UKURASA WA 264; Mchakato Na Matokeo.

By | September 21, 2015

Tunapoangalia mafanikio ya watu wengine, mara nyingi huwa tunaona matokeo. Alianza kuuza karanga na sasa anamiliki mahoteli… Alianza kuuza chipsi na sasa anamiliki viwanda… Alikuwa hana pa kulala ila sasa ni tajiri. Ni hadithi nzuri sana hizi kuzisikia, zinatia moyo na ninatupa uhakika kwamba inawezekana. Tatizo kubwa ni kwamba watu (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Nguvu Moja Unayomiliki Yenye Uwezo Wa Kuibadili Dunia.

By | September 20, 2015

Karibu tena kwenye makala ya wiki hii ya FALSAFA MPYA YA MAISHA. Naamini umekuwa unajifunza na kujijengea maisha mapya kupitia falsafa hii ambayo tunaitengeneza. Kama ambavyo tumeshajifunza, iwe unajua au hujui, unaishi falsafa fulani. Sasa kama unaishi falsafa ambayo huijui ni vigumu sana kuwa na maisha ya furaha na mafanikio. (more…)

UKURASA WA 263; Kama Sio Ngumu Ni Laini.

By | September 20, 2015

Kama sio ngumu ni laini… Kama sio moto ni baridi… Kama sio haraka ni polepole… Kama sio nyeupe ni nyeusi…. Hivi ndivyo mafanikio yanavyokwenda, ni unafanya kinachokupeleka kwenye mafanikio au hufanyi na hakuna hali ya kati kati, kwamba najiandaa kwamba nitaanza. Chochote unachofanya, kipe kila kitu ulicho nacho au achana (more…)

UKURASA WA 260; Kabla Hujasema Ndiyo….

By | September 17, 2015

Wote tunakubaliana kwamba hatuwezi kufanya kila kitu ambacho tunatamani kufanya. Na pia hatuwezi kukubali kila kitu kinachokuja mbele yetu. Hii ni kwa sababu tuna mambo mengi na muhimu ya kufanya na wakati huo huo muda sio rafiki kwetu. Hivyo basi tunahitaji kuwa makini sana ni wakati gani wa kusema NDIYO (more…)

UKURASA WA 259; Kwa Nini Hujiheshimu?

By | September 16, 2015

Ili watu wakuheshimu ni lazima wewe mwenyewe kwanza ujiheshimu. Ili ufikie mafanikio makubwa kwenye maisha yako ni lazima ujiheshimu. Lakini watu wengi wamekuwa hawajiheshimu, na hii imekuwa inawazuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Na kujiheshimu ninakozungumzia hapa hakuishii tu wewe kuwa mtu mwema na kuwa na maadili mazuri. Bali (more…)

MAMBO 20 NILIYOJIFUNZA KWNEYE KITABU THE LUNCH TIME TRADER.

By | September 15, 2015

Kitabu THE LUNCH TIME TRADER ni kitabu kinachofundisha jinsi ya kufaidika na uwekezaji kwenye soko la hisa. Kupitia kitabu hiki unajifunza mbinu za kununua na kuuza hisa ili kuweza kupata faida kubwa. Kuna mengi mazuri kwenye kitabu hiki, ila hapa nitakushirikisha sababu 20 kwa nini uwekeze kwenye kununua hisa. SABABU (more…)

UKURASA WA 258; Moja Ni Bora Kuliko Sifuri.

By | September 15, 2015

Watu wengi wamekuwa wakiweka mipango mizuri na mikubwa sana kwenye maisha yao. Ila katika utekelezaji hujikuta wanakwama. Chanzo kikubwa cha kukwama huwa ni kutaka kufanya mambo hayo yote makubwa kwa wakati mmoja au kwa muda mfupi. Lakini haijawahi kutokea sehemu yoyote kwenye maisha yetu mambo yakaenda haraka kama tunavyotarajia. Kila (more…)

UKURASA WA 257; Ihesabu Leo Kuwa Siku.

By | September 14, 2015

Zaidi ya nusu ya vitu utakavyopanga kufanya leo kuna uwezekano mkubwa hutaweza kuvifanya, hutapata nafasi ya kuvifanya. Zaidi ya nusu ya vitu utakavyotaka kusoma leo, hutaweza kuvisoma. Zaidi ya nusu ya vitu utakavyosema NDIO leo hutaweza kuvitimiza. Vipindi vya tv utakavyopanga kuangalia leo hutapata muda huo. Kwa kifupi ni kwamba (more…)