#TAFAKARI YA LEO; DUNIA ITAKURUSHIA VITU…

By | October 20, 2018

Seneca said, “Things will get thrown at you and things will hit you. Life’s no soft affair.” Siku mpya, Siku bora na ya kipekee sana imeanza. Ni siku ambayo umekuwa unaisubiria kwa hamu, siku ambayo jana ulisema kesho nita…. Kesho ya jana ndiyo tayari imeshafika hivyo nenda kachukue hatua leo. (more…)

1388; Namba Hatari Sana Kwenye Maisha Yako…

By | October 19, 2018

Kuna namba moja hatari sana kwenye maisha yako, namba hii ni hatari kwa chochote kile unachofanya, ni namba unayopaswa kuijua na kuiepuka kwa namna yoyote ile. Namba hiyo ni namba moja. Namba moja, kwenye jambo lolote kwenye maisha ni namba hatari. Unapoweka mategemeo yako yote kwenye kitu kimoja, unajiweka kwenye (more…)

1387; Siku Unayoanza Kuanguka Ni Unapofikiri Umeshakuwa Bora…

By | October 18, 2018

Tunapokuwa tunaanza kufanya kitu, huwa tunakuwa ni watu wa kujifunza. Tunakuwa tunajua hatujui na hivyo kuweka juhudi katika kujifunza ili kuweza kufanya vizuri zaidi. Ni kiu hii ya kujifunza ndiyo inayotuwezesha kuwa bora zaidi, kuweza kufanya vizuri zaidi na kupata matokeo bora zaidi. Lakini kadiri tunavyokuwa bora, kadiri tunavyopata matokeo (more…)

1386; Maisha yako yanapotelea wapi?

By | October 17, 2018

Ukiwa mbali na msitu, unachokiona ni msitu, unaona miti ambayo imefunga kila eneo na hutaweza kuiona ardhi kwa wazi wazi. Lakini unapoigia ndani ya msitu, huwezi tena kuuona msitu, badala yake unaona mti mmoja mmoja, unaona ardhi na vitu vingine vidogo vidogo ambavyo kwa mbali havionekani. Hivi ndivyo maisha yetu (more…)

1385; Ili Kujijua, Unahitaji Kupitia Mateso Makali…

By | October 16, 2018

Huwezi kujua unaweza kwenda mbali kiasi gani, mpaka uende mbali zaidi ya ulivyozoea. Kadiri unavyokwenda mbali zaidi ya ulivyozoea, ndivyo unavyozidi kugundua kwamba unaweza kwenda mbali zaidi. Kama umeacha kwenda mbali zaidi, utaamini kwamba pale ulipofika ndiyo kikomo, lakini uhitaji unapokuja, utagundua ya kwamba unaweza kwenda mbali zaidi. Njia pekee (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KAMA HAIENDANI NA NDOTO ZAKO, NI USUMBUFU…

By | October 16, 2018

“I’m here to build something for the long term. Anything else is a distraction,” Facebook cofounder Mark Zuckerberg said when he declined Yahoo’s $1 billion offer to buy his social networking service in 2006. Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya (more…)

1384; Mambo Matatu Yatakayokuwezesha Kufanya Maamuzi Bora Sana Kwenye Maisha Yako.

By | October 15, 2018

Moja ya changamoto kubwa kwenye zama tunazoishi sasa ni wingi wa maarifa na taarifa ambazo zinawafanya wengi washindwe kufanya maamuzi sahihi kwenye maisha yao. Kuna maarifa na taarifa nyingi ambazo zinakinzana na mtu anapofuatilia zote, anashindwa kujua afanye nini. Anaanza kubishana na yeye mwenyewe, anaanza  kuwa na wasiwasi juu yake, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WAKATI SAHIHI WA KUCHIMBA KISIMA…

By | October 15, 2018

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii mpya ya leo, Ni siku nyingine nzuri sana kwetu, ambapo tumepata nafasi ya kipekee ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa (more…)