Category Archives: SHERIA ZA SIKU

#SheriaYaLeo (326/366); Ungana na kilicho karibu yako.

By | September 22, 2022

#SheriaYaLeo (326/366); Ungana na kilicho karibu yako. Maisha ni mafupi na nguvu zetu zina ukomo. Kwa kuongozwa na tamaa zetu, tunaweza kupoteza muda na nguvu kwenye kutafuta mabadiliko. Kwa ujumla, hupaswi kusubiri na kutumaini mambo yatakwenda vizuri, bali unapaswa kutumia vizuri kile ulichonacho. Asili inakuunga mkono. Kwa kuzamisha akili yako (more…)

#SheriaYaLeo (325/366); Fokasi na vipaumbele.

By | September 21, 2022

#SheriaYaLeo (325/366); Fokasi na vipaumbele. Baadhi ya mambo unayofanya ni upotevu wa muda wako. Baadhi ya watu unaojihusisha nao ni wa hadhi ya chini, ambao watakuvuta urudi chini. Unapaswa kuepuka mambo na watu hao kama ukoma ili kutumia muda wako vizuri. Macho yako yanapaswa kuwa kwenye malengo yako makuu na (more…)

#SheriaYaLeo (324/366); Hatima ya maisha yako.

By | September 20, 2022

#SheriaYaLeo (324/366); Hatima ya maisha yako. Watu wote waliowahi kufanya makubwa hapa duniani walikuwa ni watu wa kuamini maisha yao yana hatima kubwa. Hawakukubali kuyumbishwa kwa namna yoyote ile kwenye hilo. Waliamini wanakwenda kufanya makubwa mpaka jamii iliyowazunguka nayo ikawaamini kwenye hayo. Kwa imani hiyo isiyoyumbishwa, waliweza kufanya makubwa sana. (more…)

#SheriaYaLeo (323/366); Angalia nje yako pia.

By | September 19, 2022

#SheriaYaLeo (323/366); Angalia nje yako pia. Kwa asili sisi binadamu huwa tunajiangalia sisi wenyewe zaidi. Huwa tunajali zaidi kuhusu changamoto zetu na matakwa yetu pia. Wewe unapaswa kwenda kinyume na hili kadiri iwezekanavyo. Na utaweza kulifanya hilo kwa njia tatu; Kwanza unakuwa msikilizaji makini. Unaweka umakini wako wote kwa wengine, (more…)

#SheriaYaLeo (322/366); Linganisha ubunifu na uhalisia.

By | September 18, 2022

#SheriaYaLeo (322/366); Linganisha ubunifu na uhalisia. Chochote unachofanya, huwa kinaanza na mawazo yako ya kibunifu. Kadiri unavyokwenda unakazana kuwa na ubunifu zaidi ili kufanya kitu cha tofauti. Unapoanza kufanya kulingana na mawazo yako ya kibunifu, kuna matokeo unayoyapata na mrejesho kutoka kwa wengine. Hapa unahitaji sana kupata maoni ya wengine (more…)

#SheriaYaLeo (321/366); Tumia kivuli chako.

By | September 17, 2022

#SheriaYaLeo (321/366); Tumia kivuli chako. Tumeshaona jinsi ambavyo kila mtu ana kivuli ndani yako. Sehemu ya nafsi ya mtu ambayo anapenda kuificha kwa sababu haikubaliki sana kwa wengine. Nafsi hiyo huwa inakuwa na nguvu kubwa kama itaweza kutumiwa vizuri. Hivyo wajibu wako ni kuangalia namna gani unavyoweza kutumia kivuli chako (more…)

#SheriaYaLeo (320/366); Kuwa na roho ya ukarimu.

By | September 16, 2022

#SheriaYaLeo (320/366); Kuwa na roho ya ukarimu. Wote tumebeba majeraha na maumivu mbalimbali tangu utotoni. Kwenye maisha yetu ya kijamii, kadiri tunavyokua, tunakutana na hali za kuangushwa na kukatishwa tamaa. Hali hizo hutufanya tujione hatuna thamani na wala hatustahili vitu vizuri kwenye maisha. Wote huwa tuna nyakati za wasiwasi juu (more…)

#SheriaYaLeo (319/366); Igiza chenye ushawishi.

By | September 15, 2022

#SheriaYaLeo (319/366); Igiza chenye ushawishi. Katika nyakati zozote tunazoishi, huwa kuna tabia fulani ambazo huwa zinaonekana chanya na kukubalika na wengine. Hizo ndizo tabia unazopaswa kujua jinsi ya kuzionyesha ili ukubalike na wengine na uwe na ushawishi. Kwa mfano, kuonekana mtakatifu kwa nje ni kitu ambacho hakijawahi kupitwa na wakati. (more…)

#SheriaYaLeo (318/366); Usivurugwe na wapumbavu.

By | September 14, 2022

#SheriaYaLeo (318/366); Usivurugwe na wapumbavu. Huwezi kuwa kila mahali na huwezi kupambana na kila mtu. Muda wako na nguvu zako ni rasilimali zenye uhaba, unapaswa kujifunza jinsi ya kutunza rasilimali hizo. Kuchoka na kuvurugwa ni matokeo ya upotevu wa rasilimali hizo na inavuruga sana uwepo wa kiakili. Dunia imejaa wapumbavu (more…)

#SheriaYaLeo (317/366); Vunja agano la mazoea.

By | September 13, 2022

#SheriaYaLeo (317/366); Vunja agano la mazoea. Kuna mazoea ambayo tayari yameshajengeka na yanazingatiwa sana kwenye jamii. Jinsi watu wanavyopaswa kuwa, vitu wanavyopaswa kusema na kufanya tayari vimeainishwa. Hali hizo zinakuwa zimejengwa kwenye tofauti za kijinsia, kikabila, kielimu na nyinginezo. Kukaa kwenye maagano haya ya mazoea ni kujizuia usifanye makubwa, kwani (more…)