Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 320; Komaa Na Mpango Wako.

By | November 16, 2015

Ingekuwa kuweka tu mipango ndio kufanikiwa, basi kila mtu angekuwa na mafanikio makubwa sana. Kila mtu anaweka mipango mizuri sana, yaani sana. Lakini mipango hii haijitekelezi yenyewe, unahitaji kuweka kazi kubwa ili kuweza kuitekeleza. Kadiri mpango ulivyo mzuri na mkubwa, ndivyo ulivyo mgumu kutekeleza na utakutana na changamoto nyingi. Na (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Upacha wa dunia na jinsi ya kuutumia kuwa na maisha bora.

By | November 15, 2015

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Naamini falsafa hii mpya ya maisha imeanza kushika kasi kwenye maisha yako, nina imani kabisa ya kwamba sasa unafikiri vyema kabla ya kufanya maamuzi ya maisha yako kwa kuangalia falsafa yetu ya maisha inasemaje. Hongera sana kwa hili kwani ndio linafanya tuweze kuishi maisha tunayoyafurahia (more…)

UKURASA WA 319; Huumizwi Bali Unachagua Kuumia.

By | November 15, 2015

Tunapokuwa na mipango na watu wengine, na watu hawa wakawa na eneo lao ambalo wanatakiwa walitekeleze ili na sisi tuweze kutekeleza eneo letu, tunaweka mategemeo yetu makubwa kwa watu hao. Na inapotokea kwamba watu hawa wakashindwa kutekeleza lile eneo lao, na hivyo sisi tukashindwa kutekeleza eneo letu pia, tunaumia na (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU 52 WEEKS OF SALES SUCCESS.

By | November 14, 2015

Kitabu 52 Weeks Of Sales Success ni kitabu ambacho kinaeleza mbinu muhimu z akuweza kufanikiwa kwenye kazi ya kuuza. Kitabu hiki ni muhimu sana kwa kila mmoja wetu kwa sababu wote tunauza. Kila mtu kuna kitu anauza. Kama umeajiriwa unauza muda na utaalamu wako kwa yule aliyekuajiri. Kama unafanya biashara (more…)

UKURASA WA 318; Watu Watakachosema….

By | November 14, 2015

Kama utakuwa na ujasiri wa kutosha, na ukafanya kitu kikubwa, ambacho hakijawahi kufanywa na ambacho kinaweza kuwasaidia wengi. Watu hawataacha kusema, na haya ndiyo yatakayosemwa.. Kuna makumi ya watu watasema ningeweza kufanya vizuri kuliko wewe. Hawa watasema wangeweza kufanya vizuri na kwa ubora kuliko ulivyofanya wewe. Lakini cha kushangaza hawakufanya, (more…)

UKURASA WA 317; Mizigo Ya Wewe Kutua Leo…

By | November 13, 2015

Pamoja na ugumu wa maisha ambao wengi wanakuwa wanausema, lakini sehemu kubwa ya ugumu huu inasababishwa na mtu mwenyewe. Kuna mizigo mingi ambayo umejibebesha na hii inafanya maisha yawe magumu zaidi na zaidi. Leo kwa ufupi sana hapa tutaangalia mizigo uliyojibebesha ili uweze kuitua mara moja; 1. Kinyongo kwa watu (more…)

Kuwa Chanya, Inalipa Sana Kuliko Kuwa Hasi.

By | November 12, 2015

Habari za wakati huu rafiki? Karibu tena kwenye mazungumzo yetu mazuri haya ambapo tunashirikishana mambo mbalimbali kwa ajili ya mafanikio. Kama uliandika email kupata nafasi kwenye program mpya ya ukocha, email bado zinafanyiwa kazi ili kuchagua ni watu gani nitafanya nao kazi. Niwashukuru na kuwapongeza sana wote ambao mmeitaka program (more…)

UKURASA WA 316; Ni Sasa Au Sio Sasa.

By | November 12, 2015

Tumekuwa tunajidanganya sana, na katika kujidanganya huku tumekuwa tukipoteza muda mwingi na kushindwa kukamilisha yale ambayo ni muhimu sana kwetu. Kuna mambo mengi ambayo tunafikiri tunataka kuyafanya, na hivyo kusema tutayafanya baadae. Lakini hii baadae huwa haifiki, na wakati mwingine tunasahau kabisa kama tulishafikiria baadae tutafanya jambo kama hili. Kwa (more…)

WORLD CLASS; Dalili Saba Kwamba Tayari Wewe Una Mtizamo Chanya Utakaokufikisha Kwenye Mafanikio Makubwa.

By | November 11, 2015

Ni ukweli usiopingika kwamba msingi wa kwanza na muhimu sana wa wewe kuweza kufikia mafanikio makubwa ni mtazamo chanya. Unaweza kufanya kazi kwa juhudi kubwa na maarifa, ila kama mtizamo wako haupo sahihi, huwezi kufikia mafanikio makubwa. Mafanikio yoyote makubwa yanaanzia kwenye mtizamo wako kwanza na kisha ndio yanajitokeza kwenye (more…)

UKURASA WA 315; Hii Ndio Zawadi Bora Kabisa Ya Kuwapa Watu Wa Karibu Yako.

By | November 11, 2015

Kuna zawadi bora sana unayoweza kuwapa watu wa karibu yako, watu wanaokuzunguka, ndugu, jamaa na marafiki. Zawadi hiyo ipo ndani yako wewe na kuweza kuwapa kunafanya maisha yenu wote na hata mahusiano yenu kuwa bora zaidi. Na zawadi hii bora sana ya kuwapa watu wako wa karibu ni wewe kuwa (more…)