Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#SheriaYaLeo (306/366); Tumaini kwa ajili yetu wote.

By | September 2, 2022

#SheriaYaLeo (306/366); Tumaini kwa ajili yetu wote. Tumeshaona jinsi ambavyo sisi binadamu ni viumbe wa kihisia. Huwa tunafanya maamuzi yetu kwa kusukumwa na hisia badala ya mantiki. Na hilo ndiyo limekuwa chanzo cha matatizo ambayo tumekuwa tunakutana nayo kwenye maisha. Lakini pamoja na hayo, bado lipo tumaini kwa ajili yetu (more…)

2801; Unaona nini ambacho wengine hawaoni?

By | September 1, 2022

2801; Unaona nini ambacho wengine hawaoni? Watu wawili, wenye uwezo sawa, wanaweza kuanza biashara ya aina moja na kwenye eneo moja, wakilenga wateja wa aina moja. Baada ya muda, mmoja kati yao akawa amefanikiwa kuliko mwingine. Je unadhani nini ambacho kinapelelea mmoja afanikiwe huku mwingine akishindwa? Kumbuka wote wanaanzia ngazi (more…)

#SheriaYaLeo (305/366); Wewe ndiyo kikwazo kwako.

By | September 1, 2022

#SheriaYaLeo (305/366); Wewe ndiyo kikwazo kwako. Maisha ni vita na mapambano, kila wakati unajikuta ukikabiliana na hali mbaya, mahusiano mabovu na mashirikiano hatari. Jinsi unavyokabiliana na hali hizo ndiyo itaamua hatima yako. Kama utajiona umepotea, kama utapoteza mwelekeo, kama huwezi kutofautisha rafiki na adui, unapaswa kujilaumu mwenyewe. Kila kitu kwenye (more…)

2800; Ushahidi mwingine kwamba biashara siyo mtaji pekee.

By | August 31, 2022

2800; Ushahidi mwingine kwamba biashara siyo mtaji pekee. Biashara kuu ya benki ni kutoa mikopo kwa watu, ambao watailipa kwa riba. Hivyo ndivyo benki zinaingiza faida. Sehemu kubwa ya mikopo ambayo benki nyingi zinatoa ni ya biashara au uwekezaji. Mtu anachukua mkopo kwenda kukuza zaidi biashara yake, kuongeza faida na (more…)

#SheriaYaLeo (304/366); Asili ya binadamu haibadiliki.

By | August 31, 2022

#SheriaYaLeo (304/366); Asili ya binadamu haibadiliki. Dunia inaendelea kupiga hatua. Maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaleta ufahamu kwenye mambo mengi ambayo huko nyuma hayakujulikana. Kwa sababu hiyo tunaweza kudhani pia kwamba binadamu nao wanabadilika. Lakini ukweli ni kwamba asili ya binadamu huwa haibadiliki. Bado watu wanafanya maamuzi kwa hisia badala (more…)

#SheriaYaLeo (303/366); Dhibiti majivuno yako.

By | August 30, 2022

#SheriaYaLeo (303/366); Dhibiti majivuno yako. Unataka kufanya makubwa na kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Umejiwekea malengo makubwa ambayo una uhakika wa kuyafikia. Hayo yote ni mazuri kabisa na ndivyo wengi waliofanikiwa walivyofanya. Ila kuna mahali pamoja wengi hukosea na hilo kupelekea kushindwa. Wanapoweka malengo yao makubwa, wanaona ni lazima (more…)

2798; Mazoezi na vita.

By | August 29, 2022

2798; Mazoezi na vita. Kabla ya wanajeshi kwenda vitani huwa wanafanya mazoezi makali. Mazoezi ambayo yanajaribu kuiga uhalisia wa yale watakayokutana nayo kwenye vita. Kabla wachezaji hawajaingia kwenye mashindano, huwa wanafanya mazoezi makali. Mazoezi hayo hugusa kila hali ambayo watakutana nayo kwenye mashindano. Mazoezi yana nguvu ya kumjengea mtu uzoefu (more…)

#SheriaYaLeo (302/366); Sogelea unachokionea wivu.

By | August 29, 2022

#SheriaYaLeo (302/366);Sogelea unachokionea wivu. Watu huwa wana tabia ya kuficha matatizo yao na kuonyesha nyuso zenye furaha. Tunachoona na kusikia kwa watu ni habari njema na ushindi. Hilo huwa linajenga hali ya wivu kwetu, kwa kuona wengine wapo pazuri kuliko pale tulipo sisi. Lakini kama tutawasogelea karibu hao tunaowaonea wivu, (more…)