KITABU; KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, TOLEO LA KWANZA 2016.

By | June 11, 2016

Habari njema kwa wana mafanikio wote, kitabu chako ambacho ndio mwongozo wa maisha ya mafanikio kwa mwaka huu 2016 tayari kimetoka. Kitabu hiki kinaitwa KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO. Hiki ni kitabu ambacho kinakupatia wewe maarifa sahihi ya kuishi maisha ya mafanikio, kwa vyovyote vile unavyoyapima mafanikio kwenye maisha yako. (more…)

KITABU; JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.

By | June 11, 2016

Kama kuna kitu kimoja ambacho tuna uhakika nacho hapa duniani ni kwamba dunia inabadilika kila siku. Ukiangalia historia ya dunia tulikotoka na tulipo sasa kumetokea mabadiliko makubwa sana. Zilianza zama za mawe, zikaja zama za chuma, yakaja mapinduzi ya viwanda na hata sasa tupo kwenye mapinduzi ya kiteknolojia. Jambo moja (more…)

KITABU; JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG.

By | June 11, 2016

Tunaishi kwenye ulimwengu wa zama za taarifa. Katika ulimwengu huu wale wenye taarifa sahihi ndio wanaonufaika kuliko wale ambao hawana taarifa sahihi. Pia katika ulimwengu huu taarifa watu wengi wameweza kunufaika kwa kuuza taarifa ambazo wanazo na wengine wanazihitaji. Je na wewe upo tayari kunufaika na taarifa ulizonazo, ambazo zinaweza (more…)

KITABU; KWA NINI MPAKA SASA WEWE NI SIO TAJIRI.

By | June 11, 2016

Madhumuni ya kuandika kitabu hiki ni kuwasaidia wale wote wenye malengo ya kufanikiwa kwenye maisha yao na kuwa matajiri. Kwa bahati mbaya sana kwenye mfumo wa elimu hakuna sehemu ambapo tunafundishwa somo linalohusiana na kutengeneza utajiri. Wachache wanaojua siri za kupata utajiri wamekuwa wakinufaika nazo na wengi ambao hawajui siri (more…)

UKURASA WA 526; Taka Kile Ulichonacho…

By | June 11, 2016

Sisi binadamu huwa tunaweka juhudi kubwa sana kwenye kutafuta kile ambacho tunakitaka, na kwa juhudi hizi tunakipata. Lakini tatizo linaanza baada ya kupata kitu hiko, tunakizoea na kuona hakina maana tena. Badala yake tunaanza kufikiria kingine ambacho hatuna na hivyo kutaka, tunakazana kukipata lakini tukishakipata tunakizoea na mchezo unaendelea hivyo. (more…)

UKURASA WA 524; Haraka Siyo Nzuri…

By | June 9, 2016

Vyakula vyote unavyoweza kuvitengeneza kwa haraka, na kula kwa haraka siyo vyakula vizuri kiafya. Mwendo wa haraka siyo mwendo salama kiafya. Njia ya haraka ya kufikia mafanikio huwa haileti mafanikio ya kudumu. Suluhisho la haraka la matatizo yetu huwa linatengeneza matatizo makubwa zaidi baadaye. Majibu ya haraka kwenye swali lolote (more…)

UKURASA WA 523; Kipimo Halisi Cha Kujifunza…

By | June 8, 2016

Kipimo halisi cha kujifunza ni kubadili tabia. Haijalishi unajua kiasi gani, kama tabia yako haiendani na kile unachojua, basi unachojua hakina msaada wowote kwako. Na hiki ndiyo kipimo cha hekima, hekima haitokani na kujua bali kufanyia kazi kile ambacho unakijua. Kwa mfano mtu ambaye ni daktari wa binadamu, anajua kabisa (more…)

UKURASA WA 522; Kila Mtu Anataka Wewe Ushindwe…

By | June 7, 2016

Jambo moja ambalo unaweza usifurahi sana kulisikia ni kwamba kila mtu anataka wewe ushindwe. Ndiyo kila mtu, hasa wale wa karibu zaidi kwako, ndiyo wanataka ushindwe zaidi. Pale unapochagua kufanya mambo makubwa, ambayo wengine hawayafanyi, kila mtu atataka wewe ushindwe. Hii ni kwa sababu kama ukiweza kufanikiwa kufanya, wao watajisikia (more…)

Sababu tatu kwa nini biashara nyingi zinakufa haraka.

By | June 6, 2016

Kati ya watu wengi wanaoingia kwenye biashara kila mwaka, ni wachache sana wanaoweza kuendeleza biashara zao na zikaweza kufikia ngazi kubwa ya mafanikio. Watu wengi wamekuwa wanaishia katikati na kufunga biashara zao. Na wale ambao hawazifungi, wanakuwa wanaziendesha bila ya faida au kwa faida kidogo kiasi cha kushindwa kuzikuza zaidi. (more…)