BIASHARA LEO; Hakuna Aliyekulazimisha Uje Kununua Hapa, Umekuja Mwenyewe…

By | September 23, 2018

Fikiria umeenda kwenye biashara, una shida ya kitu fulani, umeoneshwa kile pale, bei yake kiasi fulani. Unataka kujua zaidi kama kitakusaidia, muuzaji anakuambia hebu usinisumbue, kama unataka chukua kama hutaki acha. Utajisikiaje? Najua utajisikia vibaya sana, na kwa kuwa sasa hivi wauzaji wa chochote unachotaka ni wengi, basi utaenda kwa (more…)

UKURASA WA 1362; Tengeneza Ukuu Kwenye Kile Unachojali…

By | September 23, 2018

Kila kitu tunachofanya kwenye maisha yetu, kinaacha alama fulani kwetu na kwa wengine pia. Hakuna chochote unachofanya ambacho kitafutika kabisa kwenye maisha yako. Wapo watakaoona kile unachofanya, na kuendelea kuwa na kumbukumbu yetu kupitia kile tunachofanya. Sasa unapohitaji kujenga ukuu, unapohitaji kujenga umaarufu au sifa yako kwa wengine, kazana kufanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NDIYO YAKO NA HAPANA YA WENGINE…

By | September 23, 2018

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila (more…)

BIASHARA LEO; Fasheni Zinapita, Biashara Yako Ni Ya Kudumu…

By | September 22, 2018

Kama umechagua kuingia kwenye biashara, basi biashara yoyote unayochagua kufanya, angalia miaka mingi ijayo. Angalia miaka mitano ijayo, miaka kumi ijayo na hata miaka 50 ijayo. Je biashara hiyo itakuwepo na je itakuwa imekua zaidi kuliko sasa? Nakuambia hivi kwa sababu kuna uwekezaji mkubwa utakaouweka mwanzo wa biashara yako, uwekezaji (more…)

UKURASA WA 1361; Una Kila Unachohitaji Ili Kuanza…

By | September 22, 2018

Watu wengi wamekuwa wanakwama kwenye kuanza. Na kikubwa ambacho wengi wanasema kinawakwamisha ni kukosa kila wanachohitaji ili waweze kuanza. Watu wengi wanafikiri hawawezi kuanza mpaka wawe na kila wanachokitaka. Kitu ambacho hakiwezi kutokea kwa hali yoyote ile. Ni vigumu sana kupata kila unachotaka, hasa mwanzoni. Hivyo njia pekee ya kuanza, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNACHOPIGANA NACHO KINA NGUVU JUU YAKO…

By | September 22, 2018

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila (more…)

BIASHARA LEO; Jinsi Ya Kuondoa Ukomo Wa Kipato Kwenye Biashara Yako.

By | September 21, 2018

Watu wengi wanapoanza biashara, wanaona ukuaji wa kipato, ambao unawaridhisha sana na kuwapa hamasa ya kuweka juhudi zaidi. Wanaweka juhudi na kipato kinaongezeka zaidi, wanazidi kufurahi na kupata hamasa pia. Wanaongeza tena juhudi na muda wa kazi, na kipato kinaongezeka. Hapo wanajifunza kwamba ukiongeza juhudi na muda, basi kipato kinaongezeka. (more…)

UKURASA WA 1360; Ruhusa Na Msamaha…

By | September 21, 2018

Rafiki, nimewahi kukuandikia kwamba, kama kuna kitu kikubwa unachotaka kufanya kwenye maisha yako, kitu ambacho hujawahi kufanya na wala wengine hawajawahi kufanya, dunia haitakuruhusu kabisa ukifanye. Hivyo kama utaomba kwanza ruhusa, ukubali mpaka uruhusiwe ndiyo ufanye, hutapata ruhusa unayotaka, na hivyo hutaweza kufanya unachotaka. Badala yake, nilikuambia usiombe ruhusa, badala (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NGUVU INAYOKUVUTA CHINI….

By | September 21, 2018

“We must all wage an intense, lifelong battle against the constant downward pull. If we relax, the bugs and weeds of negativity will move into the garden and take away everything of value.” —Jim Rohn AMKA Mwanamafanikio, AMKA kwenye siku hii nyingine nzuri sana ya leo, Siku ambayo tumepata nafasi (more…)

BIASHARA LEO; Kuuza Vitu Vya Kawaida Kwa Watu Wa Kawaida…

By | September 20, 2018

Kwenye maisha, kitu ambacho ni rahisi kufanya, pia ni rahisi kutokufanya. Pia kitu ambacho ni rahisi kufanya, huwa hakina thamani kubwa, huwa hakilipi kama mtu anavyoweza kuwa anataka. Hivyo kwa kifupi, tunaweza kusema kuchagua kufanya vitu rahisi, ni kujiweka kwenye mstari wa kushindwa. Njia rahisi ya kuingia kwenye biashara ni (more…)