Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Nguvu Kubwa Inayokurudisha Nyuma Na Jinsi Ya Kuishinda.

By | November 22, 2015

Habari za leo mwanafalsafa? Karibu tena kwenye makala zetu hizi za falsafa mpya ya maisha ambapo tunapata maarifa sahihi ya kuishi maisha yetu kwa furaha na mafanikio. Kila mmoja wetu anastahili maisha bora, ya furaha kwake na mafanikio makubwa. Lakini wengi hawapati nafasi ya kuishi maisha hayo kutokana na kukosa (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU MIDAS TOUCH(MSHIKO WA MAAJABU)

By | November 21, 2015

Kitabu MIDAS TOUCH ni kitabu ambacho kimeandikwa na wajasiriamali wakubwa wawili wa nchini marekani. Wajasiriamali hawa ni ROBERT KIYOSAKI na DONALD TRUMP. Kitabu hiki kinaelezea misingi mikuu mitano ya ujasiriamali ambayo inawatofautisha wajasiriamali wanaofanikiwa na wale ambao wanashindwa. Misingi hii mitano inafananishwa na vidole vitano vya mkono na hivyo mjasiriamali (more…)

UKURASA WA 325; Anayeongea Sana Ndiye Anayepoteza.

By | November 21, 2015

Katika jambo lolote lile, yule anayeongea sana ndiye anayepoteza. Iwe ni kwenye kufikiana makubaliano au hata kwenye biashara, anayeongea sana anapoteza. Anayeongea sana anapoteza nafasi nzuri ya kuweza kunufaika zaidi. Anakosa nafasi ya kujua kwa undani hasa. Hii ni kwa sababu anayeongea sana anakosa nafasi ya kusikiliza kwa makini, na (more…)

UKURASA WA 324; Sababu Zipo Tayari…..

By | November 20, 2015

Simba na yanga wakiwa na mchezo wa mpira, kuna majibu ya ya aina tatu yanaweza kutokea kwa timu yoyote kati ya hizo. Kushinda, kushindwa au kutoka suluhu. Ikatokea simba wameshinda, watu wanakuwa na sababu z akutosha ni kwa nini wameshinda, na zitakuwa sababu nzuri sana. Na hata ikatokea simba wameshindwa, (more…)

Hivi Ndivyo Waajiriwa Wanavyopoteza Uhuru Wao Wenyewe, Na Jinsi Ya Kuudai Tena.

By | November 19, 2015

Habari za leo rafiki? Naamini unaendelea vyema sana na majukumu yako ya kila siku. Na nina imani kabisa ya kwamba kama unafanyia kazi haya ambayo tunashirikishana hapa basi mambo yako yatakuwa yanabadilika kadiri siku zinavyokwenda. Naomba nikukumbushe pia ya kwamba mabadiliko hayaji mara moja kama mvua, bali yanakuja kidogo kidogo (more…)

UKURASA WA 323; Kabla Hujafanikiwa Wewe Ni Lazima Mtu Huyu Afanikiwe Kwanza.

By | November 19, 2015

Ndio kila mmoja wetu anapenda mafanikio makubwa kwenye maisha. Lakini jambo moja la ukweli ambalo huenda hujawahi kulipa uzito ni kwamba mafanikio yako hujiletei wewe mwenyewe. Kwa dunia tunayoishi ambayo kila kitu unamtegemea mwingine, huwezi kusema kwamba utajipa mafanikio yako wewe mwenyewe. Mafanikio yako yatatoka kwa watu wengine. Yaani wengine (more…)

UKURASA WA 322; Mwishowe Watakubali Tu…

By | November 18, 2015

Hakuna kitu kikubwa na kizuri ambacho ni rahisi kufanya au kupata. Chochote unachofanya au unachotaka, mwanzoni utakufana na upinzani, tena mkubwa sana. Upinzani huu utatoka kwa watu, utatoka kwenye mazingira yanayokuzunguka, na pia unaweza kutoka ndani yako mwenyewe. Utakapoanza kufanya utaona kama vile kila kitu kipo kinyume na wewe. Utaona (more…)

UKURASA WA 321; Hujui Ambacho Hujui, Na Hiyo Ni Vizuri Sana.

By | November 17, 2015

Unasoma hapa kwa sababu unataka mafanikio makubwa kwenye maisha yako. kama hutaki mafanikio ni vyema ukaacha kuwa unasoma makala hizi fupi za kurasa kila siku. Tumekuwa tunajadili mengi sana kuhusiana na safari yetu ya mafanikio. Mbinu za kufikia, changamoto za kuvuka na kadhalika. Leo tutaangalia moja ya changamoto, ambayo wengi (more…)

Mambo matano(5) muhimu ambayo hujawahi kuambiwa kuhusu ujasiriamali.

By | November 16, 2015

Watu wengi wanaingia kwenye ujasiriamali kwa sababu wanaona ndio sehemu nzuri ya kujitengenezea kipato huku ukiwa na uhuru mkubwa. Ni kweli kabisa kwamba ujasiriamali unakupatia uhuru mkubwa. Lakini pia kuna mambo mengi ambayo watu wengi wanaoingia kwenye ujasiriamali huwa hawajui mpaka pale wanapokutana nayo. Na hata baada ya kukutana nayo (more…)