UKURASA WA 521; Mateso Siyo Mashindano…

By | June 6, 2016

Unapoendesha maisha yako ndani ya jamii kuna vitu vingi unatakiwa kuwa makini navyo. Kuna vitu ambavyo watu wamekuwa wanafanya kwa mazoea tu, huwa haiulizwi kwa nini inafanyika. Usipokuwa makini unajikuta unafanya vitu ambavyo havina manufaa yoyote kwako. Moja ya vitu ambavyo vimekuwa vinachukuliwa kama ni kitu cha kawaida wakati siyo (more…)

Ujue Uwekezaji Kwenye Hatifungani (BONDS) Na Faida Zake.

By | June 5, 2016

Nachukua nafasi hii kuwakaribisha kwenye darasa la leo ambapo tutakwenda kujifunza kuhusu uwekezaji wa HATI FUNGANI kwa kiingereza BONDS. Katika darasa la leo tutajifunza yafuatayo; 1. Maana ya uwekezaji kwenye masoko ya mitaji. 2. Maana ya uwekezaji kwenye hatifungani. 3. Mfumo wa uwekezaji wa hati fungani na faida zake. 4. (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Kwa Nini Hisia Bado Zinatushinda Kudhibiti Na Namna Ya Kuzidhibiti.

By | June 5, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Karibu kwenye kipengele chetu cha FALSAFA MPYA YA MAISHA ambapo tunashirikishana mbinu za kujenga falsafa ambayo itatuwezesha kuwa na maisha bora na yenye mafanikio makubwa. kile tunachotaka kinaanzia ndani yetu na tunapokuwa na falsafa imara tunaweza kujenga maisha imara. Leo tunakwenda kuangalia kitu kimoja ambacho (more…)

UKURASA WA 520; Kabla Hujafanya Maamuzi…

By | June 5, 2016

Kabla hujafanya maamuzi yoyote muhimu kwenye maisha yako, hakikisha una taarifa zote muhimu kuhusu jambo hilo. Unapokuwa na taarifa sahihi kuhusu jambo unakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanya maamuzi sahihi kwako ambayo yatakupatia kile unachotaka. Changamoto kubwa ni kwamba watu wanaotaka wewe ufanye maamuzi ambayo yatawanufaisha wewe, hawakupi taarifa sahihi (more…)

UKURASA WA 519; Barabara Lazima Zifagiliwe…

By | June 4, 2016

Tunapozungumzia mafanikio, wapo wengi ambao huwa wanafikiri kwamba watafanikiwa kama watafanya kazi fulani ambazo kwa nje zinaonesha mafanikio. Labda kama akiwa daktari au rubani au injinia ndiyo ataweza kufanikiwa. Huu sio ukweli, mafanikio tunayozungumzia hayatoki nje yako, bali yanaanzia ndani yako. Mafanikio yako yanaanza na kile ambacho unakifanya sasa, pale (more…)

UKURASA WA 518; Je unauzika?

By | June 3, 2016

Kabla watu hawajanunua kile unachouza, wanakununua wewe kwanza. Kabla watu hawajakubali kile unachowaambia, lazima wakukubali wewe kwanza. Kwa asili binadamu tunapenda kuhusiana na wale ambao tunawajua vizuri, na tunajua wanaendana na sisi. Watu ambao wanaonekana ni wageni kwetu wanatupa wasiwasi. Hatuna hakika kama wanajali maslahi yetu au wanataka kututapeli. Hivyo (more…)

UKURASA WA 517; Unavyopoteza Uhuru Wako…

By | June 2, 2016

Kitu muhimu sana kwenye maisha ni kuwa na uhuru, kuweza kuyaendesha maisha yako kwa vile unavyotaka wewe bila ya kuingilia maisha ya wengine ni kitu muhimu sana. Maisha yenye uhuru ndiyo maisha yenye furaha na mafanikio. Lakini wengi wanakosa uhuru huu na sio kwa kunyang’anywa bali kwa kuamua kuupoteza wao (more…)

UKURASA WA 516; Ongozwa Na Matokeo…

By | June 1, 2016

Unawezaje kujua kama maisha yako ni bora kama ambavyo umekuwa unataka kuwa na maisha bora? Jibu ni rahisi, unaangalia matokeo unayopata kwenye maisha yako. Kama yanaendana na vile unavyotaka basi una uhakika maisha yako ni bora. Kama yanakwenda kinyume, kuna tatizo mahali. Njia bora ya kupima kile unachofanya na kuangalia (more…)

UKURASA WA 515; Bure…

By | May 31, 2016

Neno bure ni njia rahisi ya kuwapata watu kulipa gharama kubwa. Ni neno ambalo linaweza kuwashawishi watu kuchukua hatua ambazo siyo bora kwao. Kwa sababu watu wengi wanapenda njia rahisi. Kitu chochote unachoambiwa unapewa bure, chunguza kwa makini, kuna gharama kubwa utakazoingia kwa kukubaliana na kitu hiko. Huenda ikawa ubora (more…)

Mambo ya kuzingatia ili kupata wawekezaji kwenye biashara yako.

By | May 30, 2016

Mtaji wa fedha ni eneo muhimu kwa biashara yoyote. Ili uweze kuanza au kukuza biashara yako, mtaji wa fedha unahitajika. Inawezekana ukawa ni mtaji kidogo au mkubwa kulingana na wazo la biashara ulilonalo. Kwa wajasiriamali na wafanyabiashara, wengi hawana kiasi cha fedha cha kutosha kuanzisha au kukuza biashara zao. Na (more…)