Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

1639; Falsafa Ya Kushindwa Haraka Na Kushindwa Mapema…

By | June 27, 2019

Watu wengi wanaoanza kitu na kushindwa mwanzoni huona kama ni kitu kibaya kwao, huona kama ni kiashiria kwamba kitu hicho siyo sahihi kwao. Lakini huo siyo ukweli, kushindwa mapema kwenye kile unachofanya siyo kiashiria kwamba huwezi au siyo sahihi kwako, bali ni zawadi kubwa kwako. Makosa yoyote unayoyafanya mwanzoni mwa (more…)

1638; Wakati Sahihi Wa Kusimamia Misingi Na Maadili Yako…

By | June 26, 2019

Huwezi kufanikiwa kama huna misingi na maadili unayoyasimamia kwenye maisha yako, kazi zako na hata biashara ambazo unafanya. Lakini pia unapokuwa na misingi hii, mambo hayatakuwa rahisi. Dunia inapojua kwamba kuna misingi unaiishi na kuisimamia, huwa inakupa majaribu kwenye misingi hiyo. Inakuletea njia na fursa za kunufaika zaidi, kama tu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; JARIBU KINYUME CHAKE…

By | June 26, 2019

“What assistance can we find in the fight against habit? Try the opposite!” —EPICTETUS, DISCOURSES, 1.27.4 Siku mpya, Siku bora, Na siku ya kipekee sana kwetu. Tumeipata nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana kwetu. Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA (more…)

1637; Fedha Ni Zao La Tabia Hizi Kumi…

By | June 25, 2019

Kila mtu anataka kupata fedha zaidi, lakini ni wachache sana ambao wanapata fedha wanazotaka kwenye maisha yao. Hii ni kwa sababu wengi hawajui msingi sahihi wa fedha. Wengi wamekuwa wanakimbizana na fedha na hivyo hawazikamati, kwa sababu fedha zina kasi kuliko wao. Wachache wanazipata fedha wala hawazikimbizi, badala yake wanazivutia. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WENYE HEKIMA HAWANA MATATIZO…

By | June 25, 2019

“This is why we say that nothing happens to the wise person contrary to their expectations.” —SENECA, ON TRANQUILITY OF MIND, 13.3b Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ambayo tumeiona leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo (more…)

1636; Mabadiliko Hayatatokea Kesho…

By | June 24, 2019

Asili ni mwalimu mzuri sana wa mafanikio, Kama utachagua kujifunza kupitia asili, utaweza kupata mafanikio makubwa sana kwenye maisha yako. Asili huwa inafanya vitu vyake kwa misingi miwili, muda na msimamo. Angalia sehemu ambapo tone la maji linadondoka kwenye mwamba kwa kujirudia rudia. Tone moja halina nguvu ya kuvunja mwamba, (more…)

1635; Fedha Na Kusudi La Maisha…

By | June 23, 2019

Ukiwa huna fedha, kitu muhimu zaidi kwako kinakuwa fedha. Hivyo haishangazi pale unapoweka juhudi zako zote kwenye kutafuta fedha, maana huna unachoweza kufanya kwenye maisha bila ya kuwa na fedha. Lakini pia hiki ni kipindi hatari sana kwako, kwa sababu unapopeleka nguvu zako zote kwenye fedha unasahau vitu muhimu kwenye (more…)