1568; Hakuna Tatizo Linaloanza Likiwa Kubwa…

By | April 17, 2019

Kila mmoja wetu amekuwa anakutana na matatizo mbalimbali kwenye maisha yake. Na matatizo mengi huanza kusumbua pale yanapokuwa makubwa. Lakini ukweli ni kwamba, hakuna tatizo linaloanza likiwa kubwa. Hakuna mtu anaamka siku moja na kujikuta kwenye deni la mamilioni. Hakuna tu anaamka siku moja na kujikuta ana uzito uliopitiliza. Na (more…)

1567; Udhibiti Mkubwa Bado Upo Ndani Yako…

By | April 16, 2019

Zama tunazoishi ni zama ngumu sana kwa fikra zetu sisi binadamu. Ni zama ambazo watu wenye ushawishi wanaonekana kuweza kuigawa jamii kama watakavyo. Wale wanaopata nafasi za uongozi au kupata ushawishi kwa njia nyingine, wanaonekana kuwa na nguvu ya kuweza kuibua hisia kali ndani ya watu na kuwagawa. Mitandao ya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; ANGALIA KISABABISHI NA MATOKEO…

By | April 16, 2019

“Pay close attention in conversation to what is being said, and to what follows from any action. In the action, immediately look for the target, in words, listen closely to what’s being signaled.” —MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 7.4 Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi (more…)

1566; Utampigia Nani Kura Leo…

By | April 15, 2019

Tukisikia kupiga kura huwa tunafikiria kipindi cha uchaguzi pekee. Lakini maisha yetu ya kila siku ni uchaguzi, kila siku tunajikuta kwenye sanduku la kupiga kura. Lakini wengi hatuelewi hili na ndiyo maana tunafanya maamuzi ambayo ni mabovu. Kila mtu ana kampeni anayopiga kwako. Wapo wanaotaka fedha ulizonazo, hivyo wanakupa matangazo (more…)

1565; Hakuna Anayefanya Kitu Mara Moja…

By | April 14, 2019

Inapotokea mtu amefanya kitu ambacho hukutegemea afanya, labda ni wizi, udanganyifu au usaliti, utetezi wao wa kwanza huwa ni kwamba ndiyo mara ya kwanza kwao kufanya na hawatarudia tena kufanya. Kama tunawaamini sana watu hawa inakuwa rahisi kukubaliana nao, na kuona kweli labda ndiyo mara ya kwanza wamefanya au kujaribu. (more…)

1564; Acha Kuisikiliza Dunia…

By | April 13, 2019

Nikuulize swali, ni mara ngapi umekuwa na sauti ndani yako inakuambia ufanye kitu fulani, lakini dunia inakuambia ufanye tofauti, unaifuata dunia na unapata matokeo ambayo siyo uliyotegemea? Jibu ni mara nyingi, kila mmoja wetu amewahi kukutana na hali hizi, sauti ya ndani inakuambia ufanye X, dunia inakuambia ufanye Y, na (more…)