Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 622; Rahisi Kufanya, Rahisi Kutokufanya.

By | September 13, 2016

Kama ambavyo nimekuwa nasema na kusisitiza mara kwa mara, ili tufanikiwe, tunahitaji kwenda tofauti na baadhi ya mambo yetu ya asili ambayo yanatufanya tuwe na maisha fulani. Akili zetu, saikolojia yetu na hata miili yetu, ina mazoea fulani ambayo yamekuwa kikwazo kwetu kupiga hatua. Kwa mfano, vitu ambavyo ni rahisi (more…)

UKURASA WA 621; Furahia Vikwazo Unavyokutana Navyo…

By | September 12, 2016

Unaweza usielewe lakini unatakiwa kufurahia vikwazo unavyokutana navyo kwenye safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa. Iwe ni kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla. Kwa nini? Kwa sababu vikwazo hivyo ndiyo vinawazuia wengi kufanikiwa. Vikwazo hivyo ndiyo vinawafanya wengi kukata tamaa na kushindwa kuchukua hatua. Vikwazo hivi ndiyo (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Sarafu Ya Maisha Yetu Na Jinsi Tunavyoweza Kuitumia Kufanya Maisha Yetu Kuwa Bora Zaidi.

By | September 11, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Karibu tena kwenye makala yetu ya leo ya FALSAFA MPYA YA MAISHA, ambapo tunakwenda kushirikishana misingi muhimu ya kuendeshe maisha yetu, ili tuweze kupata kile tunachotaka na kuwa na maisha bora na yenye furaha. Kabla hatujaingia kwenye makala ya leo ya falsafa, naomba nikukumbushe mambo (more…)

UKURASA WA 620; Kanuni Rahisi Ya Mafanikio Ambayo Wengi Hawaitumii.

By | September 11, 2016

Niliwahi kuandika kwenye makala za nyuma kwamba, haijalishi unajua nini, bali anakujua nani. Unaweza kuwa unajua sana, unaweza kuwa bora sana kwenye kile unachofanya, lakini kama watu sahihi hawajui kama unajua, hutaweza kufanya makubwa. Lakini wengi wanaposikia hili wanasikitika, kwamba sasa wao wametokea familia masikini, hawana ndugu wenye uwezo wanaowajua (more…)

UKURASA WA 619; Rahisi Kupata, Ngumu Kutunza…

By | September 10, 2016

Ni saikolojia ya binadamu kwamba, kile ambacho kinapatikana kwa urahisi, huwa hatukipi thamani kubwa. Na hivyo kutokukijali, au kutokitunza na hivyo kukipoteza haraka. Kwa mfano, watu wanaopata fedha nyingi kwa haraka, bila ya kuweka kazi kubwa, hujikuta wakipoteza fedha hizo zote ndani ya muda mfupi, au wakizitumia hovyo na kurudi (more…)

UKURASA WA 618; Kilichokufikisha Hapo Ulipo Sasa Ni Hiki…

By | September 9, 2016

Kwa kumwangalia tu mtu, unaweza kujua ni kitu gani kimemfikisha pale alipo sasa, ni maamuzi gani alifanya au hakufanya yamepelekea kuwa pale alipo sasa. Kwa mfano unapomwangalia mtu ambaye yupo kwenye ajira miaka mingi na malalamiko yake ni kipato kutokutosheleza, huku akiwa na madeni mengi, iko wazi kwamba mtu huyu (more…)

UKURASA WA 617; Maneno Ya Kujifariji Yanayowafanya Watu Kuendelea Kuwa Masikini, Yaepuke.

By | September 8, 2016

Hakuna kitu chenye nguvu kwenye maisha yetu kama maneno, maneno yanaumba. Hata mtu ajaribu kiasi gani kubadilika, kama hatabadili maneno yake, basi ataendelea kubaki pale alipo. Kwa sababu maneno yake yanampa nguvu ya kuendelea kuwa pale ambapo yupo. Kumekuwa na maneno ya kujifariji ambayo masikini wamekuwa wakijiambia, na maneno haya (more…)

UKURASA WA 616; Watu Wanakudharau Kwa Sababu Hii Moja…

By | September 7, 2016

Je umewahi kutokuridhishwa na jinsi watu wanavyokuchukulia? Labda unataka watu wakuone wewe ni mtu makini lakini hawakuoni hivyo? Au unataka watu waheshimu muda wako lakini hawauheshimu? Au unataka watu wakuheshimu na kukusikiliza lakini wanakudharau na kutokukusikiliza? Unapokuwa kwenye hali kama hii ni rahisi kuona kwamba watu wanakuchukulia tofauti na unavyotaka (more…)

UKURASA WA 615; Kila Kitu Ambacho Umekuwa Unahubiriwa Kuhusu Mafanikio Ya Wengine Umedanganywa, Ukweli Ni Huu…

By | September 6, 2016

Ni kweli kabisa tunahitaji kupata hamasa kutoka kwa wengine. Tunapojua ya kwamba kuna watu ambao waliweza kufika pale ambapo tunataka kufika, basi tunakuwa na hamasa kubwa sana kwamba hata sisi tunaweza. Hii ni nzuri. Lakini kumekuwa na upendeleo mkubwa sana kwenye kutoa na kutafuta taarifa za watu hawa ambao wameweza (more…)

UKURASA WA 614; Lazima Uumie Na Kimoja Kati Ya Hivi Viwili…

By | September 5, 2016

Hakuna ambaye anapenda kuteseka kwenye maisha, hakuna anayependa kuumia. Lakini uhalisia wa maisha upo tofauti kabisa na matakwa yetu, chochote tunachotaka kwenye maisha yetu, kinahusika na kuumia. Japokuwa watu wengi wamekuwa wakidanganyana kwamba kuna njia rahisi ya kupata kile ambacho wanataka bila ya kuumia, hakuna kitu kama hicho. Sasa kuna (more…)