2609; Asili haipendi utupu.

By | February 21, 2022

2609; Asili haipendi utupu. Kama kuna kitu ambacho asili huwa haikipendi kabisa ni utupu. Safisha chumba chako vizuri kisha kifunge na kuondoka. Ukirudi utakuta kuna vitu vimejikusanya, vumbi, utando wa wadudu na vingine. Lima shamba lako na usipande chochote na haitachukua muda magugu mbalimbali yatakuwa yameota kwenye shamba hilo. Usipofanya (more…)

#SheriaYaLeo (113/366); Panda mbegu za mashaka.

By | February 21, 2022

#SheriaYaLeo (113/366); Panda mbegu za mashaka. Mashaka ni silaha yenye nguvu kubwa unayoweza kuitumia kumkabili adui. Unapovuruga sifa yake kwa kufanya watu wamtilie mashaka, anabaki na jukumu kubwa la kutunza sifa yake. Atajikuta njia panda katika kulikabili hilo. Akiamua kujitetea ili kuondoa mashaka hayo, bado kuna watu hawatamwamini. Wataona katika (more…)

2608; Mategemeo yako kwa wengine.

By | February 20, 2022

2608; Mategemeo yako kwa wengine. Kila mmoja wetu huwa ana mategemeo fulani kwa watu wengine. Lakini sehemu kubwa ya mategemeo hayo huwa siyo sahihi. Kwa sababu hatujui kile kinachoendelea ndani ya mtu. Unaweza kuwa unategemea mtu awe kwa namna fulani yeye akawa kwa namna ya tofauti. Ukadhani labda amefanya kwa (more…)

#SheriaYaLeo (112/366); Usiwaonee huruma maadui.

By | February 20, 2022

#SheriaYaLeo (112/366); Usiwaonee huruma maadui. Maadui zako hawakutakii mema. Kitu pekee wanachotaka kuona ni wewe ukishindwa na kuanguka kabisa. Hivyo watafanya kila mbinu kuhakikisha wanakamilisha hilo. Katika kukabiliana na maadui zako, kamwe usiwaonee huruma. Pale unapoelekea kuwashinda wanaweza kutumia mbinu hiyo ya kutaka huruma kwako. Kwa kuonyesha wamesalimu amri na (more…)

2607; Kama siyo maamuzi ya kufa na kupona.

By | February 19, 2022

2607; Kama siyo maamuzi ya kufa na kupona. Kuna maamuzi ya kufa na kupona, maamuzi ambayo ukikosea yana madhara makubwa na huwezi kuyabadili tena. Hayo ni maamuzi machache sana kwenye maisha na utakutana nayo mara chache mno katika kipindi chote cha maisha yako. Lakini kwenye maisha ya kila siku, maamuzi (more…)

#SheriaYaLeo (111/366); Watu wanakuchukulia vile unavyojiweka.

By | February 19, 2022

#SheriaYaLeo (111/366); Watu wanakuchukulia vile unavyojiweka. Jinsi unavyojiweka ndivyo watu wanavyokuchukulia. Kama unajithamini na kujiheshimu, watu pia watakuthamini na kukuheshimu. Kama unajidharau na kutokujithamini, hivyo pia ndivyo watu watakavyokuchukulia. Ukijiweka wa kawaida na wa bei rahisi, hivyo ndivyo watu watakavyokuchukulia, kwa ukawaida kabisa. Wote wanaoheshimiwa sana na kuthaminiwa ni kwa (more…)

2606; Washindani siyo shida.

By | February 18, 2022

2606; Washindani siyo shida. Watu wengi huona ushindani ni hatari kubwa kwenye biashara, au kitu kingine chochote. Huona uwepo wa washindani utawaondoa kabisa kwenye kitu hicho. Kufa kwa biashara au kitu chochote kile huwa hakusababishwi na udhindani, bali ni udhaifu wa ndani. Japo kwa nje ushindani ndiyo utaonekana umesababisha, lakini (more…)

#SheriaYaLeo (110/366); Sifia kwa umakini.

By | February 18, 2022

#SheriaYaLeo (110/366); Sifia kwa umakini. Njia nzuri ya kukubalika na wale walio juu yako ili wakupe fursa nzuri za kupata kile unachotaka ni kuwasifia. Sisi binadamu huwa tunapenda sana kusifiwa, inatufanya tujione ni wa muhimu sana. Lakini unapaswa kuwa makini sana kwenye kusifia kwako, kwani ni rahisi mtu kuona unamsifia (more…)

#SheriaYaLeo (109/366); Watoe maadui mafichoni.

By | February 17, 2022

#SheriaYaLeo (109/366); Watoe maadui mafichoni. Unaweza kuwa na maadui ambao wamejificha. Ambao kwa nje wanaonekana kama marafiki, lakini kwa ndani wana uadui mkubwa. Wanakuwa wanasubiri wapate fursa ili wakumalize. Na kwa kuwa hujui, basi inakuwa rahisi kwako kuwapa fursa ya kutimiza lengo lao. Katika safari ya mafanikio, adui usiyemjua ni (more…)