1703; Siyo Kinacholipa Zaidi…

By | August 30, 2019

Huwa tunakuana na fursa mbalimbali kwenye maisha yetu. Ili kuchagua ni fursa ipi mtu utaifanyia kazi, watu wamekuwa na vigezo mbalimbali wanavyotumia. Na wengi hutumia kigezo cha malipo, huwa wanachagua ile fursa ambayo inawalipa zaidi, kitu ambacho siyo kibaya kwa sababu nani asiyependa fedha? Lakini katika kuchagua kile kinacholipa zaidi, (more…)

1702; Watu Wasiosaidika…

By | August 29, 2019

Unaweza kuwa unakazana sana kuwasaidia watu, lakini huoni matokeo mazuri. Hilo linaweza kukushangaza usielewe kwa nini mtu apinge msaada ambao unampa kwa kujitoa zaidi wewe. Unachopaswa kujua ni kwamba kuna watu ambao hawasaidiki, hata ufanye nini. Hivyo ni muhimu kuwajua mapema kabla hujapoteza muda, nguvu na hata fedha zako kuwasaidia (more…)

1701; Siyo Kitu Cha Kijinga…

By | August 28, 2019

Ukiona mtu aliyepiga hatua kuliko wewe anafanya kitu kwa kukirudia rudia, jua kina manufaa fulani kwake. Hata kama hukubaliani na mtu huyo au kile anachofanya, jua kabisa kile anachofanya siyo kitu cha kijinga. Kina manufaa fulani ndiyo maana anakifanya. Na wewe unaweza kujifunza na ukakifanya pia, au ukakifanya kwa ubora (more…)

1700; Kushindwa Ni Tabia…

By | August 27, 2019

Kushindwa hakutokei mara moja, siyo ajali. Kushindwa ni matokeo ya tabia ambazo mtu anakuwa amejijengea na kuzirudia rudia kwa muda mrefu. Hakuna mtu anaamka siku moja na kujikuta kwenye madeni makubwa, bali ni tabia ambayo inatengenezwa kidogo kidogo na baadaye inakuwa kubwa. Hakuna mtu anaamka siku moja na kujikuta ana (more…)

1699; Umaarufu Hewa…

By | August 26, 2019

Siku hizi kila mtu anataka kuwa maarufu. Na umaarufu wenyewe sasa unachekesha sana. Kwa sababu ni umaarufu hewa, umaarufu ambao hauna msingi, umaarufu ambao upepo ukivuma tofauti basi unapotezwa kabisa. Tunapenda umaarufu kwa sababu tunajua utatupa ‘koneksheni’, utatufungulia baadhi ya milango kwa sababu unapokuwa unajulikana ni rahisi kupata baadhi ya (more…)