BIASHARA LEO; Tofauti Ya Kutangaza Biashara Yako Na Kupiga Kelele.

By | March 17, 2016

Watu wengi wanaofikiri wanatangaza biashara zao, ukweli ni kwamba wanapiga kelele. Kabla hatujaendelea ni vyema tukajua kelele ni nini, ili tuone unahusianaje na wale wanaotangaza biashara. Kelele ni sauti zisizo na mpangilio au sauti zisizohitajika kwa mahali husika au wakati husika. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakiwapigia watu wengi kelele kuhusu biashara (more…)

UKURASA WA 442; Mwalimu Yupo Hapo Ulipo.

By | March 17, 2016

Kila kitu kinachoendelea kwenye maisha yako ni mwalimu wako. Hali yoyote unayopitia, changamoto zozote unazokutana nazo, hawa ni walimu kwako na wamekuja na masomo muhimu sana unayotakiwa kuyazingatia. Unapompoteza mtu unayempenda, au ambaye ni muhimu sana kwako, tukio hili ni mwalimu kwako. Na linakupa funzo kubwa sana kwamba hutakuwa na (more…)

BIASHARA LEO; Sababu Ya Mteja Wako Kwenda Kwa Mshindani Wako.

By | March 16, 2016

Njia bora sana ya kuifikiria biashara yako, ni wewe mmiliki wa biashara kuvaa viatu vya mteja wako. Hebu fikiria kama wewe ndiyo ungekuwa mteja wa biashara hiyo unayoifanya wewe, je ungeendelea kuwa mteja wa biashara hiyo? Na unapofanya hivi usijaribu kujidanganya, ondoa hisia za kujipendelea na fikiri kwa kina. Kwa (more…)

VITU 100 AMBAVYO KILA MJASIRIAMALI ANATAKIWA KUJUA NA KUFANYA ILI KUFANIKISHA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA.

By | March 16, 2016

Je wewe ni mjasiriamali? Au unataka kuingia kwenye ujasiriamali? Kuna mambo muhimu sana unayotakiwa kujua katika safari yako ya ujasiriamali. Bila ya kujua mambo haya utajikuta kwenye wakati mgumu na hata kukata tamaa, kwa sababu ujasiriamali sio safari rahisi kama wengi ambao bado hawajaingia wanafikiri. Karibu tujifunze mambo 100 ambayo (more…)

UKURASA WA 441; Dunia Inakusoma Tu…

By | March 16, 2016

Wanasema vitendo vinaonekana zaidi kuliko maneno yanavyosikika. Kwamba unaweza kusema sana, lakini watu wataona zaidi vitendo vyako. Dunia inakusoma kwa kila unachofanya. Unaiambia dunia unachoamini na unachosimamia kupitia matendo yako ya kila siku. Kuwa mtu wa kulalamika na kulaumu na unaidhihirishia dunia kwamba huna mamlaka juu ya kitu chochote kile, (more…)

BIASHARA LEO; Majukumu Makubwa Matano Kwa Kila Mmiliki Wa Biashara Kuzingatia.

By | March 15, 2016

Watu wengi hufikiri biashara ni kwenda kununua vitu kwa bei ya jumla, kuja kuviweka kwenye eneo lako la biashara na kuuza kwa reja reja. Unakaa eneo lako la biashara na mtaja akipita anaona upo pale unauza, anakuja, anauliza bei unamjibu, akitaka kununua unampa, kama asipotaka anaondoka. Au wengine wanafikiri ukishakuwa (more…)

ONGEANA COACH; Nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi.

By | March 15, 2016

Habari rafiki yangu? Unaendeleaje na harakati za kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi? Nina hakika uko vizuri na licha ya changamoto na vikwazo ulivyopitia, bado hujakata tamaa, unaendelea kuweka juhudi kwa sababu unajua ni kitu gani unataka kwenye maisha yako na unajua kuwa utakipata. Lakini pia huenda umejaribu na kukutana (more…)

UKURASA WA 440; Jinsi Ya Kumpata Mtu Sahihi Kwako…

By | March 15, 2016

Kumpata mtu sahihi ni changamoto ambayo watu wengi sana wamekuwa wakikutana nayo. Inawezekana kuwa unatafuta mtu sahihi wa kufanya naye kazi, au biashara. Au pia unatafuta mtu sahihi wa kuishi naye kama mwenza wa maisha. Huwa tunaweka sifa na vigezo mbalimbali na kisha kuanza kutafuta ni nani sahihi anayeweza kuendana (more…)

Matumizi ya mitandao ya kijamii kwenye ukuaji wa biashara yako.

By | March 14, 2016

Hakuna anayeweza kukataa kwamba dunia inabadilika, na sio tu kwamba inabadilika, bali inabadilika kwa kasi kubwa sana. Mtandao wa intaneti umegusa kila eneo la maisha, na kwenye biashara ndio umegusa kila eneo la biashara. Wakati mtandao wa intaneti unaanza kukua na kusambaa kwa kasi, watu wengi walifikiri ni kitu ambacho (more…)

UKURASA WA 439; Hasira Na Huzuni…

By | March 14, 2016

Hizi ni hisia mbili hasi ambazo zinaweza kuleta madhara makubwa sana kwenye maisha yako, kama utashindwa kujua jinsi ya kwenda nazo vyema. Hasira na huzuni. Tunaishi kwenye dunia yenye utata wa hali ya juu, tungependa mambo yawe rahisi na mazuri kama tunavyotegemea lakini hayaendi hivyo. Tunapenda watu wawe kama vile (more…)