UKURASA WA 272; KESHO….

By | September 29, 2015

Kesho ni siku ambayo haijawahi kufikiwa. Kesho ni mwizi wa ndoto kubwa za watu wengi. Kesho ni njia ambayo umekuwa unatumia kutoroka matatizo yako. Kesho ni siku ambayo inapatikana kwenye kalenda ya wajinga, hakuna kalenda yoyote duniani imeandikwa kesho. Lakini tunaipenda kesho, tunaitumia kesho kila mara, na bado hatujawahi kuifikia (more…)

Mambo muhimu ya kuzingatia pale unapoanza biashara na mtaji mdogo.

By | September 28, 2015

Moja ya maswali ambayo huwa napokea sana kutoka kwa watu wanaotaka kuanza biashara huwa ni biashara gani waanze kwa mtaji kidogo wanaokuwa nao. Mfano wa swali huwa, “nina laki tano, naweza kuanza biashara gani kwa kiasi hiki cha fedha?” swali hili huwa linaulizwa mara nyingi sana kwa viwango vidogo na (more…)

UKURASA WA 271; Unachoweza Kufanya Baada Ya Kushindwa.

By | September 28, 2015

Pamoja na malengo na mipango mizuri ambayo unaiweka kabla ya kuanza kufanya jambo lolote, bado huna uhakika wa asilimia 100 kwamba utafanikisha kufanya. Na nafasi ya kushindwa ni kubwa kuliko ya kushindwa. Kwa kifupi utashindwa, katika baadhi ya mambo ambayo utakuwa umepanga kufanya. Sasa kushindwa sio tatizo, ila kinachotokea baada (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Jinsi Ya Kuimarisha Falsafa Yako Mpya Ya Maisha.

By | September 27, 2015

Habari mwanafalsafa? Ndio, wewe ni mwanafalsafa, na wala huhitaji kusubiri mpaka mtu akuite hivyo. Chimbuko la neno falsafa au kwa kiingereza philosophy ni neno la kigiriki filosofia ambalo maana yake ni kupenda busara/hekima. Kwa kifupi ni kupenda kujifunza na kufikiri zaidi juu ya kile kitu unachofanya au vile unavyoishi. Kwa (more…)

UKURASA WA 270; Mafanikio Ya Kushikiza Kwenye Vitu.

By | September 27, 2015

Jamani hii ni vita, Halafu ni safari ndefu sana. Halafu maisha yako ndio haya, huwezi kuyasimamisha uje uyaishi baadae. Mara nyingi tunapozungumzia mafanikio, watu huwa na picha ya vitu vikubwa ambavyo wamevifikia, ni vizuri sana, kwa sababu mafanikio yana maana tofauti kwa watu tofauti. Na mafanikio haya yanaweza kumfanya mwingine (more…)

UKURASA WA 269; Hapa Ndipo Unapojificha.

By | September 26, 2015

Kuna sehemu ambapo umekuwa unajificha. Unajificha sehemu hii sio kwa ajili ya kujilinda bali kwa ajili ya kutoroka kufanikiwa, kwa ajili ya kutoroka kufanya mambo makubwa. Umetafuta sehemu ambayo ukishajificha pale hakuna mtu anayeweza kukulaumu kwamba kwa nini hujafanya mambo makubwa au kwa nini hujatimiza ulichoahidi. Wewe mwenyewe umeshafurahia hapo (more…)

UKURASA WA 268; Hii Ni Vita Kali, Jipange Sana.

By | September 25, 2015

Kuwa bora ni vita kali sana, kwa sababu kila kinachokuzunguka kinakulazimisha kuwa kawaida. Kuwa tofauti ni vita kali sana, kwa sababu kila mtu anategemea uwe kama wengine walivyo. Kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako ni vita kuu kuliko zote utakazokuja kupigana kwenye maisha yako. Vita hii itaanza na wewe binafsi, (more…)

UKURASA WA 267; Wakati Wa Mabadiliko Na Kinachochochea Mabadiliko Ya Kweli.

By | September 24, 2015

Moja; watu hatupendi mabadiliko. Ndio hatupendi kabisa. Hatujui ni kitu gani kitakachotokea baada ya mabadiliko na hivyo hii inatuletea hofu zaidi. Tunapenda kufanya kile ambacho tuna uhakika nacho, “nikifanya kazi mwisho wa mwezi nitapewa mshahara. Nikiingia kwenye biashara sina uhakika kama nitapata wateja”. Hivyo hili linawazuia wengi kubadilika. Mbili; kama (more…)

UKURASA WA 266; Je Ni Hofu Au Ndoto?

By | September 23, 2015

Maamuzi yote ambayo kila mmoja wetu anafanya kwenye maisha, yanaendeshwa na moja kati ya nguvu hizi mbili, HOFU au NDOTO. Maamuzi tunayofanya kwenye kazi, kwenye biashara na hata maeneo yote muhimu kwenye maisha, yanatokana na jinsi tunavyochukulia nguvu hizi mbili. Maamuzi yanayofanywa kutokana na hofu huwa yanaendeshwa na hofu ya (more…)

UKURASA WA 265; Acha Kutoroka Tatizo.

By | September 22, 2015

Binadamu sisi ni wajanja sana. Tunaweza kufanya kila kitu ili kutoroka tatizo na sio kulitatua. Kwa nini tunafanya hivi? Kwa sababu kutatua tatizo kunatutaka tufanye vitu ambavyo hatujisikii vizuri kufanya, au kunatuhitaji tubadilike. Lakini sisi hatupendi kubadilika, hatupendi kufanya vitu ambavyo hatujisikii vizuri kufanya, hivyo hatua rahisi ya kuchukua ni (more…)