UKURASA WA 507; Kupata Unachotaka, Fanya Usichotaka…

By | May 23, 2016

Jambo moja la kushangaza kuhusu maisha ni kwamba ili uweze kupata kile unachotaka, ni lazima ufanye kile usichotaka kufanya. Huu ndiyo ukweli wa maisha na hakuna namna unaweza kuukwepa. Kama unataka kuwa na afya bora ni lazima ule vyakula ambavyo hupendi kula, mara zote vile vyakula unavyopendelea kula huwa siyo (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Kinachotuzuia Kuujua Ukweli Na Hivyo Kushindwa Kuwa Na Maisha Bora.

By | May 22, 2016

Ujue ukweli nao utakuweka huru… Hii ni falsafa ambayo imekuwepo tangu zamani, na ni falsafa nzuri sana kwa kuwa na maisha bora na ya mafanikio. Lakini kwa bahati mbaya sana wengi tunashindwa kuitumia na hivyo kushindwa kuwa na maisha bora. Wote tunajua ya kwamba uhuru ndiyo kitu muhimu sana kwenye (more…)

UKURASA WA 506; Simama Mwenyewe…

By | May 22, 2016

Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii, inakuwa rahisi kwetu kufanya jambo kama kila mtu anakubaliana na sisi na yupo tayari kutusaidia. Ni salama zaidi kufanya kile ambacho kila mtu anafanya, au wanakushauri kufanya. Kwa sababu kama utashindwa basi watakusaidia. Lakini hivi unavyolazimika kufanya siyo vile ambavyo ni bora kwako, na (more…)

UKURASA WA 505; Zaidi Ya Kawaida…

By | May 21, 2016

Watu wengi wanaishi maisha yao yote bila ya kujijua wao wenyewe. Hawajui uwezo mkubwa ulio ndani yao na wanaondoka kwenye dunia hii wakiwa bado hawajatumia uwezo wao huo. Kwa kufanya kile ambacho kila mtu anafanya, au ulichochagua kufanya lakini unafanya kwa hali ya kawaida, huwezi kujijua wewe mwenyewe. Unaishia kufanya (more…)

UKURASA WA 504; Kile Unachokitaka Hasa….

By | May 20, 2016

Kile unachokitaka hasa, ndiyo unachokwenda kukipata, ndivyo maisha yalivyo. Hupati tofauti na unachotaka. Na hivyo kile unachotaka ndicho kinastahili muda wako na mawazo yako. yafanye mawazo yako kutawaliwa na kile ambacho unakitaka, na tumia muda wako kufanya kitu hiko. Tunaishi kwenye dunia yenye kelele na mengi yanayotaka akili zetu na (more…)

UKURASA WA 503; Msingi Wa Hasira…

By | May 19, 2016

Siyo vibaya kukasirika, kama unaweza kuzidhibiti hasira zako. Kama utaweza kujizuia usichukue hatua kutokana na hasira ulizonazo, kwa sababu hatua unazochukua wakati ukiwa na hasira, huwa siyo hatua nzuri. Hili ni jambo muhimu sana la kuzingatia pale unapokuwa umekasirika. Leo tunakwenda kuchimba ndani na kuangalia ni upi hasa msingi wa (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; DEEP WORK (Mbinu Za Kufanya Kazi Yenye Maana Kwenye Zama Hizi Za Usumbufu).

By | May 18, 2016

Ukweli ni kwamba tunaishi kwenye zama ambazo kuna usumbufu wa hali ya juu sana. Sasa hivi mtu yeyote anaweza kukusumbua muda wowote anaoamua wewe. Ukuaji wa teknolijia na mtandao na ujio wa mitandao ya kijamii pamoja na simu janja (smartphone) umefanya iwe rahisi sana kusumbuliwa. Tunasumbuliwa kwa simu zisizokuwa muhimu, (more…)

UKURASA WA 502; Kuweza Kufanya Na Kufanya….

By | May 18, 2016

Kuweza kufanya na kufanya ni vitu viwili tofauti kabisa. Watu wengi wanasema wanaweza kufanya, lakini cha kushangaza huwaoni wakifanya. Wanasubiri mtu mwingine afanye halafu wao ndiyo waje kukosoa, ya kwamba hata wao wangeweza kufanya vizuri zaidi ya vile ambavyo wengine wanafanya. Pande mbili za jambo hili. Upande wa kufanya. Kama (more…)

UKURASA WA 501; Njia Mbili Za Kuwa Mbele Ya Wengine…

By | May 17, 2016

Katika jambo lolote ambalo unachagua kufanya, kuna wengine wengi ambao nao pia wanalifanya. Inawezekana umeanza kufanya kwa sababu uliona wengine wanafanya au wengine wamekuona wewe unafanya na wao wakaanza kufanya. Hivyo ushindani ni kitu ambacho huwezi kukikimbia. Kama unavyojua, kushindana moja kwa moja ni kitu ambacho sikushauri ufanye kwa sababu (more…)

Vitu vinne vinavyochangia thamani na kipato cha biashara yako.

By | May 16, 2016

Kujua thamani ya biashara yako na kipato unachoweza kuingiza kupitia biashara hiyo ni moja ya vitu muhimu unavyotakiwa kuzingatia. Na kama ukiweza kufanya hivi kabla hujaanza biashara yako unaweza kuianza ukiwa na mpango bora wa kutoa thamani kubwa na kutengeneza kipato kizuri.  Watu wengi wamekuwa wanaingia kwenye biashara na kufanya (more…)