💥 #TAFAKARI YA LEO; NJIA YA KUTAJIRIKA HARAKA BILA KAZI…

By | July 30, 2017

Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo rafiki yangu. Ni nafasi nyingine nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora sana. Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu NJIA YA KUTAJIRIKA HARAKA (more…)

UKURASA WA 942; Kinachokupoteza Ni Vipaumbele…

By | July 30, 2017

Mwandishi mmoja amewahi kuandika kwamba neno kipaumbele kwa Kiingereza, zamani halikuwa na wengi, yaani lilikuwa ni priority na hakukuwa na priorities. Alisema vikishakuwa vipaumbele basi maana yake halisi inapotea. Kinapaswa kuwa kipaumbele, kitu kimoja ambacho unakipa nafasi na kuachana na vitu vingine vyote kwa wakati huo. Nimekuwa nafikiria hilo kwa (more…)

BIASHARA LEO; Miaka 20 Ijayo Mteja Atakutafuta?

By | July 29, 2017

Watu wote ambao wanaingia kwenye biashara kwa msukumo wa kupata faida pekee, huwa hawadumu muda mrefu. Ni sheria ya dunia kwamba chochote ambacho hakipo kwenye misingi sahihi, kinaanguka. Wale wanaofikiria faida pekee, wanafanya kila wawezalo kupata faida, hata kama linaharibu mahusiano na wateja. Kipimo kizuri sana kwako kuepuka hilo ni (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; UNAMWANGALIA NANI?

By | July 29, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa, ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu UNAMWANGALIA NANI? Katika maisha yetu (more…)

UKURASA WA 941; Juhudi Hizo Weka Kwenye Kila Eneo La Maisha Yako…

By | July 29, 2017

Juhudi kubwa unazoweka katika kuhakikisha unakuwa na kipato cha kutosha, ni juhudi hizo hizo unapaswa kuweka kwenye kuhakikisha mahusiano yako na watu wengine ni bora, afya yako ni bora, imani yako iko vizuri na kila kitu kinachokuhusisha wewe, kinaenda kwa ubora wa hali ya juu. Huwezi kuwa bora sana kwenye (more…)

BIASHARA LEO; Malengo Yako Kibiashara Yanakusukuma Kiasi Gani?

By | July 28, 2017

Moja ya sababu za biashara nyingi kudumaa, yaani biashara kuwa pale pale miaka nenda miaka rudi, ni wamiliki wa biashara hizo kuwa na malengo ambayo hayaendani na biashara zao. Labda malengo yanakuwa madogo sana, kiasi kwamba wanayafikia bila ya kuhitaji juhudi za ziada. Kwa mfano kama unataka biashara ikupe hela (more…)

UKURASA WA 940; Kuna Kitu Unaweza Kufanya…

By | July 28, 2017

Tofauti ya wale wanaoweza kufanya makubwa licha ya kuwa na changamoto na wale wanaokata tamaa na kuacha, siyo ukubwa wa changamoto, wala siyo uwezo wa kifedha au kiakili, bali ni tofauti ya mtazamo. Wale wanaokata tamaa na kuacha ni wale ambao wakikutana na changamoto wanajiambia hakuna ninachoweza kufanya. Nimejaribu sana (more…)

BIASHARA LEO; Mteja Mmoja Baada Ya Mwingine…

By | July 27, 2017

Kosa kubwa ambalo wafanyabiashara wapya wamekuwa wanafanya ni kutaka siku ya kwanza ya biashara wawe na wateja wengi, waliopanga foleni kusubiri kuhudumiwa. Hilo halijawahi kutokea, hivyo achana nalo, kama ndiyo unaanza biashara au unapanga kuanza biashara. Hata kama watu wanakuahidi kiasi gani kwamba watanunua kwako, ukweli unaupata unapoanza biashara, hutawaona. (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; KUONEKANA NA WEWE UPO…

By | July 27, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana kwetu. Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUONEKANA NA WEWE UPO… (more…)