UKURASA WA 532; Mambo Yanapokwenda Mrama…

By | June 17, 2016

Katika maisha yetu kuna maamuzi ambayo huwa tunafanya na tunakuwa tumekosea, kwa kukosea maamuzi hayo tunapata matokeo mabaya, yaani mambo yanakwenda vibaya. Sasa hapa ndipo penye hatari kubwa sana. Hapa kuna hatari kubwa kwa sababu mambo yanapoanza kuharibika, huwa tunakaza na kuchukua hatua haraka sana, na kwa bahati mbaya sana (more…)

UKURASA WA 531; Watu Wanaokera…

By | June 16, 2016

Kuna watu ambao wametuzunguka, kwenye kazi zetu, biashara zetu na hata maisha yetu ya kawaida ambao huwa wanakera. Yaani watu hawa unatamani hata wasingekuwa karibu na wewe kwa sababu kila kitu wanachofanya wanakukera sana. Wengine wanaweza hata kukuharibia siku yako na kukupotezea muda wako kutokana na mambo ambayo wanayafanya. Watu (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; Getting Results The Agile Way (Mbinu Za Kuwa Na Matumizi Mazuri Ya Muda Na Kupata Ufanisi Mkubwa.)

By | June 15, 2016

Kama kuna kitu kimoja ambacho kila mtu anapigania kwenye maisha haya ni kuweza kutumia muda vizuri na kupata matokeo bora, kuwa na ufanisi mkubwa kwenye shughuli mbalimbali. Matumizi mazuri ya muda kwa sasa imekuwa ni changamoto kutokana na kuongezeka kwa mambo yanayohitaji muda wetu huku muda ukibaki ule ule. Kumekuwa (more…)

UKURASA WA 530; Wasaidie Kuondokana Na Hofu Ya Kutokujua…

By | June 15, 2016

Mteja yeyote anayekuja kununua kwenye biashara yako kwa mara ya kwanza anakuwa na hofu kama kweli kile unachotaka kumuuzia kitamsaidia, au kitakuwa na sifa ambazo unazisema. Anachukua hatari kubwa sana kununua kwa mtu ambaye hamjui kabisa. Mtu yeyote anayekuajiri kwa mara ya kwanza anakuwa na hofu kama kweli utaweza kutimiza (more…)

UKURASA WA 529; Fedha Na Uhuru…

By | June 14, 2016

Uhuru ndiyo kitu ambacho tunakipigania na kukitafuta, kwa sababu uhuru kwenye maisha ndiyo unaotuwezesha kuishi yale maisha ya ndoto yetu, ambayo ni bora na yenye furaha. Kwa bahati mbaya sana kwenye jamii zetu, uhuru umewekwa pamoja na fedha. Kwamba kama unataka kuwa huru basi unahitaji kuwa na fedha nyingi, tafuta (more…)

Njia bora za kutatua hali ya kutoelewana baina yako na mteja wako.

By | June 13, 2016

Biashara zina changamoto mbalimbali katika uendeshaji. Zile biashara ambazo unaona zimekua na kufanikiwa, siyo kwamba hazina changamoto ila waendeshaji wa biashara hizo wanajua jinsi ya kukabiliana na changamoto za kibiashara wanazokutana nazo. Moja ya changamoto ambazo zinasumbua biashara nyingi ni hali ya kutokuelewana baina ya mteja na mfanyabiashara. Kuna nyakati (more…)

UKURASA WA 528; Watakie Watu Mema Na Furaha…

By | June 13, 2016

Tuliona ya kwamba watu wanaokuzunguka wanataka wewe ushindwe, hasa pale unapopanga kufanya mambo makubwa, ambayo wao hawakuweza kufanya. Lakini hili halitokei kwa wengine pekee, hata kwako pia linatokea. Kuna nyakati ambapo unatamani mtu ashindwe au apate changamoto kwenye jambo analofanya. Hasa pale anapojaribu kufanya jambo kubwa, au anapopingana na kile (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Changamoto Za Kuondoka Kwenye Vifungo Vya Maisha Na Kupata Uhuru Wa Maisha.

By | June 12, 2016

Maisha bora, yenye furaha na mafanikio yanaanza na pale mtu anapokuwa huru kwenye maisha. Ndiyo maana kuna watu wengi ambao kwa nje wanaweza kuonekana wamefanikiwa lakini ndani yao wanaona maisha yao bado hayapo kama ambavyo walitaka yawe. Uhuru wa maisha ndiyo unaoleta kila kitu kwenye maisha, lakini pia uhuru huu (more…)

UKURASA WA 527; Punguza Maamuzi Unayofanya…

By | June 12, 2016

Moja ya vitu ambavyo vinamaliza nguvu zetu ni idadi ya maamuzi tunayofanya. Ubongo wetu ndiyo kiungo cha miili yetu ambacho kinatumia sehemu kubwa ya nguvu ya mwili. Na kwa kuwa ubongo ndio unaohusika kwenye maamuzi, kadiri unavyofanya maamuzi mengi ndivyo nguvu nyingi inavyotumika. Miili yetu kwenye nguvu ni kama betri. (more…)

KITABU; BIASHARA NDANI YA AJIRA, JINSI YA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA YAKO UKIWA BADO UMEAJIRIWA.

By | June 11, 2016

BIASHARA NDANI YA AJIRA ni kitabu ambacho kinakupa mbinu za kuanzisha na kukuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa. Ni kitabu ambacho kila mwajiriwa anapaswa kukisoma kwa sababu kina maarifa muhimu ya kumwezesha mwajiriwa kujikomboa kiuchumi. Wote ni mashahidi kwamba hali ya ajira kwa sasa imebadilika sana. Na kipato cha ajira (more…)