Tag Archives: KURASA 365 ZA MWAKA 2015

UKURASA WA 168; Kama Umeshaanza Kutumia Kauli Hizi Sahau Kuhusu Mafanikio.

By | June 17, 2015

Enzi zangu mimi bwana, hela ndogo ndogo kama hizi zilikuwa hazinipigi chenga….. Enzi hizo nilikuwa msanii maarufu sana sema basi tu sasa hivi mambo yangu hayako vizuri… Enzi zangu biashara niliyokuwa nafanya ilikuwa na mafanikio makubwa sana. Sema sasa hivi tu mambo hayajakaa vizuri….. Enzi hizo kazini mimi ndio nilikuwa (more…)

UKURASA WA 167; Maisha Ni Mchezo Na Sheria Za Kuushinda.

By | June 16, 2015

Kuna kauli nyingi sana kuhusu maisha. Mfano wa kauli hizo ni; Maisha ni mapambano… Maisha ni vita… Maisha ni safari…. Na nyingine nyingi. Lakini leo nataka nikuambie kwamba katika kauli zote hizi kuhusu maisha, hakuna ambayo inayaelezea vizuri maisha. Na hapa tutajadili ile ambayo inayaelezea vizuri maisha yetu wanadamu. Kauli (more…)

UKURASA WA 166; Usijishike Na Vitu Hivi Kwenye Maisha Yako, Yatakuwa Magumu Sana.

By | June 15, 2015

Lengo la kila makala ninayoandika, lengo la kila ujumbe ninaoutoa wka njia mbali mbali iwe ni maongezi au hata video(angalia na jiunge na AMKA TV) ni kukupa wewe maarifa na mbinu za kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi. Kwa kuwa hiki ndio unachotaka kwenye maisha yako, au sio? Leo nataka (more…)

UKURASA WA 165; Kuna Kitu Hujui? Hongera Sana Na Jua Jinsi Ya Kukitumia Hapa.

By | June 14, 2015

Moja ya sababu ambazo watu wamekuwa wakizitumia kwamba zinawazuia kufikia mafanikio ni kutokujua vitu fulani au kwa kuelewa zaidi kutokuwa na uzoefu. Kwa kuwa mimi lengo langu ni kukuwezesha wewe kufikia mafanikio makubwa, nahakikisha visababu hivi vinakosa nguvu na wewe unaanza kufanyia kazi kile unachotaka kupata. Sasa leo tuanze na (more…)

UKURASA WA 164; Vitu Ambavyo Ni Rahisi Kufanya…. Na Madhara Yake.

By | June 13, 2015

Vitu ambavyo ni rahisi kufanya ndio vitu ambavyo havina thamani kubwa kwako. N vitu ambavyo hutakiwi kuviamini au kuvitegemea maana havitakupeleka kule ambapo unataka kufika. Unapokutana na changamoto yoyote kuna njia mbili za kufuata, kupambana na changamoto hiyo, kitu ambacho ni kigumu kufanya na kinaweza kukuletea changamoto zaidi. Au unaweza (more…)

UKURASA WA 163; Unapokuwa Mpinzani Wako Mwenyewe… Na Hasara Yake Kwenye Maisha Yako.

By | June 12, 2015

Moja ya changamoto kubwa zinazowazuia watu wengi kupata kile wanachotaka, kufikia mafanikio wanayotarajia ni kuwa wapinzani wao wenyewe. Yaani wewe unakuwa mpinzani wako mwenyewe. Bado hujaelewa inakuwaje? Nitakufafanulia vizuri zaidi ili uweze kuelewa na kuchukua hatua pia. Umekuwa unajifunza mambo mazuri na yatakayobadili maisha yako na unakubali kabisa ya kwamba (more…)

UKURASA WA 162; Hakuna Namna Nyingine…

By | June 11, 2015

Hakuna namna nyingine, ni lazima ufanikiwe. Kuna watu ambao wameanzia chini kuliko ulikoanzia wewe lakini wameweza kufanikiwa, kwa nini na wewe usifanikiwe? Kuna watu ambao wamepata elimu ndogo kuliko uliyopata wewe, lakini wameweza kufanya mambo makubwa kwenye maisha yako, kwa nini wewe ushindwe kufanya? Kuna watu ambao walikataliwa na kutelekezwa. (more…)

UKURASA WA 161; Hiki Ndio Kinachokuzuia Wewe Kupata Kile Unachotaka Kwenye Maisha Yako.

By | June 10, 2015

Hakuna wakati bora wa kuwa hai kama sasa. Huu ni wakati bora sana kwa mimi na wewe kuwa hai hapa duniani. Hii ni kwa sababu kuna uhuru mkubwa sana wa kuweza kufanya kile ambacho kila mmoja wetu anapenda kufanya. Huhitaji tena kupewa ruhusa ndio uweze kufanya kile ambacho unataka kukifanya. (more…)

UKURASA WA 160; Poteza Vitu Vyote Ila Sio Hiki Kimoja Muhimu.

By | June 9, 2015

Unaweza ukapoteza vitu vyote kwenye maisha yako, ndio namaanisha vyote. Iwe ni magari, nyumba, fedha zenyewe na kila kitu cha thamani ambacho umetumia nguvu nyingi kukipaya kwenye maisha yako. Ila utaweza kuvipata vyote kama hutapoteza kitu kimoja muhimu sana. Kitu hiko utajifunza leo hapa baada ya muda mfupi. Kabla hujajifunza (more…)

UKURASA WA 159; Njia Bora Ya Kuweza Kufanya Kitu Unachohofia Kufanya.

By | June 8, 2015

Hofu ni moja ya vitu ambavyo vinawazuia watu wengi kuweza kupiga hatua kwenye maisha yao. Hofu imewafanya watu wengi kushindwa kuzichangamkia fursa zinazowazunguka na hivyo kushindwa kufikia mafanikio kwenye maisha. Moja ya hofu kubwa zinazowazuia wengi kupata maendeleo ni hofu ya kupoteza. Mtu akishakuwa na kitu, hufanya kila lililo ndani (more…)