Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 543; Sifa Zinakwenda Kwa Nani?

By | June 28, 2016

Mambo makubwa sana yangefanyika kwenye jamii zetu na dunia kwa ujumla kama tusingejali sifa zinakwenda kwa nani. Kama tungekuwa tayari kujitoa kufanya ile sehemu yetu, bila ya kujali nani anapewa sifa, tungefanya makubwa sana. Lakini hali haipo hivyo, wengi wetu tunaangalia kama kuna sifa ambazo tutapata kwa kufanya kitu fulani. (more…)

UKURASA WA 542; Tofauti Ya Masikini Na Matajiri Kwenye Kupata Fedha.

By | June 27, 2016

Kitu kimoja unachotakiwa kujua kwenye kupata fedha ni kwamba fedha zinakuja na gharama. Yaani hupati tu fedha hivi hivi, bali kuna kitu lazima utoe au upoteze ndiyo uweze kupata fedha. Iwe ni kwenye ajira au biashara, unatoa kitu ambacho unacho na unapata malipo kwa kutoa kitu hiko. Katika utoaji huu (more…)

UKURASA WA 541; Njia Bora Ya Kuwa Mwaminifu…

By | June 26, 2016

Kama umekuwa msomaji wa makala hizi za KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, mpaka sasa utakuwa umeshagundua kitu kimoja kikubwa, kwamba msingi wa kila kitu tunachofanya kwenye maisha yetu ni UAMINIFU. Watu watafanya biashara na wewe kutokana na uaminifu wako. Watu watakuajiri na kuendelea kuwa na wewe kwa sababu ya uaminifu. (more…)

UKURASA WA 540; Umuhimu Wa Kupiga Hatua Nyuma…

By | June 25, 2016

Tumekuwa tunafikiri ya kwamba ili kufanikiwa kwenye maisha, mara zote tunahitaji kupiga hatua mbele. Tunahitaji kwenda mbele kwa mbele na nyuma ni mwiko kabisa. Lakini hakuna sehemu muhimu kwenye mafanikio yako kama kupiga hatua nyuma. Tena naweza kusema kama unaona kila kitu kinakwenda mbele peke yake kuwa na wasiwasi, huenda (more…)

UKURASA WA 539; Acha Kujificha…

By | June 24, 2016

Moja ya vitu ambavyo vinawazuia watu kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao ni kujificha. Watu wanakuwa na hamasa kubwa sana ya kufikia mafanikio, lakini wanapopiga hatua kidogo wanapata sehemu ya kujificha, na wao wanajificha. Mtu anakuwa na mipango mizuri ya kibiashara, anaingia kwenye biashara hiyo na mwanzoni anaweza kutengeneza faida (more…)

UKURASA WA 538; Biashara Tayari Unayo…

By | June 23, 2016

Kama bado hujaingia kwenye biashara na kama bado hujajua ni biashara ipi bora kwako kufanya, au kama umekuwa unafikiria kukuza biashara yako na kuanzisha biashara nyingine, huwa unafikiria mambo makubwa sana kabla ya kuingia kwenye biashara hiyo. Tunafikiria mambo makubwa tukiamini kupata wazo bora la biashara inabidi tutumie nguvu kubwa (more…)

UKURASA WA 536; Nje Na Ndani…

By | June 21, 2016

Mambo yanapoharibika, au yanapokwenda kinyume na matarajio yetu, huwa tunakimbilia kuangalia ni nini kimesababisha. Na kwa haraka sana huwa tunatafuta ni kitu gani cha nje ambacho kimechangia mambo kwenda tofauti na matarajio yetu. Biashara inapopata hasara, au inaposhindwa kuleta faida uliyotarajia kupata, mawazo yako yote yanakwenda kwenye kitu cha nje (more…)

UKURASA WA 535; Upendeleo…

By | June 20, 2016

Moja ya tabia zetu binadamu ni kuhakikisha tunakwenda sawa na maamuzi yetu, yaani yale maamuzi ambayo tunayafanya, tunahakikisha tunaweza kuyatetea na yanaendana na sisi. Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa ananieleza ni jinsi gani kumiliki gari binafsi siyo muhimu kwake. Kwamba ni kutumia fedha ambazo hazina malipo kwake. Alinielewa kwa mifano (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Ni Kiasi Gani Cha Fedha Unahitaji Kuwa Nacho Ili Kuwa Na Maisha Bora Na Yenye Furaha?

By | June 19, 2016

Fedha, fedha, fedha, leo imepata nafasi kwenye falsafa yetu mpya kwa sababu ni moja ya vitu vinavyogusa maisha yetu moja kwa moja. Ni moja ya vitu muhimu sana kwenye maisha yetu baada ya hewa tunayovuta. Hii ni kwa sababu kila kitu kinapimwa thamani kwa fedha, chochote tunachotaka, tunaweza kukipata kwa (more…)