2495; Unajua cha kufanya.

By | October 30, 2021

2495; Unajua cha kufanya. Wakati naanza huduma ya ushauri na ukocha, nilidhani watu hawafanikiwi kwa sababu hawajui cha kufanya. Hivyo nilikuwa na haraka sana ya kuwaambia nini wanapaswa kufanya, hasa wanapokuwa kwenye changamoto mbalimbali. Lakini kadiri ambavyo nimeendelea kufanya huduma hii, nimegundua kitu kimoja kikubwa sana. Watu hawafanikiwi siyo kwa (more…)

2494; Kuna neno hajasikia.

By | October 29, 2021

2494; Kuna neno hajasikia. Nikiwa kwenye sherehe fulani, mshereheshaji alikuwa anatumia njia mbalimbali kuwashawishi watu kutoka kwenye viti na kwenda kucheza muziki. Kwanza alianza kwa kutumia kigezo cha kupendeza, akisema wote mmependeza sana, na kwa kupendeza huko mje kucheza. Akaona siyo wengi wanaotoka kucheza, akasema wale ambao hawatoki hawajapendeza. Bado (more…)

2493; Unapoteza Ulichonacho.

By | October 28, 2021

2493; Unapoteza Ulichonacho. Changamoto nyingi kubwa kwenye maisha majibu yake huwa ni rahisi kabisa. Lakini tumekuwa hatukubali wala kufanyia kazi majibu hayo kwa sababu ya urahisi wake, tunaona hayawezi kuwa sahihi. Ni majibu hayo rahisi tunayoyapuuza kwenye maisha ndiyo yamekuwa kikwazo kikubwa kwetu kupiga hatua kubwa. Leo tuangalie mfano wa (more…)

2492; Kidogo kidogo halafu ghafla.

By | October 27, 2021

2492; Kidogo kidogo halafu ghafla. Mambo yote kwenye maisha huwa yanaanza kidogo kidogo kisha baadaye yanatokea ghafla. Lakini mara nyingi watu huwa hawaoni yanapotokea kidogo kidogo na kuchukua hatua sahihi, wanakuja kushtuka wakati yametokea ghafla na hawawezi tena kuchukua hatua kwa haraka. Hakuna mtu anaamka siku moja na kujikuta kwenye (more…)

2491; Hawabadiliki, wanachoka kuigiza.

By | October 26, 2021

2491; Hawabadiliki, wanachoka kuigiza. Watu huwa hawabadiliki, bali wanachoka kuigiza. Angalau siyo kwa haraka kiasi hicho, yaani hata kama watu watabadilika, haiwi haraka na rahisi. Hivyo unapojiambia mtu amebadilika, kuwa makini, mara nyingi anakuwa amechoka kuigiza na kuamua kuishi uhalisia wake. Kwamba mtu alikuwa mwaminifu na ghafla amekuwa siyo mwaminifu (more…)

2490; Kama inabidi utumie nguvu sana, kuna kitu

By | October 25, 2021

2490; Kama inabidi utumie nguvu sana, kuna kitu hakipo sawa. Kama inabidi utumie nguvu nyingi kuwaonyesha watu umefanikiwa, jua hujafanikiwa. Kama inabidi utumie nguvu kubwa kuwaonyesha watu kwamba wewe ni mwaminifu, basi siyo mwaminifu. Kama inabidi uwalazimishe watu kuuona ukweli, huo utakuwa siyo ukweli. Kama kila wakati unajiuliza iwapo una (more…)

2486; Machaguo mengi.

By | October 21, 2021

2486; Machaguo mengi. Tuna bahati kubwa ya kuishi kwenye zama ambazo tuna machaguo mengi kwenye kitu chochote tunachofanya. Hulazimiki kuchukua chochote kilichopo, bali una uhuru wa kuchagua kile unachotaka. Tulidhani katika zama hizi za machaguo mengi wengi wangekuwa na furaha na mafanikio kutokana na uhuru mkubwa uliopo wa kuchagua. Lakini (more…)