Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

FALSAFA MPYA YA MAISHA; KWA NINI TANO(5), Njia Ya Uhakika Ya Kutatua Tatizo Lolote Ulilonalo.

By | September 4, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Hongera kwa kuendelea kutengeneza falsafa ya maisha yako, ili uweze kuwa na msingi imara wa kufanya maamuzi muhimu ya maisha yako. bila ya kuwa na falsafa, bila ya kuwa na kitu unachosimamia, utakuwa unapelekwa na kila kitu kama bendera inavyopelekwa na upepo. Hayo siyo maisha (more…)

UKURASA WA 613; Rasilimali Mbili Muhimu Unazohitaji Ili Kuwa Bora…

By | September 4, 2016

Kama unataka kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa, kuna uwekezaji mmoja muhimu sana ambao huwezi kukwepa kuufanya. Uwekezaji huu ni kuwekeza kwako wewe binafsi, kuongeza maarifa, ujuzi na hatimaye uzoefu wako. Kama hakuna maarifa mapya unayopata, utaendelea kufanya unavyofanya sasa na hivyo kuendelea kupata unachopata sasa. Ili kupata matokeo ya (more…)

UKURASA WA 612; Kupendwa na kila mtu….

By | September 3, 2016

Unataka kila mtu akupende? Unataka kila mtu akukubali kwa kile unachofanya? Unataka kila mtu akubaliane na wewe na kukusifia kwenye kile unachofanya? Basi nina jibu rahisi kwako, ondoka kwenye hii dunia. Kwa sababu unachotaka hakipo, na pia hakiwezi kutokea kwenye dunia hii. Huwezi kupendwa na kila mtu, huwezi kukubalika na (more…)

SUPERCOACHING; Timiza Malengo Yako Ya Mwaka 2016 Ndani Ya Siku 120.

By | September 2, 2016

Habari za leo rafiki? Ni mimi rafiki na kocha wako, Makirita Amani, Kila siku nimekuwa nakuandikia makala kuhusu maisha, biashara na mafanikio kupitia AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA. Nina habari kubwa sana kwako, ambazo unahitaji kusikiliza kwa makini ili uweze kuchukua hatua. Mpaka kufikia sasa, zimebaki siku 120 ili (more…)

UKURASA WA 611; Utumwa Wa Kujinunulia Mwenyewe…

By | September 2, 2016

Kwenye haya maisha, kuna utumwa ambao tunakuwa tumeingizwa bila ya sisi wenyewe kujua, tunakuja kustuka tayari tupo kwenye utumwa. Lakini pia upo utumwa ambao tunaununua sisi wenyewe, sisi wenyewe tunachagua kuwa watumwa wa watu wengine. Katika aina hizi mbili za utumwa, huu wa kujinunulia mwenyewe ndiyo mbaya zaidi, kwa sababu (more…)

UKURASA WA 610; Uhusiano Wako Na Fedha…

By | September 1, 2016

Kila kitu kwenye maisha yetu kinaendeshwa na mahusiano. Kuna mahusiano yetu na wengine, mahusiano yetu na sisi wenyewe, pia mahusiano yetu na mafanikio. Pale ambapo mahusiano ni mazuri, ushirikiano unakuwa mkubwa na mafanikio ni dhahiri. Lakini mahusiano yanapokuwa mabovu, ushirikiano unakosekana na inakuwa vigumu kufanikiwa. Leo tuangalie mahusiano yetu na (more…)

BIASHARA LEO; Fukuza Wateja Hawa…

By | August 31, 2016

Nimekuwa nakuandikia na kukushauri kuhusu biashara kwa muda sasa, nafikiri unashangaa ninapokuambia ufukuze wateja. Kabla hujashangaa, soma kwa makini ili mwisho uweze kufanya maamuzi sahihi ya biashara yako. Tatizo la wafanyabiashara wengi. Wafanyabiashara wengi wamekuwa na tatizo moja, ambalo limekuwa linawasumbua sana na kuwazuia kukuza biashara zao. Tatizo hilo ni (more…)

UKURASA WA 609; Kitu Kimoja Walichonacho Mashujaa Na Waoga…

By | August 31, 2016

Kuna watu ambao ni mashujaa, watu ambao tunawaona wana uthubutu mkubwa na kuweza kufanya yale yaliyowashinda wengine. Kila mmoja anapenda kuwa shujaa, japo ni wachache wanaofikia kiwango hiko. Kuna watu ambao ni waoga, watu ambao hawathubutu kufanya mambo makubwa. Watu ambao wapo tayari kufanya kwa ukawaida ili tu wasijiingize kwenye (more…)

UKURASA WA 608; Hasara Ya Kutokufanya Maamuzi Ya Maisha Yako…

By | August 30, 2016

Maisha yetu yanaathiriwa na kila kitu ambacho tunachagua kufanya au kutokufanya. Yaani upo hapo ulipo sasa, kutokana na mambo ambayo ulifanya au ulishindwa kufanya huko nyuma. Na kile unachofanya leo, au unachoshindwa kufanya, ndiyo kinaamua maisha yako ya kesho yaweje. Kitu ambacho kimekuwa kinawashinda wengi kwenye maisha yao, ni kufanya (more…)

BIASHARA LEO; Cross-Selling Na Up-Selling, Mbinu Mbili Za Kuongeza Mauzo Bila Kuongeza Wateja.

By | August 29, 2016

Linapokuja swala la kuongeza mauzo ili kuongeza faida kwenye biashara, wafanyabiashara wengi huwa wanaangalia sehemu moja pekee, kuongeza wateja wengi zaidi. Kuongeza wateja ni mbinu muhimu ya kibiashara kwa sababu biashara yako inaweza kuwafikia watu wengi zaidi. Na kadiri unavyokuwa na wateja wengi, ndivyo unavyotengeneza uhuru wa biashara yako. Lakini (more…)