#TAFAKARI YA LEO; USHINDI UNALETA USHINDI ZAIDI…

By | October 15, 2017

Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Ni siku nyingine nzuri na ya kipekee ambapo tumepata nafasi ya kipekee ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu. Asubuhi (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Toa Changamoto Kwa Mambo Yaliyozoeleka…

By | October 14, 2017

KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. UKURASA; 101 -110. Socrates anasifika kwa mfano wake wa watu waliozaliwa na kukulia pangoni. Huku wakiwa wamefungwa minyororo wasiweze kugeuga. Wanaangalia ukuta na nyuma yao unakuja mwanga ambao unaonesha vivuli vya vitu kwenye (more…)

UKURASA WA 1018; Ubaya Na Uzuri Wa Fedha Uko Wapi?

By | October 14, 2017

Fedha, neno ambalo likitajwa kila mtu anapata hisia zake. Wapo ambao wanaona ni kitu kizuri na bora sana, kitu ambacho wapo tayari kukifanyia kazi maisha yao yote. Wapo ambao neno hilo likitajwa wanapata simanzi, wanaona ni kitu ambacho kimeharibu kabisa maisha yao. Kitu ambacho kimewatenganisha na wale wa muhimu, kuharibu (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Mbinu Saba Za Kufikiri Kwa usahihi.

By | October 13, 2017

KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. UKURASA; 91 – 100 Socrates alijenga sifa yake kupitia kufikiri kwa kina na kuuliza maswali mazuri. Hivi ni vitu viwili vinavyokosekana kwenye zama tunazoishi sasa, watu hawafikiri, wanapokea kila wanachoambiwa, kama kilivyo. Watu (more…)

BIASHARA LEO; Biashara Inaanza Kushindwa Ndani Na Siyo Nje…

By | October 13, 2017

Katika wakati wowote ule, huwa kuna mabadiliko yanayoendelea kwenye uchumi wa nchi na hata dunia kwa ujumla. Kuna wakati uchumi unakuwa vizuri na kuna wakati uchumi unakuwa vibaya. Kuna wakati watu wana uwezo mzuri wa kununua na kuna wakati ambapo watu hawana uwezo wa kununua. Haya ni mambo ambayo yamekuwa (more…)

UKURASA WA 1017; Acha Kufanya Kazi, Anza Kuzalisha…

By | October 13, 2017

Siku za nyuma kidogo, kuna rafiki yangu alikuwa ndiyo ameajiriwa kwa mara ya kwanza. Alipofika kazini alikuwa na hamasa kubwa ya kufanya kazi. Akatumwa kwenda mkoa fulani kikazi, alipofika kule alipanga kufanya kazi hiyo na kuikamilisha haraka ili arudi eneo lake la kazi. Alipoanza ufanyaji wake wa kazi wa kasi (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Fikiri Kwa Akili Yako…

By | October 12, 2017

KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. UKURASA; 81 – 90. Changamoto kubwa ambayo watu wanayo, na imekuwepo tangu enzi za Socrates ni watu kuamini sana maoni ya wengine. Watu wakishaambiwa kitu, hasa na watu ambao wapo juu yao, basi (more…)

UWEKEZAJI LEO; Kwenye Uwekezaji Waepuke Watu Wa Aina Hii…

By | October 12, 2017

Watu wengi wamekuwa wakipata hasara kwenye uwekezaji kwa sababu hawatumii akili zao kutafuta maarifa sahihi na kufanya maamuzi sahihi. Badala yake wamekuwa wakitegemea wengine wawafanyie hivyo. Wamekuwa wakisubiri wengine wawaambie nunua hisa hizi, utapata faida kubwa na kadhalika. Wengi wanabeba ushauri huo kama ulivyo, wananunua hisa fulani, au kuwekeza eneo (more…)