UKURASA WA 939; Sikiliza Zaidi Ya Unavyoongea…

By | July 27, 2017

Mwanasaikolojia mmoja amewahi kusema, watu hawawezi kuficha siri. Kama ataficha kwa maneno, basi matendo yake yataonesha. Kama atajipanga asionekane hata kwa matendo, basi hata sauti yake itaonesha siri inayofichwa. Lakini huwezi kujua hayo, kama hujui jinsi ya kuyajua. Na jinsi pekee ya kujua hayo mazito, ni kusikiliza zaidi ya unavyoongea. (more…)

BIASHARA LEO; Kuwa Makini Unapoingia Kwenye Biashara Mpya, Hata Kama Umeshazoea Biashara…

By | July 26, 2017

Kila biashara ina changamoto zake, hii ina maana kwamba kama umekuwa kwenye biashara fulani kwa kipindi kirefu, na umeshajifunza na kuzoea biashara, haimaanishi unaweza kufanya kila aina ya biashara. Utakuwa na unafuu ukilinganisha na ambaye hajawahi kufanya biashara kabisa, lakini bado unahitaji kujifunza kwenye kila biashara mpya unayoingia. Watu wengi (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; SUBIRI….

By | July 26, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa, ili kuweza kupata matokeo makubwa. Msingi wetu mkuu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA, tupambane sana na msingi huu kwani ndiyo utakaotuwezesha kufikia mafanikio makubwa. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu SUBIRI… (more…)

UKURASA WA 938; Nyakati Ngumu Ndiyo Za Kutengeneza Maana.

By | July 26, 2017

Kitu kikiwa rahisi sana, tunakizoea na kuona cha kawaida, hatukipi heshima ya kutosha, thamani yake inakuwa ndogo kwetu na hatukifurahii. Hii ni saikolojia ya binadamu, ambayo usipoielewa vizuri, maisha yako wakati wote yatakuwa magumu, hata ufanye nini. Watu huwa tunalalamikia ugumu na changamoto mbalimbali tunazopitia kwenye maisha, tunatamani mambo yangekuwa (more…)

UKURASA WA 937; Usishindane Na Mtu Huyu…

By | July 25, 2017

Kwanza kabisa, msimamo wako muhimu kwenye maisha unapaswa kuwa ni kutokushindana. Usishindane, hakuna jema linalopatikana kwenye kushindana. Hatua bora unayoweza kuchukua ni kuwa tofauti, kujitofautisha na wengine na hata pale ushindani unapokuja kwako kabisa, angalia njia gani ya kuwa bora zaidi. Lakini hayo yote yanaposhindikana, pale inapokubidi ufanye kitu ili (more…)

BIASHARA LEO; Maana ya neno HAPANA kwenye biashara…

By | July 24, 2017

Kama unafanya biashara na hujawahi kuambiwa neno HAPANA, huenda kuna makosa unafanya kwenye biashara yako. Labda unaifanya kwa viwango vya chini sana, au huna mpango wa kuikuza. Lakini kwa kawaida, neno HAPANA utalisikia sana kwenye biashara, mno yaani. Na utalisikia kwa kila mtu, kuanzia wateja wako, wafanyabiashara wengine, washirika wako, (more…)

UKURASA WA 936; Tatizo Ni Kutafuta Furaha Sehemu Ambapo Haiwezi Kupatikana…

By | July 24, 2017

Watu wengi wamekuwa wanaihusisha furaha na mafanikio, lakini siyo mafanikio kama mafanikio, bali mafanikio ya vitu, fedha, mali na kadhalika. Na hapo ndipo utawasikia wengi wakisema fedha hazileti furaha, au utajiri hauleti furaha, au mali hazileti furaha. inakuwa sahihi kabisa kwa sababu watu wanakuwa wanafanya kosa la kutafuta furaha sehemu (more…)

BIASHARA LEO; Teknolojia Pekee Mteja Anayojali Kwenye Biashara Yako Ni Hii.

By | July 23, 2017

Kila ninapokuwa nawauliza watu nini kinawazuia kuingia kwenye biashara, majibu huwa yananishangaza mno. Watu huwa wanataja vitu ambavyo unashangaa vinawezaje kumzuia mtu asiingie kwenye biashara anayotaka kuingia. Watu wengi wamekuwa wakisubiri mpaka wawe kamili kwa kila kitu, mpaka waandae na vipeperushi vya kuwavutia wateja ndiyo waanze biashara rasmi. Lakini unajua (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; UNACHOKOSA SIYO APP, BALI NIDHAMU…

By | July 23, 2017

Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nzuri na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa, ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya nakubwa sana leo na kila siku. Asubuhi (more…)