunia kwa utengano wa viumbe na vitu mbalimbali, badala ya kuangalia jinsi vyote vinavyokuwa vimeungana pamoja. (more…)

#SheriaYaLeo (344/366); Vuka ubinadamu na fikia uwezo usio na ukomo.

By | October 10, 2022

#SheriaYaLeo (344/366); Vuka ubinadamu na fikia uwezo usio na ukomo. Mara nyingi tunaishi kwenye hali ya ubinadamu ambayo huwa ina ukomo mkubwa. Tunakuwa tumezama kwenye mazoea yetu ya kila siku, ambayo yanatuzuia kufikia uwezo usio na ukomo wa ulimwengu. Wapo wanaojaribu kuondoka kwenye hali hiyo, lakini bado hawafanikiwi kwa sababu (more…)

#SheriaYaLeo (343/366); Ungana na kitu kikubwa kuliko wewe.

By | October 9, 2022

#SheriaYaLeo (343/366); Ungana na kitu kikubwa kuliko wewe. Mara nyingi changamoto tunazokutana nazo kwenye maisha huwa zinatupa msongo na hata sonona. Hilo huweza kututikisa kwa kiasi kikubwa na kutuzuia kufanya makubwa tunayotaka. Njia ya kuondoka kwenye hali hizo ni kuungana na kitu kikubwa kuliko wewe. Kwenye maisha yako kuna kipindi (more…)

#SheriaYaLeo (342/366); Kutembea na kifo.

By | October 8, 2022

#SheriaYaLeo (342/366); Kutembea na kifo. Watu wengi huwa wanaishi maisha yasiyo na maana na kupoteza muda kwa kuona wana muda mwingi wa maisha. Ni mpaka pale wanapokutana na hali ya kukabiliana na kifo, ndipo wanaiona thamani ya muda na kuutumia kwa uangalifu mkubwa. Kwa mfano mtu anapogundulika kuwa na saratani (more…)

#SheriaYaLeo (341/366); Muda hai au muda mfu?

By | October 7, 2022

#SheriaYaLeo (341/366); Muda hai au muda mfu? Muda ambao upo hai ndiyo kitu pekee unachokimiliki. Vitu vingine vyote ulivyonavyo unaweza kuvipoteza – familia yako, nyumba, magari, kazi na hata biashara. Muda ambao upo hai ndiyo kitu pekee kilicho ndani ya udhibiti wako. Jinsi ya kutumia muda wako, ni maamuzi yako (more…)

#SheriaYaLeo (340/366); Zamisha akili yako kwenye wakati uliopo.

By | October 6, 2022

#SheriaYaLeo (340/366); Zamisha akili yako kwenye wakati uliopo. Kutokutulia kwa akili zetu imekuwa ndiyo chanzo kikubwa cha kukosa umakini na kufanya makosa ambayo yanatugharimu sana. Kwa asili, akili yetu haiwezi kutulia sehemu moja, huwa inahama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Akili zetu ni rahisi sana kuhamishwa na usumbufu unaokuwa (more…)

#SheriaYaLeo (339/366); Ulimwengu upo ndani yako.

By | October 5, 2022

#SheriaYaLeo (339/366); Ulimwengu upo ndani yako. Kama unataka kuelewa ukubwa na ukuu wa ulimwengu usio na ukomo, anza kwa kuangalia ubongo wako. Ndani ya ubongo wako kuna miunganiko ya seli zaidi ya milioni bilioni moja. Kama ingebidi uhesabu miunganiko hiyo, mmoja kwa kila sekunde, ingekuchukua miaka milioni 32 kukamilisha. Ukiangalia (more…)

#SheriaYaLeo (338/366); Kiangalie kifo chako.

By | October 4, 2022

#SheriaYaLeo (338/366); Kiangalie kifo chako. Wengi wetu huwa tunatumia muda mwingi wa maisha yetu kujaribu kukiepuka kifo. Kifo ni kitu ambacho hakuna namna tunaweza kukikwepa, hivyo tunapaswa kukifikiria muda wote. Kwa kuelewa ufupi wa maisha yetu hapa duniani, inatufanya tuishi kwa kusudi na kuyaharakishia malengo yetu. Kujifunza kukubaliana na uhalisia (more…)

#SheriaYaLeo (337/366); Tukio ambalo huenda lisingetokea.

By | October 3, 2022

#SheriaYaLeo (337/366); Tukio ambalo huenda lisingetokea. Huwa tunayachukulia maisha kikawaida na kwa mazoea. Lakini tukitafakari kwa kina, ni tukio ambalo huenda lisingetokea. Tangu kuanza kwa maisha hapa duniani, mabilioni ya miaka iliyopita, kila tukio limekuwa linatokea kwa namna ambayo haiwezi kuelezeka. Hata wakati sisi binadamu tunajitenga na wanyama wengine na (more…)