UKURASA WA 403; Furaha Ipo Kwenye Mchakato, Sio Mwisho.

By | February 7, 2016

Moja ya vitu ambavyo dunia imekuwa inatudanganya sana, na tunadanganyika ni kwamba furaha ipo mwisho. Yaani teseka sasa na baadaye utakuwa na furaha, baada ya kufikia kile ambacho unakitafuta au kukifanyia kazi. Huu ni uongo, na ndio imesababisha maisha ya wengi kuendelea magumu hata baada ya kupata kile ambacho wamekuwa (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; Why Motivating People Doesn’t Work And What Does. (Sayansi Mpya Ya Hamasa Na Uongozi)

By | February 6, 2016

Kitabu WHY MOTIVATING PEOPLE DOESN’T WORK, kinaangalia kwa undano sayansi ya hamasa. Katika kitabu hiki tunajifunza mbinu mpya za kuwafanya watu wahamasike na kuchukua hatua zaidi. Kupitia kitabu hiki mwandishi Susan Fowler anatukumbusha kwamba huwezi kumhamasisha mtu, kwa sababu kilamtu tayari amehamasika. Unachoweza kufanya ni kujua mtu amehamasika kwenye nini (more…)

UKURASA WA 402; Tunavyopoteza Dakika Na Tunavyopoteza Masaa…

By | February 6, 2016

Kuna njia mbili za kupoteza muda. Njia ya kwanza ni kupoteza dakika na njia ya pili ni kupoteza masaa. Ni njia tofauti kwa sababu upotevu wa muda unatofautiana kwenye njia hizo. Tunapoteza dakika kwa bahati mbaya, bila ya kujua, yaani ni kama zinatuponyoka. Na ni vigumu sana kujua kwa hakika (more…)

BIASHARA LEO; Njia Bora Ya Kutatua Mgogoro Kati Yako Na Mteja Wako.

By | February 5, 2016

Karibu tena kwenye makala hizi za biashara leo ambapo tunapeana mbinu za kuboresha biashara zetu zaidi. Na leo tutaangalia njia bora ya kutatua mgogoro unaoweza kuibuka kati yako na mteja wako. Kama ambavyo tumeshaona kwenye makala zilizopita, mara zote mteja yupo sahihi, na kama kuna ushindani wowote kati yako na (more…)

UKURASA WA 401; Tatizo La Machaguo Mengi.

By | February 5, 2016

Tunaishi kwenye dunia ambayo kuna machaguo mengi sana. Kwa kitu chochote unachotaka kufanya, kuna njia nyingi mbadala za kukuwezesha kufanya au kufikia kitu hiko. Kwa jicho la kawaida unaweza kusema kwa kuwa na machaguo haya mengi ni maendeleo na inaturahisishia maisha. Lakini ukiangalia kwa jicho halisi, huo sio ukweli. Kuwepo (more…)

BIASHARA LEO; Mteja Njoo Na ‘Chenji’ Yako.

By | February 4, 2016

Utawasikia wafanyabiashara wengi wadogo wakilalamika kwamba biashara ni ngumu sana. Watakupa kila sababu kwa nini biashara zao hazisongi mbele. Na unaweza ukakubaliana nao kabisa. Ila sasa nenda kwenye biashara hiyo asubuhi, nenda na noti ya shilingi elfu kumi na unataka kitu cha shilingi mia tano. Unaweza hata ukatukanwa, mfanyabiashara atakushangaa (more…)

Jinsi ya kujua biashara bora kwako kufanya kwa mtaji wowote unaoweza kuanza nao.

By | February 4, 2016

Moja ya maswali ambayo huwa napokea kila mara kutoka kwa wasomaji ni biashara gani mtu afanye kwa mtaji fulani ambao anao. Huwa napokea ujumbe labda nina mtaji wa milioni moja, nifanye biashara gani? Hili ni swali ambalo huwa linawatatiza wengi hasa wale ambao ni wageni kabisa kwenye biashara. Pamoja na (more…)

UKURASA WA 400; Maana Halisi Ya Neno SIWEZI…

By | February 4, 2016

SIWEZI, kama yalivyo maneno mengine mengi ambayo watu hupenda kutumia hasa katika safari ya mafanikio, ni neno ambalo linatumika kuficha hali halisi. Ukweli ni kwamba siwezi siyo neno linalosimama lenyewe, ni neno linaloficha vitu vingine ambavyo mtu anavyo. Na mara nyingi neno hili SIWEZI, halina uhalisia kwa yule anayelitumia. Japo (more…)

BIASHARA LEO; Hisia Zako Weka Mbali Na Biashara.

By | February 3, 2016

Sisi binadamu ni viumbe wa hisia, japo tunapenda kufikiri kwa mantiki, lakini bado maamuzi yetu mengi tunayafanya kwa hisia. Hisia ni nzuri sana katika kujenga mahusiano mazuri, lakini ni mbaya sana katika kufanya maamuzi. Mara nyingi maamuzi unayofanya kwa hisia huishia kuwa ni maamuzi mabaya na yanayokugharimu kwakiasi kikubwa, iwe (more…)

KITABU; Kurasa Za Maisha Ya Mafanikio, Nidhamu Uadilifu Na Kujituma.

By | February 3, 2016

Kuna mambo matatu muhimu sana kila mmoja wetu anatakiwa kujua kuhusu maisha, ili kuweza kuwa na maisha bora na yenye mafanikio. Na hapa mafanikio ni vile wewe unavyoyaona maisha yako kwa ubora, vile wewe unavyotamani maisha yako yawe na vile ambavyo ndoto zako kubwa kwenye maisha zilivyo. Jambo la kwanza (more…)