Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2180; Kama Umeridhika, Inatosha…

By | December 19, 2020

Ni mara ngapi umefanya kazi au jambo ambalo umeridhishwa nalo kweli kweli. Unajivunia kwamba umeweza kufanya kitu ambacho ni tofauti na mazoea, zaidi ya ambavyo umekuwa unafanya. Lakini baadaye mtu mwingine anakuja na kukosoa kile ulichofanya na kukuambia hakuna ulichofanya kabisa, ni kitu cha hovyo. Unakubaliana naye, unajidharau, unaamini kweli (more…)

2178; Nunua Kabla Hujauza…

By | December 17, 2020

Watu hawawezi kununua kitu unachouza kama hawajahamasika, Na huwezi kuwahamasisha watu kununua kitu kama wewe mwenyewe hujahamasika, Na zaidi, huwezi kuhamasika kama hujakikubali kweli kile unachouza. Hivyo kama unataka kuuza vizuri kitu, kinunue wewe mwenyewe kwanza, kikubali kweli kweli, hamasika juu ya kitu hicho. Kadiri unavyokuwa umehamasika kuhusu kitu, ndivyo (more…)

2177; Wakati Wa Kufanya Maamuzi Muhimu…

By | December 16, 2020

Watu wengi wamekuwa wanashindwa kufanya maamuzi yenye manufaa kwao, hasa pale maamuzi hayo yanapokuwa muhimu na magumu. Hiyo inatokana na kutoyapa uzito wa kutosha maamuzi hayo na kutengeneza mazingira yatakayosaidia maamuzi hayo yawe bora. Wengi wanaruhusu hali fulani ziingilie maamuzi yao kitu kinachofanya yasiwe bora. Kuna makosa matatu ambayo watu (more…)

2176; Hakuna Anayekosea…

By | December 15, 2020

Moja ya vitu vikubwa sana nilichojifunza kwenye kitabu cha THE PYSCHOLOGY OF MONEY kilichoandikwa na Morgan Housel kuhusu maamuzi ya kifedha ni kwamba hakuna anayedhani hayuko sahihi. Kila maamuzi ya kifedha ambayo anayafanya mtu, yako sahihi kwa upande wake na kwa hali anayokuwa nayo wakati anafanya maamuzi hayo. Hili ni (more…)

2173; Kwa Sababu Hawawezi Kuishi Bila Hivyo…

By | December 12, 2020

Kuna mashindano mengi huwa yanaendeshwa kuibua vipaji vya wasanii, yaani kupata wasanii wapya ambao kwa namna fulani hawapati nafasi ya kuonekana. Lakini wasanii wote wakubwa unaowajua, hawajaibuliwa na mashindani ya aina hiyo. Kuna mashindano mbalimbali ya kibiashara huwa yanafanyika, kuibua mawazo ya biashara ambayo watu wanayo na kuwapa nafasi ya (more…)

2172; Uimara Wa Msingi…

By | December 11, 2020

Msingi wa kitu chochote kile, unapaswa kuwa imara, ili kuweza kubeba uzito unaoambatana na kitu hicho. Hivyo uimara wa msingi ndiyo unaopima ukubwa kiasi gani unaweza kufikiwa. Ukichukua mfano wa mimea, miti mikubwa na inayodumu kwa muda mrefu, huwa ina mizizi mikubwa na mirefu, hiyo ndiyo inaipa nguvu, kwa kuhakikisha (more…)

2171; Bila Ya Ukinzani…

By | December 10, 2020

Tusingeweza kutembea duniani, maana tungekuwa tunateleza tu. Tusingeweza kuanzisha moto. Mashine zisingeweza kuwashwa wala kuzimwa. Ndege zisingeweza kupaa angani. Lakini ukinzani huo… Unamaliza soli za viatu, Unafanya vifaa vya mashine viishe haraka, Unapelekea hitaji ya nishati kubwa kuendesha mashine mbalimbali. Unaweza kuona jinsi asili inavyofanya kazi hapo, ukinzani unazuia vitu, (more…)