UKURASA WA 960; Usiishi Kwenye Hali Ya Haraka Kila Wakati…

By | August 17, 2017

Mwanafalsafa mmoja amewahi kunukuliwa akisema maisha ni kile kinachotokea wakati sisi tunakazana kufanya mambo mengine. Akiwa na maana kwamba, mengi tunayokazana kufanya siyo yanayotengeneza maisha yetu, bali vile tunavyoenda ndivyo tunavyotengeneza maisha yetu. Kwa bahati mbaya sana, huwa tunakazana na yale tunayofanya na kusahau kabisa vile tunavyoenda. Ndiyo maana mtu (more…)

UKURASA WA 959; Jitangazie Uhuru Huu Muhimu Sana Kwa Mafanikio Yako…

By | August 16, 2017

Kila mtu ana matarajio fulani kutoka kwako, kila mtu anataka uendeshe maisha yako kutokana na anavyotaka yeye, kulingana na anavyojia na hata alivyozoea. Lakini hebu jiulize ni watu wangapi wanaokuzunguka? Na je iwapo utataka kutimiza matarajio ya kila mtu, utakuwa na maisha ya aina gani? Ni dhahiri kwamba huwezi kuishi (more…)

💥#TAFAKARI YA LEO; CONSISTENCY….

By | August 15, 2017

MAKIRITA AMANI: Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nzuri na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora. Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA, ambao utatuwezesha kufanya makubwa kwenye maisha yetu na kufanikiwa. Asubuhi ya leo tutafakari (more…)

UKURASA WA 958; Kesho Inapuuza Vitu Hivi Viwili…

By | August 15, 2017

Kila mtu ana hisia na maoni yake juu ya jambo lolote lile. Ndiyo maana huwa hakitokei kitu watu wakakosa la kusema na kuhisi pia. Watu watajigawa wenyewe, wale ambao watakubaliana na kitu, kukisifia na kutafuta kila ushahidi wa kuonesha kwamba kitu kile ni sahihi na kweli kabisa. Kuonesha kwamba ndiyo (more…)

UKURASA WA 957; Ongea Unavyotaka, Lakini Watu Watasikia Wanachotaka Kusikia…

By | August 14, 2017

Moja ya eneo lenye changamoto kubwa sana kwenye maisha yetu ni mawasiliano. Unaweza kuongea kitu kwa nia njema kabisa, lakini wengine wakatafsiri kuwa cha nia mbaya na ukaonekana wewe ni mbaya. Hii ni hali ya kawaida kabisa, hivyo kabla hujalalamika au kujitetea kwenye hilo, unapaswa kwanza kulielewa kwa undani. Watu (more…)

💥#TAFAKARI YA LEO; KAZI NZURI NA ISIYOCHOSHA…

By | August 13, 2017

MAKIRITA AMANI: Habari za asubuhi ya leo rafiki? Ni siku nyingine nzuri sana ya leo ambapo tumepata nafasi nzuri ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa. Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; THAMANI IPO KWENYE KUPOTEZA…

By | August 13, 2017

Habari za asubuhi ya leo rafiki? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo, nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu. Asubuhi (more…)

UKURASA WA 956; Usijioneshe, Bali Onekana…

By | August 13, 2017

Mtu mmoja amewahi kunukuliwa akisema watu huingia kwenye matatizo pale wanapotumia fedha ambazo hawana, kununua vitu ambavyo hawavihitaji ili kuwaridhisha watu ambao hawajali. Umeliona mara ngapi hilo? Labda kama hujaelewa vizuri hapo kwenye huo usemi, ni kwamba watu wengi wamekuwa wanakopa vitu ili kujionesha kwa wengine kwamba na wao wana (more…)