UKURASA WA 1369; Kadiri Unavyosubiri, Ndivyo Inavyokuwa Vigumu Kuanza…

By | September 30, 2018

Watu wengi wamekuwa wanapata mawazo mazuri sana, mawazo ambayo kama watayatekeleza basi maisha yao yatakuwa bora sana. Changamoto ni kwamba wengi wamekuwa hawatekelezi mawazo mazuri wanayokuwa nayo, wamekuwa hawachukui hatua kuyageuza mawazo hayo kuwa uhalisia. Na kinachowazuia wengi kuchukua hatua kwenye mawazo yao, ni kusubiri. Pale unapopata wazo, unakuwa na (more…)

BIASHARA LEO; Kusema Hapana Kwa Fursa Nzuri…

By | September 29, 2018

Kitu kimoja ambacho kinapelekea baadhi ya biashara zinazoanza vizuri na kukua kisha zinaanguka vibaya, ni wafanyabiashara kushindwa kusema hapana kwa fursa nzuri zinazojitokeza mbele yao. Iko hivi, unaanza biashara ukiwa na maono fulani kwenye akili yako. Unataka biashara yako iwe ya aina fulani, iwasaidie watu wa aina fulani na ikupe (more…)

UKURASA WA 1368; Kubishana Ni Kupoteza Muda Wako…

By | September 29, 2018

Hakuna kitu cha hovyo, kinachopoteza muda na nguvu za watu kama mabishano. Kwa sababu baada ya mabishano hakuna matokeo yoyote ya tofauti ambayo mtu unayapata. Chukulia mfano wa mabishano ya kawaida kwenye mambo ambayo yana pande mbili, labda vyama vya siasa, dini, michezo na kadhalika, hata watu wabishaneje, kila mtu (more…)

BIASHARA LEO; Wingi Wa Wateja Na Ubora Wa Wateja…

By | September 28, 2018

Wafanyabiashara wengi huwa wanafurahi sana pale wanapokuwa na wateja wengi. Kwa sababu wanaamini wingi wa wateja ndiyo mafanikio ya biashara. Na huwa hawaelewi pale wanapokuwa na wateja wengi lakini biashara inakufa, hapo ndipo wanaamini kwamba kuna chuma ulete. Haiwezekani wauze kwa wateja wengi halafu biashara isipate faida. Ipo kampuni moja (more…)

UKURASA WA 1367; Umekalia Mgodi Wa Dhahabu Hapo Ulipo…

By | September 28, 2018

Upo usemi kwamba nyasi za jirani huwa zinaonekana ni za kijani kuliko nyasi zetu wenyewe. Yaani kama kwenye uwanja wako umepanda nyasi, na jirani yako naye amepanda nyasi, ukiangalia nyasi za jirani yako utaona zinaendelea vizuri kuliko zako. Unaweza kuona labda jirani huyo ana bahati na wewe huna bahati. Lakini (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UIMARA WAKO AU UDHAIFU WA WENGINE?

By | September 28, 2018

AMKA Mwanamafanikio, AMKA Kwenye siku hii nyingine nzuri sana ya leo. AMKA Na uende kwenye mapambano mapya ya siku hii ya leo. Leo ni nafasi nyingine nzuri na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja (more…)

BIASHARA LEO; Usiajiri Watu Wanaotaka Kazi, Ajiri Watu Wanaotaka Hiki…

By | September 27, 2018

Changamoto nyingi zinazotokana na kuajiri kwenye biashara, zinatokana na watu wanaotafuta kazi ya kufanya. Watu ambao wanakuambia wanaweza kufanya kazi yoyote na wanaoangalia ni nini wanalipwa pekee. Hawa ni watu ambao unaweza kuwapata kirahisi sana, unaweza kuwalipa rahisi pia, lakini pia utawapoteza kirahisi na kazi yoyote wanayoiweka inakuwa ya urahisi, (more…)

UKURASA WA 1366; Mwajiri Mbovu Sana Kuwahi Kutokea Duniani Ni Huyu…

By | September 27, 2018

Hakuna mwajiri mbovu kabisa amewahi kutokea hapa duniani kama mwajiri aliyekuajiri wewe. Huyu ni yule mwajiri wa kwanza kabisa, ambaye ndiye mtu wa kwanza kabisa mwenye jukumu kuu la maisha yako. Na mwajiri huyu wa kwanza kwenye maisha yako ni wewe mwenyewe. Kama ambavyo nimewahi kukuambia, haijalishi nani amekuajiri au (more…)