Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2440; Shabiki wako namba moja…

By | September 5, 2021

2440; Shabiki wako namba moja… Wewe ndiye unayepaswa kuwa shabiki wa kwanza kwako mwenyewe. Unapaswa kujikubali sana na kujishabikia kwenye yale makubwa ambayo unayafanya. Usiwe shabiki wa wengine au wa michezo mbalimbali kabla hujawa shabiki wako mwenyewe. Usifurahie ushindi wa wengine unaowashabikia na kuona kama ni ushindi wako wakati wewe (more…)

2439; Alama kwamba umefanya wewe…

By | September 4, 2021

2439; Alama kwamba umefanya wewe… Kitu chochote kile unachofanya, unapaswa kuacha alama kwamba ni wewe umefanya. Unapaswa kukifanya kwa upekee wa hali ya juu sana, kwa namna ambayo hakuna mwingine anayeweza kukifanya hivyo. Na hilo linawezekana kabisa kama utajitambua wewe mwenyewe na kuchagua kuwa wewe badala ya kuhangaika kuwaiga wengine. (more…)

2438; Pata Pesa Kwanza…

By | September 3, 2021

2438; Pata Pesa Kwanza… Huwa kuna picha huwa inazunguka mtandaoni, ikimnukuu Warren Buffett akisema; pesa siyo kila kitu, ila hakikisha unazo za kutosha kabla hujaongea huo ujinga. Nina hakika Buffett hajawahi kusema maneno ya aina hiyo, ila ujumbe huo umekuwa maarufu kwa sababu umebeba ujumbe mkubwa na muhimu sana kuhusu (more…)

2437; Unahangaika na watu wasio sahihi…

By | September 2, 2021

2437; Unahangaika na watu wasio sahihi… Watu ndiyo kazi yetu kubwa kwenye maisha. Tunahitaji kushirikiana na watu mbalimbali kwenye safari yetu ya mafanikio. Watu hawafanani, wana sifa na tabia mbalimbali. Wapo ambao tunaweza kwenda nao vizuri na wakawa na manufaa makubwa kwetu. Lakini pia wapo ambao tunapokuwa nao tunasumbuana sana (more…)

2436; Kuiga mpaka uwe…

By | September 1, 2021

2436; Kuiga mpaka uwe… Huwa kuna kauli maarufu ya Kiingereza inayosema; fake it till you make it. Ikiwa inamaanisha chochote kile unachotaka, unapaswa kukiigiza mpaka kiwe kweli kwenye maisha yako. Na dhana kuu ni kwamba akili yetu ya ndani huwa haiwezi kutofautisha ukweli na maigizo. Yenyewe inachukulia kile mtu anachofanya (more…)

2435; Kukusanya na kutawanya…

By | August 31, 2021

2435; Kukusanya na kutawanya… Kitu kimoja ambacho nazidi kujifunza kwenye eneo la mafanikio ni wanaofanikiwa na wanaoshindwa wote wanaanza na rasilimali zinazolingana. Mwanzoni watu hao hawatofautiani sana kwenye eneo la rasilimali. Kama ni muda wanakuwa nao sawa. Akili pia hawatofautiani sana. Na hata kwenye fedha, wengi huanzia chini wakiwa hawana (more…)

2434; Hadithi unayojilisha na kupima…

By | August 30, 2021

2434; Hadithi unayojilisha na kupima… Kitu pekee kinachotutofautisha sisi binadamu na wanyama wengine kama mbuzi ni hadithi ambazo tunajipa. Na hadithi hizo zinatokana na ubongo wetu wa mbele, ambao ni mkubwa na umeendelezwa ukilinganisha na wa wanyama wengine. Wanyama wengine wanapokea na kuishi katika hali walizozaliwa nazo. Lakini sisi binadamu (more…)

2433; Kichekesho cha jamii…

By | August 29, 2021

2433; Kichekesho cha jamii… Mchekeshaji mmoja amewahi kusema watu wanatumia fedha ambazo hawana, kununua vitu ambavyo hawavitaki ili kujionyesha kwa watu ambao hawajali. Na mwandishi Morgan Housel kwenye kitabu chake cha psychology of money ameandika kuhusu dhana ya mtu aliye kwenye gari la kifahari. Anasema wengi hununua magari ya kifahari (more…)

2432; Kila kitu ni rahisi isipokuwa kufanya…

By | August 28, 2021

2432; Kila kitu ni rahisi isipokuwa kufanya… Kuahidi ni rahisi, Kuweka malengo ni rahisi, Kupanga ni rahisi, Kukosoa ni rahisi, Kuomba ushauri ni rahisi, Kushauri ni rahisi, Kulalamika ni rahisi. Kila kitu ni rahisi, isipokuwa kimoja tu, ambacho ni kufanya. Kuweka juhudi katika kufanya kitu, ili kuleta matokeo ya tofauti, (more…)

2431; Kuchinja kuku anayetaga…

By | August 27, 2021

2431; Kuchinja kuku anayetaga… Ili upate mayai zaidi ni jambo la ajabu lakini ambalo limekuwa linafanywa na wengi. Wengi huanza na kitu chini kabisa, wanaweka juhudi kubwa na hizo kupelekea kitu hicho kuwapa matokeo mazuri. Wakishapata matokeo mazuri wanajisahau na kujikuta wanaharibu kabisa kile kilichokuwa kinawapa matokeo hayo. Kinachotokea ni (more…)