Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

1840; Anza Upya…

By | January 14, 2020

Kinachofanya maisha yetu yawe magumu, kinachotufanya tuwe na msongo ni kwa sababu tunafanya leo yale ambayo tulifanya jana. Kwa kifupi tunafanya kila kitu kwa mazoea na siyo kwa sababu ni muhimu kufanya. Hata mahusiano uliyonayo na wengine, majukumu unayokubali kutoka kwa wengine, kazi na biashara unayofanya na mengine mengi, yote (more…)

1839; Kiraka Juu Ya Kiraka…

By | January 13, 2020

Kama nguo imeharibika na ukaweka kiraka, halafu kiraka hicho kikaharibika tena, wote tunajua kwamba hapo suluhisho siyo kuweka tena kiraka, bali kununua nguo nyingine mpya kabisa. Jambo hili la msingi kabisa huwa tunashindwa kulitumia kwenye maisha yetu ka kila siku. Ni mara ngapi umekuwa unakutana na tatizo au changamoto fulani, (more…)

1837; Tunathamini Zaidi Vinavyopotea…

By | January 11, 2020

Tunajua hili, kwamba sisi binadamu tunasukumwa kuchukua hatua kwa hisia kuu mbili, tamaa na maumivu. Tunafanya kile ambacho kinatupa manufaa na kuacha kile ambacho kinatupa maumivu. Kwenye tamaa, ipo nguvu kubwa sana inayotusukuma kuchukua hatua, ambayo ndani yake pia kuna maumivu kama tusipochukua hatua. Nguvu hiyo ni uhaba. Tunapojua kwamba (more…)

1836; Tengeneza, Tunza, Kuza.

By | January 10, 2020

Hizi ni hatua tatu ambazo ni muhimu sana kuzifanyia kazi kwenye kila eneo la maisha yetu. Tukianza na maisha yetu wenyewe, tunapaswa kuyatengeneza, kuyatunza na kisha kuyakuza zaidi. Kwenye fedha, tunapaswa kutengeneza kipato, kukitunza na kisha kukikuza zaidi. Kwenye mahusiano, tunapaswa kuyatengeneza, kuyatunza na kisha kuyakuza zaidi. Watu wengi wanashindwa (more…)

1835; Pesa Zipo Kwenye Hisia…

By | January 9, 2020

Dunia inaendesha na kitu kimoja, hisia. Na hii ni kwa sababu sisi binadamu huwa tunafanya maamuzi yetu yote kwa hisia kwanza na kisha kuyahalalisha kwa fikra. Watu huwa wanatumia fedha zao kwenye vitu ambavyo vinawafanya wajisikie vizuri. Na kule ambapo fedha inapoenda, ndipo nguvu na mamlaka yalipo. Sasa kwa kuwa (more…)

1834; Kama Watu Hawakuelewi Ni Tatizo Lako…

By | January 8, 2020

Watu wanaweza wasikubaliane na wewe, na wengi watakupinga au kukukosoa, hilo siyo tatizo lako, ni tatizo la mtazamo wao. Lakini kama watu hawakuelewi, hilo ni tatizo lako wewe, na siyo tatizo lako, hata kama watu hao uelewa wao ni mdogo. Kwa chochote unachofanya au kusimamia, hakikisha unaweza kumweleza mtu yeyote (more…)

1833; Kazi Yako Ni Kufanya Kazi Yako…

By | January 7, 2020

Kama kazi yako haihusishi mitandao ya kijamii, kutumia mitandao wakati wa kazi ni kutoroka kazi yako. Kama kazi yako haihusishi matumizi ya simu, kutumia simu wakati wa kazi ni kutoroka kazi yako. Kama kazi yako haihusishi majungu na kufuatilia maisha ya wengine, kufanya mambo hayo wakati wa kazi ni kutoroka (more…)

1832; Upendo Na Heshima…

By | January 6, 2020

Tunapenda kupendwa, na hilo ndiyo linalotusukuma kwenye mambo mbalimbali tunayofanya. Tunavaa nguo nzuri ili tupendwe, tunafanya yale wengine wanafanya hata kama hatutaki kuyafanya ili tu tupendwe. Kuna wakati tunaenda mbali na hata kufanya mambo ambayo siyo sahihi kwetu, ili tu tupendwe. Sasa leo nina ujumbe wa tofauti kwako rafiki yangu, (more…)

1831; Nguvu Ya Mvutano…

By | January 5, 2020

Kinachotuzuia sisi binadamu tusiweze kuruka angani kama jamii ya ndege ni kwa sababu hatuna njia ya kuishinda nguvu ya mvutano ya dunia. Mabawa ya ndege yanawawezesha kutengeneza nguvu inayokinzana na nguvu ya mvutano wa dunia na hivyo kuweza kuruka angani. Lakini kwa kuwa sisi binadamu tumepewa kitu ambacho wanyama wengine (more…)