Category Archives: SHERIA ZA SIKU

#SheriaYaLeo (336/366); Ulimwengu wa kushangaza na usio na ukomo.

By | October 2, 2022

#SheriaYaLeo (336/366); Ulimwengu wa kushangaza na usio na ukomo. Ulimwengu ni wa kushangaza na usio na ukomo. Katika kulielewa na kulisimamia hilo, jamii mbalimbali zimekuwa na tararibu zake. Ni taratibu ambazo zinalenga kuwafanya watu waweze kuyathamini maisha yao hapa duniani. Matambiko, ubatizo na hata taratibu nyingine za kimila, kifalsafa na (more…)

#SheriaYaLeo (335/366); Nenda mbele kwa kusudi.

By | October 1, 2022

#SheriaYaLeo (335/366); Nenda mbele kwa kusudi. Kwenye historia ya jeshi, kuna aina mbili za majeshi. Aina ya kwanza ni jeshi linalopigana kwa kusudi kubwa. Jeshi hilo huwa tayari kupambana kwa kila aina na hata kufia katika mapambano. Aina ya pili ni jeshi linalopigana kama sehemu ya kazi na kupata pesa. (more…)

#SheriaYaLeo (334/366); Mwendeshaji na farasi.

By | September 30, 2022

#SheriaYaLeo (334/366); Mwendeshaji na farasi. Uhusiano kati ya fikra na hisia zetu ni kama mwendesha farasi na farasi. Hisia zetu ni farasi na fikra zetu ni mwendesha farasi. Farasi ana nguvu kubwa, lakini bila ya kuongozwa vyema anaishia kuzunguka huku na huko na kutokuleta matokeo yoyote yenye tija. Hivyo ndivyo (more…)

#SheriaYaLeo (333/366); Jifunze kwenye zama zilizopita.

By | September 29, 2022

#SheriaYaLeo (333/366); Jifunze kwenye zama zilizopita. Vile tunavyoishi sasa ni matokeo ya mambo yaliyotokea kipindi cha nyuma. Mabadiliko yote ambayo binadamu tumeyapitia tangu enzi na enzi, ndiyo yamezalisha yote tuliyonayo sasa. Huwa tuna tabia ya kubeza zama zilizopita, kwa kuona zimepitwa na wakati. Kufanya hivyo kunatuzuia tusijifunze. Lakini pia ni (more…)

#SheriaYaLeo (332/366); Huwajui watu kama unavyodhani unawajua.

By | September 28, 2022

#SheriaYaLeo (332/366); Huwajui watu kama unavyodhani unawajua. Hatari kubwa uliyonayo ni kudhani unaweza kuwajua na kuwaelewa vizuri watu kwa mwonekano wa haraka wa nje. Watu wanaokuzunguka wamevaa sura ya kuigiza mbele yako, wakitaka waonekane kwa namna fulani, ambayo ni tofauti na uhalisia wao. Kama utakuwa haraka kukimbilia kuamua, utaishia kuamua (more…)

#SheriaYaLeo (331/366); Kuona unachotaka kuona.

By | September 27, 2022

#SheriaYaLeo (331/366); Kuona unachotaka kuona. Huwa tunapenda kuthibitisha mawazo ambayo tunayo, kwa kuonyesha kwamba ni sahihi. Hivyo tunajikuta tukitafuta ushahidi wa kuonyesha hilo. Tatizo linalokuja ni kwamba, ushahidi tunapata hauwi kweli, bali unakuwa ni upendeleo wa kile tunachotaka. Inapokuja kwenye kuthibitisha mawazo tuliyonayo, huwa tunaishia kuwa na upendeleo. Tunajikuta tukileta (more…)

#SheriaYaLeo (330/366); Geuza upendo binafsi kuwa huruma.

By | September 26, 2022

#SheriaYaLeo (330/366); Geuza upendo binafsi kuwa huruma. Huwa tunadhani tunawaelewa vizuri watu tunaojihusisha nao. Maisha yanaweza kuwa magumu na tuna majukumu mengi ya kukamilisha. Pia tu wavivu na tunapendelea kuwahukumu watu kwa mazoea. Lakini hayo yote siyo sahihi. Mafanikio yetu kwenye maisha yanategemea sana uwezo wetu wa kuwasoma na kuwaelewa (more…)

#SheriaYaLeo (329/366); Kaa kwenye kundi sahihi.

By | September 25, 2022

#SheriaYaLeo (329/366); Kaa kwenye kundi sahihi. Dhumuni la makundi mbalimbali ni kukamilisha majukumu, kufanya kazi, kutatua matatizo. Makundi yanakuwa na rasilimali muhimu ambazo zikitumika vizuri zinakuwa na tija kubwa. Lakini pia ndani ya kundi huwa kuna ushindani baina ya watu, ambao unaweza kuwasukuma watu kufanya zaidi. Kundi lenye afya huwa (more…)

#SheriaYaLeo (328/366); Sifia ukuu wa watu.

By | September 24, 2022

#SheriaYaLeo (328/366); Sifia ukuu wa watu. Kusifia ni kinyume na wivu – tunatambua mafanikio ya watu na kuyafurahia bila ya kujisikia vibaya. Tunakubali ubora wao kwenye sanaa au sayansi au biashara bila ya kupata maumivu. Hilo linaenda zaidi, katika kutambua ukuu wa wengine, tunasherekea uwezo wa juu kabisa wa jamii (more…)

#SheriaYaLeo (327/366); Pokea kila kinachokuja kwako.

By | September 23, 2022

#SheriaYaLeo (327/366); Pokea kila kinachokuja kwako. Kwenye safari yako ya maisha, kuna mengi yatakuja kwako ambayo ni tofauti kabisa na mategemeo yako. Kwenye hali kama hiyo ni rahisi sana kulalamika na kulaumu wengine kwa hayo unayokuwa unapitia. Lakini kufanya hivyo hakutasaidia chochote. Utaendelea kubaki kwenye hali hiyo hiyo. Kitu pekee (more…)