UKURASA WA 735; Matatizo Yako Siyo Matatizo Yao…

By | January 4, 2017

Watu wana matatizo yao, na wewe una matatizo yako, unachopaswa kuelewa vizuri kabisa ni kwamba matatizo ya watu siyo matatizo yako. SOMA; Watu Wana Matatizo Yao, Hawataki Kusikia Yako…. Na hapa tunakwenda kuzungumzia kwenye upande wa kazi na biashara. Kumekuwa na mazoea ya mfanyabiashara au mtoa huduma kutumia matatizo yake (more…)

UKURASA WA 734; Kipimo Cha Misingi Sahihi Kwako…

By | January 3, 2017

Je utajuaje kama misingi unayofuata kwenye kazi zako, biashara zako na hata maisha yako kwa ujumla ni misingi sahihi? Hili ni swali ambalo watu wengi wamekuwa hawapati nafasi ya kujiuliza na hivyo kupelekea kujikuta wakifuata misingi ambayo siyo sahihi na baadaye kuanguka. Watu wengi wamekuwa hawajiulizi swali hili kwa sababu (more…)

UKURASA WA 733; Wakati Sahihi Wa Kufanya Mabadiliko Ni Huu…

By | January 2, 2017

Pale mambo yanapokwenda vizuri, sisi binadamu tuna tabia ya kujisahau, tunaanza kuona mambo yanakwenda vizuri kwa sababu labda sisi ni wajanja sana, au labda tuna bahati sana, au sisi ni zaidi ya wale ambao mambo yao hayaendi vizuri. Tunapojisahau hivi kwa muda mrefu, tunakuja kustuka mambo yakiwa hayaendi vizuri kama (more…)

UKURASA WA 732; Tatizo Siyo Mipango, Tatizo Ni Ustahimilivu Wa Mipango…

By | January 1, 2017

Kila mtu ana mpango, mpaka pale mambo yanapokwenda tofauti na alivyotarajia. Hakuna mtu anafanya kitu bila ya mpango wowote, hata kama hajaandika vizuri, lakini ndani ya mawazo yake, ana mpango fulani wa namna atakavyokwenda na kile anachofanya. SOMA; Mipango Siyo Matumizi… Watu wanakuwa na mipango mizuri ya kibiashara, namna itakavyokuwa (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; NITAANZA MWAKA MPYA…

By | December 31, 2016

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo makubwa. Tutumie nafasi hii vizuri rafiki. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu NITAANZA MWAKA MPYA. Siku chache zilizopita nilikuwa na marafiki tukifanya mazungumzo mbalimbali kuhusu maisha. Tukafika eneo la (more…)

UKURASA WA 731; Sababu Moja Ya Kukufanya Uingie Au Uendelee Kubaki Kwenye Biashara Yako…

By | December 31, 2016

Tunaishi kwenye kipindi ambacho kuna fursa nyingi za kibiashara kuliko wakati mwingine wowote. Mtu aliyeishi miaka 200 iliyopita, akipata nafasi ya kurudi duniani leo, atashangazwa sana na fursa hizi zilizopo sasa. Zamani ilikuwa kuingia kwenye biashara siyo kitu rahisi, mazingira yalikuwa magumu, ushindani mkali na masoko madogo. Lakini sasa hivi (more…)

💥#TAFAKARI YA LEO; HAPO ULIPO SASA.

By | December 30, 2016

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa kwenye kile ambacho tumechagua kufanya. Tukumbukenya kwamba muda ndiyo rasilimali muhimu sana kwetu, tuutumie muda wetu vizuri. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu HAPO ULIPO SASA, HAPO ULIPO SASA ndipo (more…)

UKURASA WA 730; Hiki Ndiyo Wanachokiamini Watu…

By | December 30, 2016

Ili ufanikiwe, unahitaji watu ambao wanakuamini. Watu ambao wanakuamini na kuweza kukuajiri. Watu ambao wanakuamini na kuweza kununua kile ambacho unauza. Watu ambao wanakuamini na kuweza kusoma kile unachoandika. Watu ambao wanakuamini na kufanya kile unachowaambia wafanye. Unahitaji sana watu wakuamini, lakini shida inaanzia hapa. Hakuna mtu yeyote ambaye anakuamini (more…)

UKURASA WA 729; Kitu Pekee Kitakachokuletea Utajiri Kwenye Maisha Yako Ni Hiki…

By | December 29, 2016

Kuhusu utajiri tu, mengi yanasemwa, mengi yanaandikwa na kila mtu ana lake la kusema. Lakini kama ujuavyo, maoni ni mengi ila ukweli ni mmoja. Na kwa kuwa mara nyingi ukweli huwa unaumiza, wengi hawapendi kuusikia na hivyo kukimbilia maoni. Utasikia watu wakikuambia lima zao fulani utakuwa tajiri, au fuga kitu (more…)

UKURASA WA 728; Sababu Halisi Ya Watu Kukuambia HAPANA…

By | December 28, 2016

Kama kuna neno utakalolisikia mara nyingi pale unapochagua maisha ya mafanikio basi ni HAPANA. Kuna mambo mengi ambayo utakuwa unataka kufanya lakini wengine wanakuambia hapana. Kuna biashara nzuri utakazokuwa umeanzisha lakini wale ambao utakuwa umewafikiria kuwa wateja wako watakuambia hapana. Unaweza kuwa na wazo zuri ambalo unahitaji watu wakuunge mkono, (more…)