UKURASA WA 514; Uliyekuwa Unamsubiri Ameshafika.

By | May 30, 2016

Pale tunapotaka kuwa na maisha bora na yenye mafanikio makubwa, tunajua tunahitaji kufanya mambo makubwa ambayo hatujawahi kufanya hapo awali. Na hapa ndipo tunagundua ya kwamba hatuna uwezo huo na hivyo kuhitaji uwezo kutoka nje yetu. Tulipokuwa watoto tulikuwa tunajipa sababu ya udogo na hivyo kusema tukiwa wakubwa tutafanya kitu (more…)

UKURASA WA 513; Anayesababisha Ushindwe…

By | May 29, 2016

Kuna mtu ambaye amekuwa anasababisha wewe unashindwa kwenye mipango yako mbalimbali unayojiwekea. Mtu huyu amekuwa anavuruga furaha ya maisha yako na kuyafanya yawe magumu zaidi. Mtu huyu amekuwa kikwazo kwako kufikia yale malengo ambayo umejiwekea. Lakini uzuri ni kwamba mtu huyu unaweza kumdhibiti. Ili uweze kumdhibiti mtu huyu unatakiwa kumjua (more…)

UKURASA WA 512; Maana Halisi Ya Utajiri…

By | May 28, 2016

Kuna watu hawapendi kusikia neno utajiri, yaani ni kama wana ‘allergy’ na neno hilo. Na siyo jambo la kushangaza kwa sababu ukiweka mambo ya kijamii na kidini pia, kuna mkanganyiko mkubwa. Wengine watakuambia siyo kila mtu anaweza kuwa tajiri, kwa hiyo wanachagua wao kuwa upande wa masikini. Wengine watakuambia masikini (more…)

UKURASA WA 511; Machaguo Yanapokuwa Mengi…

By | May 27, 2016

Machaguo yanapokuwa mengi, akili inachoka na hivyo uwezo wa kufanya maamuzi sahihi unapungua. Hii ndiyo changamoto kubwa kwenye ulimwengu wa sasa ambapo machaguo ni mengi na kila siku yanazidi kuongezeka. Leo hii ukitaka kununua kitu, utakuta vipo vitu vya aina nyingi, kujua kipi ununue ni changamoto ambayo inaweza kukuchosha kuamua (more…)

UKURASA WA 510; Ni Asilimia Moja (1%)

By | May 26, 2016

Watu wengi wamekuwa wakifikiri kwamba ili waweze kubadili maisha yao basi wanahitaji kufanya mapinduzi makubwa sana ndani ya muda mfupi. Wanakuwa wanawaangalia wale ambao wameshapiga hatua na kuona kwamba wakiweza kupiga hatua moja pekee watakuwa mbali sana. Lakini hivi sivyo mambo yanavyokwenda, hakuna mtu anayeweza kufanya mabadiliko makubwa ndani ya (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; FAIL FORWARD (Hatua 15 Za Kufikia Mafanikio Kupitia Kushindwa).

By | May 25, 2016

Ni rahisi sana kuona watu waliofanikiwa na kusema na wewe unataka ufanikiwe kama wao. Lakini unapoianza safari ya mafanikio ndipo unapogundua kuna mengi hukuyajua. Kuna mengi sana ambayo utayashindwa kwenye safari yako hiyo na kama utakuwa hujajiandaa vizuri hutafika mbali. Watu waliofanikiwa hawakufika walipo kwa mara moja tu, bali wamevuka (more…)

UKURASA WA 509; Kitu Kimoja Ambacho Walioshindwa Wote Wanacho….

By | May 25, 2016

Kwenye tafiti za kisayansi, kama kwenye kila tukio kuna kitu fulani, basi kitu hiko ndiyo kinachangia kutokea kwa tukio hilo. Kwa mfano kama imetokea kwenye eneo fulani watu wameanza kuharisha ghafla, na kila anayeharisha akipimwa anaonekana kuwa na vijidudu vya aina fulani, basi kuna uwezekano mkubwa vijidudu vile ndiyo vimepelekea (more…)

ONGEA NA KOCHA; Jambo Muhimu La Kuzingatia Kabla Hujahukumu.

By | May 24, 2016

Habari za leo rafiki? Karibu kwenye mazungumzo yetu ambapo tunakwenda kushirikishana mambo mbalimbali ambayo ni muhimu kwetu ili kuweza kuishi maisha bora, ya furaha na mafanikio makubwa. Katika mazungumzo ya leo tutakwenda kuangalia upande wa hukumu ambazo tumekuwa tunazitoa kila siku. Kama kuna kitu ambacho binadamu tupo vizuri, basi ni (more…)

UKURASA WA 508; Kufanikiwa Kwenye Kila Kitu Ni Hatari…

By | May 24, 2016

Lengo la kila mmoja wetu ni kufanikiwa, kuwa bora zaidi ya tulivyo sasa na kufikia hatua ambazo kwa sasa bado hatujazifikia. Lakini kama kwenye kila kitu unachofanya unafanikiwa, kama kila lengo unaloweka unalifikia ni hatari kubwa sana. Unaweza kushangaa kwa nini iwe hivyo, kama kweli utaweka juhudi na kufikia kile (more…)

Dhumuni kuu la biashara siyo kupata faida pekee.

By | May 23, 2016

Moja ya tofauti ya wajasiriamali na wafanyabiashara ni kwenye faida. Wafanyabiashara wanaongozwa na faida pekee, yaani wao wanaangalia ni kipi chenye faida na hivyo kukifanya. Lakini wajasiriamali wapo tofauti kidogo, wao hawaangalii faida pekee, bali wanaangalia mchango wanaoutoa kwa wengine. Wajasiriamali wanaangalia ni kipi ambacho kinakosekana na wanatafuta njia ya (more…)