UKURASA WA 744; Acha Kucheza Michezo Ya Wengine…

By | January 13, 2017

Maisha ni mchezo mkubwa ambao kuna michezo mingi midogo midogo ndani yake. Kuna michezo ya kazi, michezo ya biashara, michezo ya maisha ya kifamilia na mingineyo. Sasa kuna ambao wanaingia kwenye mchezo, kwa kuchagua kufanya vile vitu muhimu kwenye maisha, kama kazi na biashara, na kuna ambao wanakaa kuuangalia tu (more…)

UKURASA WA 743; Utengano Ni Muhimu Kwa Mafanikio Yako…

By | January 12, 2017

Kutoka hapo ulipo sasa na kufika kwenye ndoto ya maisha yako, kuna vitu unahitaji kutengana navyo. Yaani kuna vitu ambavyo lazima uviache ili uweze kufika kule unakotaka kufika. Hili ni somo muhimu ambalo watu wengi wamekuwa hawalielewi. Ndiyo maana mabadiliko yanakuwa magumu sana kwa watu wengi. Kwa sababu wanachotaka wao (more…)

UKURASA WA 742; Kufanya Mara Moja Moja Na Kufanya Kila Siku…

By | January 11, 2017

Kuna vitu ambavyo huwa tunafanya mara moja moja kwenye maisha yetu, halafu kuna vile vitu ambavyo huwa tunavifanya kila siku. Katika vitu hivi vya aina mbili, unafikiri vipi vyenye nguvu kwetu? Vipi ambavyo vinayajenga maisha yetu? Maisha yetu yapo pale yalipo sasa, kutokana na tabia ambazo tunazo, na tabia yoyote (more…)

UKURASA WA 741; Mafanikio Ya Wengine Ndiyo Mafanikio Yako…

By | January 10, 2017

Mara nyingi tunapofikiria mafanikio, huwa tunajiangalia sisi wenyewe sana. Huwa tunaangalia namna gani tufanikiwe au vikwazo gani vinatuzuia kufanikiwa. Tunakazana kujiangalia wenyewe na bado tunashindwa kufanikiwa. Hii ni kwa sababu mafanikio yetu siyo sisi wenyewe, bali mafanikio yetu ni mafanikio ya wengine. SOMA; Mafanikio Yoyote Yanaanza Na Mtu Mmoja… Kabla (more…)

UKURASA WA 740; Unahitaji Changamoto Ili Ufanikiwe….

By | January 9, 2017

Hakuna siku ambayo inaweza kupita na usiwe na changamoto yoyote kabisa. hata kama itakuwa siyo kubwa basi inaweza kuwa ndogo. Mfano unataka kuwahi mahali halafu njiani ukakuta foleni ni ndefu na hivyo usiweze kufika kwa wakati. Au kuna mtu ulitegemea atimize wajibu wake na yeye hajatimiza. Kwa asili binadamu tunaona (more…)

UKURASA WA 739; Uhuru Pia Unatokana Na Uvumilivu Wa Wengine…

By | January 8, 2017

Ni kawaida kwetu binadamu kuona kwamba kile tunachoamini sisi ndiyo sahihi, na wale ambao wanaamini tofauti na tunavyoamini sisi wanakosea. Kwa hali hii kuna watu wamekuwa wanatumia muda mwingi kuwapinga wengine badala ya kutumia muda huo kuhakikisha wanakuwa bora zaidi. Watu wote hawawezi kuamini kitu kimoja, au kukubaliana kwenye kila (more…)

UKURASA WA 738; Huhitaji Kila Mtu, Unahitaji Watu Sahihi…

By | January 7, 2017

Sasa hivi karibu kila kitu kimefanywa kuwa demokrasia. Zile enzi za kitu kimoja kukubaliwa na watu wote zimeshapitwa na wakati na hazitarudi tena. Kuanzia kwenye biashara, kazi, huduma na hata maisha kwa ujumla, hakuna kitu kimoja ambacho kinaweza kukubalika na kila mtu. Ila kila kitu kina watu wake sahihi. Lakini (more…)

UKURASA WA 737; Watu Wanakuangalia Zaidi Ya Kukusikiliza….

By | January 6, 2017

Wewe kama mzazi, kiongozi, mwajiri au hata mfanyakazi, kuna namna ambavyo unataka watu wawe, kuna mambo ambayo unataka watu wafanye, kwa sababu unajua ni muhimu kwa mafanikio yao na yako pia. Hivyo unaweza kuchukua muda wako kuwaambia na kuwahubiria namna wanavyopaswa kufanya na kubadilika. Lakini kama umewahi kujaribu hili najua (more…)

UKURASA WA 736; Zipo Fedha Za Kutosha Kila Mtu Kuwa Bilionea…

By | January 5, 2017

Moja ya vitu ambavyo vinayajenga maisha yetu ni ile imani ambayo tunayo juu ya maisha yetu kwa ujumla. Vile tunavyoamini yanayowezekana na yasiyowezekana, ndivyo tunavyofanyia kazi. Kwenye jamii zetu, imani kubwa ya watu, hasa linapokuja swala la fedha ni ile imani ya uhaba. Tumeaminishwa kwamba chochote tunachotaka basi kina uhaba, (more…)