Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUITAWALA DUNIA…

By | September 1, 2018

Siku mpya, Siku bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu. Asubuhi ya leo tutafakari HIVI NDIVYO (more…)

BIASHARA LEO; Biashara Siyo Fedha, Ni Watu…

By | August 31, 2018

Watu wengi wanapofikiria kuhusu biashara, cha kwanza wanachofikiria ni fedha. Wanasema hawajaingia kwenye biashara kwa sababu hawana mtaji. Wanasema hawawezi kukuza biashara zao kwa sababu hawana fedha za kutosha. Wanasema biashara zao zinakufa kwa sababu hakuna fedha. Kufikiria biashara kwa upande wa fedha pekee ni kosa ambalo limewazuia wengi kuanzisha (more…)

UKURASA WA 1339; Hujakamilika Na Hutakuja Kukamilika…

By | August 31, 2018

Kama maisha ni nyumba basi tunaweza kusema kitu kimoja, ni nyumba ambayo ujenzi wake haujakamilika, na kila siku kuna kitu kinaendelea kujengwa. Wengi huwa tunachukulia maisha kama kuanza ukiwa hujakamilika, kisha kukamilika na maisha kuwa mazuri, pale unapokuwa umefanikiwa. Lakini wale wanaofuata njia hiyo, huwa wanaishia kuanguka. Pale mtu anapofikiria (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KESHO HAITAKUWA TOFAUTI SANA NA LEO…

By | August 31, 2018

Siku mpya, Siku bora na ya kipekee sana kwetu. Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu. (more…)

BIASHARA LEO; Hakuna Njia Moja Sahihi Ya Kufanya Biashara Yako…

By | August 30, 2018

Moja ya vitu vinavyoua biashara nyingi ni mazoea. Watu wanakuwa wameanza biashara na kugundua njia moja ya kufanya biashara zao ambayo inawapa manufaa na kutumia njia hiyo kwa mazoea bila ya kubadili au hata kuwa bora zaidi. Watu wengine wamekuwa wanashauriwa kwamba njia pekee ya kufanikiwa ni kufanya biashara fulani (more…)

UKURASA WA 1338; Linda Rasilimali Hii Muhimu Sana Uliyonayo…

By | August 30, 2018

Jina lako, yaani ile sifa ambayo wengine wanayo juu yako, ndiyo rasilimali muhimu sana unayomiliki kwenye maisha yako. Hii ndiyo rasilimali pekee ambayo hakuna mtu anayeweza kukuibia, na pia hakuna mtu anayeweza kuiiga kwa namna ilivyo. Ndiyo kitu pekee kinachoweza kukutofautisha wewe na wengine wote hapa duniani. Swali ni je (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUFANYA NA KUTAKA KUONEKANA UNAFANYA…

By | August 30, 2018

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila (more…)

BIASHARA LEO; Vitu Unavyotafuta Kwenye Biashara Ambavyo Hutavipata…

By | August 29, 2018

Nimekuwa nasema hili na bado naona wengi hawalipati vizuri. Watu wengi wanaingia kwenye biashara kwa sababu ambazo siyo sahihi, na hilo linawaumiza sana. Watu wanakuwa na mategemeo fulani wanapoingia kwenye biashara, lakini wakiingia wanakutana na uhalisia tofauti ambao unawaumiza sana. Watu wanaingia kwenye biashara wakiamini watakuwa na uhuru na muda (more…)

UKURASA WA 1337; Mchakato Na Matokeo…

By | August 29, 2018

Hadithi za mafanikio ya wengine huwa haziwasaidii wengi kwa sababu hadithi hizi zinaonesha matokeo na siyo mchakato. Utaambiwa mtu alianzia hapa na sasa amefika pale, alianzia chini kabisa na ameweza kufika juu sana. Mchakato huwa hauelezwi kwenye hadithi hizi, na hata ukimuuliza mtu aliyefanikiwa sana akueleze mchakato wake, kuna vitu (more…)