UKURASA WA 1144; Kuwa Makini Sana Na Mazingira Yanayokuzunguka….

By | February 17, 2018

Mazingira yanayotuzunguka, yana nguvu kubwa sana ya kutufanya vile tulivyo sisi. Japo wengi huwa hatulioni hili, na huwa tunafikiri kwamba tuna nguvu ya kuyashinda mazingira yetu. Ukweli ni kwamba hatuna nguvu hiyo. Mazingira ninayozungumzia hapa ni kila kinachokuzunguka, kuanzia watu, vitu na hata hali mbalimbali zinazokuzunguka. Kwa mfano kama unazungukwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TATIZO SIYO TUSI UNALOTUKANWA, TATIZO NI TAFSIRI YAKO KWA TUSI HILO…

By | February 17, 2018

It is not he who reviles or strikes you who insults you, but your opinion that these things are insulting. – Epictetus Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi (more…)

BIASHARA LEO; Kwa Nini Mitandao Ya Kijamii Haina Faida Kubwa Kwako Kibiashara Kama Unavyodhani.

By | February 16, 2018

Kwenye zama hizi za taarifa, wateja wanapaswa kuwa na taarifa sahihi za biashara yako ili waweze kuchukua hatua ya kuja kununua kwako. Na moja ya njia rahisi za kutoa taarifa za biashara yako ni kupitia mitandao ya kijamii. Kwa sasa karibu kila mtu mwenye simu, yupo kwenye mitandao hii ya (more…)

UKURASA WA 1143; Sababu Kuu Ya Kufanya Kazi Yako…

By | February 16, 2018

Kuna watu wanafanya kazi ili waonekane wanafanya kazi. Watu wa aina hii kazi zao huwa ni za juu juu na hazina thamani kubwa. Kwa sababu pale ambapo hakuna anayewaona, basi hawana msukumo wa kufanya kazi. Na mara nyingi kazi inakuhitaji uifanye wakati hakuna anayekuona. Wapo watu wanaofanya kazi ili wasifiwe, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; ADHABU KUBWA YA MKOSAJI…

By | February 16, 2018

The first and greatest punishment of the sinner is the conscience of sin. – Lucius Annaeus Seneca Asubuhi njema mwanamafanikio. Hongera kwa siku hii mpya na ya kipekee sana kwetu. Ni nafasi nyingine nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Ni kwa msingi wa NIDHAMU, (more…)

UKURASA WA 1142; Sheria Tatu Zinazoweza Kuyafanya Maisha Yako Kuwa Bora Sana…

By | February 15, 2018

Sheria huwa zinatengenezwaje? Ni baada ya watu kufanya mambo fulani, halafu matokeo yake yakaonekana siyo mazuri hivyo sheria inawekwa kuwazuia watu kufanya kitu hicho. Kwa mfano, watu kunywa pombe na kisha kuendesha magari au mashine hupelekea kupata ajali zaidi. Hivyo sheria inakuwa hairuhusiwi kunywa pombe na kisha kuendesha mashine au (more…)

UKURASA WA 1141; Hofu Ya Fedha Ni Upotevu Wa Muda…

By | February 14, 2018

Leo nakuambia kitu ambacho kinaweza kukuumiza, lakini ukweli lazima usemwe kama ulivyo. Ni mazoea kwetu kuwa na hofu juu ya fedha, hasa pale ambapo tunakuwa hatuna uhakika na kipato chetu, hatutajijengea uhuru wa kifedha na hatujui kesho itakuwaje. Labda huna kazi maalumu na hivyo hujui kwa hakika kipato chako cha (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KINATOKEA KAMA KINAVYOPASWA KUTOKEA…

By | February 14, 2018

Everything that happens happens as it should, and if you observe carefully, you will find this to be so. – Marcus Aurelius Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo (more…)

UKURASA WA 1140; Dhana Yako Ya Ubaya Na Uzuri Siyo Sahihi…

By | February 13, 2018

Kuna maeneo ya maisha yetu, ambayo tunajijua hatupo vizuri, lakini sasa si kweli kwamba hatupo vizuri kama tunavyofikiri. Kadhalika yapo maeneo ya maisha yetu ambayo tunajijua tupo vizuri, lakini na hapo pia hatupo vizuri kama tunavyofikiri. Kinachotokea ni kwamba huwa tunajiumiza sana kwa yale maeneo ambayo tunafikiri hatupo vizuri wakati (more…)