Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 552; Mchango Wako Ni Jinsi Ulivyo…

By | July 5, 2016

Kama kuna mchango wowote unaoweza kutoa kwenye dunia hii, basi unautoa kwa jinsi ulivyo wewe. Na siyo kwa jinsi unavyofikiri au kusema utatoa mchango gani kwenye dunia hii. Jinsi ulivyo, haiba yako na matendo yako ndiyo vinavyotoa mchango kwenye dunia hii kwa kuanzia na wale wanaokuzunguka. Mchango wako unatokana na (more…)

UKURASA WA 551; Kushindwa Ni Sehemu Ya Kukua…

By | July 4, 2016

Mtoto hawezi kujua kutembea sawasawa bila ya kuanguka. Anayejifunza kuendesha baiskeli hawezi kujua kuendesha kama hatoanguka mara kadhaa. Watu wote ambao tunawaona leo wameweza kufanya mambo makubwa, hawakuanza kuyafanya mambo hayo tangu awali, bali walishindwa sana na kujifunza kupitia kushindwa kwao. Hivyo basi kushindwa kwenye kile unachofanya siyo jambo baya (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Misingi Minne (4) Ya Maisha Ya Wema.

By | July 3, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Karibu kwenye makala yetu ya leo ya FALSAFA MPYA YA MAISHA ambapo tunashirikishana mambo muhimu kuhusu maisha ili tuweze kuwa na maisha bora yenye furaha na mafanikio makubwa. Tatizo moja ambalo limekuwa linafanya maisha ya wengi kuwa ya hovyo ni kukosa misingi. Tumekuwa kwenye jamii (more…)

UKURASA WA 550; Vitu Vitatu Vinavyowaangusha Wengi Wanapokaribia Mafanikio…

By | July 3, 2016

Tumekuwa tunaona watu wengi ambao wanaelekea kwenye mafanikio. Watu hawa wanakuwa wamejitoa kweli, wanaweka juhudi kubwa na dalili zinaonesha kwamba watafika mbali. Lakini ghafla tunaona wanaporomoka na kuondoka kabisa kwenye uelekeo wa mafanikio. Tunaweza kupata sababu nyingi za nje zinazopelekea hali hizo, lakini mara zote sababu huwa zinaanzia ndani ya (more…)

UKURASA WA 549; Adhabu Ya Dunia…

By | July 2, 2016

Dunia imekuwa inatoa adhabu kali sana kwa kila mtu. Wale wanaojifunza kutoka kwenye adhabu ya kwanza wanaepuka adhabu nyingine za baadaye. Lakini wale ambao wanashindwa kujifunza, wanaendelea kuadhibiwa na dunia kila siku. Dunia haina huruma kwenye adhabu hii, wale ambao hawajifunzi wanaendelea kuadhibiwa mara zote, bila ya kujali ni adhabu (more…)

UKURASA WA 548; Tabia Zenye Faida Kubwa Kwa Sasa…

By | July 1, 2016

Asilimia kubwa ya mambo tunayofanya kwenye siku za maisha yetu tunafanya kwa tabia. Yaani tunafanya kwa sababu ndivyo tulivyozoea kufanya. Na mara nyingi huwa ndivyo ambavyo imezoeleka kufanyika kwenye jamii ambazo tunaishi. Kadiri siku zinavyokwenda, mambo yanazidi kuwa magumu na hivyo tabia za watu kubadilika na kuzidi kuwa mbaya au (more…)

UKURASA WA 547; Tatizo La Kusubiri…

By | July 1, 2016

Tatizo la kusubiri ni kwamba ndiyo njia rahisi sana ya kutokuchukua hatua. Huwa inakuwa hivi, unapata wazo zuri sana ambalo unaona kama utalitekeleza, basi maisha yako yatakuwa bora sana. Au unaiona fursa nzuri sana, ambayo kama utachukua hatua utanufaika sana. Lakini kama ilivyo kwa wengi, unasema nitaifanya, subiri kwanza hili (more…)

UKURASA WA 546; Kitu Kimoja Unachoweza Kukitegemea Hatakama Unakosa Vitu Vingi…

By | July 1, 2016

Inawezekana huna akili sana kama ambavyo watu wengine wanaonekana kuwa nazo. Inawezekana huna vipaji ambavyo unaona vimewawezesha wengine kufika pale ambapo wamefika. Inawezekana hukupata elimu bora na ya juu kama ambayo wengine wameweza kupata. Inawezekana huna mtandao mzuri na mkubwa unaoweza kukupa fursa nzuri kama ambavyo wengine wana mitandao hii. (more…)

UKURASA WA 545; Usitumie Nguvu Nyingi…

By | June 30, 2016

Watu wengi wamekuwa wakitumia nguvu nyingi kutaka kuwaonesha wengine au kuonekana wao ni watu wa aina gani. Wapo ambao wanatumia nguvu nyingi kujieleza kwamba ni watu wema na wanaojali sana kuhusu wengine. Pia wapo ambao wanatumia nguvu nyingi kuwatishia wengine ili waonekane kwamba siyo watu wa kuchezewa. Lakini binadamu wana (more…)

UKURASA WA 544; Unavyochagua Kuharibu Maisha Yako Mwenyewe…

By | June 29, 2016

Unachagua kuharibu maisha yako mwenyewe pale unapokubali kuwa mwathirika. Pale unapoona ya kwamba mambo yanatokea kwako kwa sababu huna jinsi ya kupambana nayo, unapoteza nguvu zako zote na kushindwa kuchukua hatua. Pale unaporuhusu utu wako wa ndani kushindwa na mambo yanayotokea nje yako, kila siku unaona maisha ni mabaya kuliko (more…)