BIASHARA LEO; Bishara Unayofanya Leo, Siyo Biashara Utakayofanya Kesho…

By | September 26, 2018

Unapaswa kuifanya biashara yako vizuri sana leo, Na wakati huo huo kujiandaa na mabadiliko yanayoendelea kutokea kwenye biashara yako. Kwa sababu biashara unayofanya leo, siyo biashara utakayofanya kesho, mwaka ujao, miaka 5 ijayo na hata miaka 10 ijayo. Mambo yanabadilika, watu wanabadilika na mahitaji yao yanabadilika pia. Watu wanataka vitu (more…)

UKURASA WA 1365; Kuzuia Dharura Isiwe Kikwazo Kwako…

By | September 26, 2018

Haijalishi unafanya nini, kuna vitu vitatokea ambavyo hukutegemea kama vingetokea. Sisi huwa tunapanga, lakini asili inaendesha mambo yake kwa namna inavyoendesha yenyewe, hivyo haitaenda kulingana na mipango yetu, bali kulingana na mipango yake. Sasa kwa kuwa huwezi kuidhibiti asili, kwa kuwa huwezi kubadili mipango inayojiendesha kwa asili, hutaweza kuzuia vitu (more…)

BIASHARA LEO; Uza Kitu Ambacho Unapata Shida Ya Kukipata…

By | September 25, 2018

Kama unajiambia unataka kuingia kwenye biashara lakini hujui biashara gani ufanye, nina ushauri mmoja mzuri sana kwako. Uza kitu ambacho unapata shida ya kukipata. Najua kwenye maisha yako kuna vitu unatafuta, ambavyo umekuwa hupati au hata ukipata siyo kwa namna ambavyo ulitaka kupata. Habari njema ni kwamba, siyo wewe mwenyewe (more…)

UKURASA WA 1364; Hofu Haitaondoa Tatizo La Kesho…

By | September 25, 2018

Karibu kila falsafa na imani ya kidini inaeleza umuhimu wa kuishi wakati uliopo, umuhimu wa mtu kuishi sasa, kuwa pale alipo, kwa wakati aliopo. Lakini sisi binadamu tuna uwezo mkubwa sana wa kuyaharibu maisha yetu bila ya kufanya chochote, bali kujitengenezea hofu ya vitu visivyokuwepo na ambavyo hatuwezi kuviathiri kwa (more…)

BIASHARA LEO; Mteja Hajali Kuhusu Ushindani Wako Na Wafanyabiashara Wengine…

By | September 24, 2018

Kama kila biashara ingeweka rasilimali zake kwenye kuwahudumia vizuri wateja wake, biashara zingefanikiwa sana. Lakini biashara nyingi zimekuwa zinatafuta njia za mkato za kupata wateja, na moja ya njia hizo ni kuwaangusha washindani wao wa kibiashara. Kama una washindani wa kibiashara, jambo jema kabisa unaloweza kufanya kwa ajili yako ni (more…)

UKURASA WA 1363; Huhitaji Muda Zaidi, Unahitaji Kuamua Sasa…

By | September 24, 2018

Kinachowazuia watu wengi kupata kile wanachotaka, kupata mafanikio makubwa, ni muda uliopo kati ya wazo, kuamua na kuchukua hatua. Watu wengi wanapata wazo, lakini inawachukua muda sana mpaka kufikia maamuzi na hata wakishafikia maamuzi, inawachukua muda sana mpaka kuanza kuchukua hatua. Kadiri muda kati ya wazo na maamuzi unavyokuwa mrefu, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAISHA KAMA MCHEZO…

By | September 24, 2018

AMKA mwanamafanikio, AMKA kwenye siku hii mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu. Ni siku nyingine ambayo tumepata nafasi ya kipekee kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa (more…)