UKURASA WA 424; Kulinganisha, Unyenyekevu Na Udadisi.

By | February 28, 2016

Unapojilinganisha na wengine, kwa njia yoyote ile unakata tamaa. Kwa sababu hata uwe bora kiasi gani, hata uwe unaweza kiasi gani, kuna ambao wanaweza kuliko wewe. Hivyo unapojilinganisha, utaona kama wewe siyo kitu, na kukata tamaa ya kuendelea kuweka ubora, hasa pale ambapo unakuwa umezidiwa sana na wengine. Hivyo basi (more…)

UKURASA WA 423; Kinachokuzuia Kubadili Tabia Usizozipenda.

By | February 27, 2016

Katika safari hii ya kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa, kuna tabia nyingi sana unahitaji kuzibadili. Hii ni kwa sababu kuna tabia ambazo ulikuwa umeshajitengenezea ambazo zinakuwa kikwazo kwako kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Lakini zoezi la kubadili tabia siyo rahisi. Wanasema tunajenga tabia halafu baadaye tabia zinatujenga. (more…)

UKURASA WA 422; Chanzo Kikuu Cha Migogoro…

By | February 26, 2016

Tumekuwa tunakutana na migogoro mingi sana kwenye maisha yetu, migogoro ya ngazi ya chini baina ya watu na hata migogoro ya ngazi za juu kabisa ambayo inapelekea mpaka vita. Migogoro hii inakuwa hatari sana kwa maendeleo na mafanikio yetu kwa sababu inavuruga kabisa mahusiano yetu na kushirikiana kwetu na wengine. (more…)

UKURASA WA 421; Kwa Sababu Kila Mtu Anafanya…

By | February 25, 2016

Binadamu sisi ni viumbe wa kijamii, tunapenda kuwa sehemu ya jamii na ili kuwa sehemu ya jamii tunalazimika kufanya yale ambayo jamii imezoea kufanya. Katika hali hii tunajikuta tunalazimika kufanya kitu sio kwa sababu tunapenda, au kwa sababu tunajua maana yake ila tu kwa sababu kila mtu anafanya. Sasa hakuna (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; Don’t Go Back To School (Usirudi Tena Darasani).

By | February 24, 2016

Tangu kuwepo kwa mfumo rasmi wa elimu, elimu ya darasani imekuwa inapewa kipaumbele kikubwa sana kwenye jamii zetu. Imekuwa ikizoeleka sana, wale ambao wanapata elimu rasmi ya darasani ndio pekee wanaopata nafasi za kuajiriwa na kuwa na maisha bora. Ila kwa sasa mambo yamebadilika sana, elimu ya darasani karibu kila (more…)

UKURASA WA 420; Njia Ya Uhakika Ya Kuwa Na Amani Isiyotikiswa.

By | February 24, 2016

Maisha bora yanaanza na amani ya moyo ambayo unayo. Kama moyoni mwako huna amani, haijalishi unamiliki vitu gani, bado maisha yataonekana kuwa magumu na huwezi kuyafurahia. Na amani hii ya moyo inatokana na mambo mengi. Kwanza inaanza na kufanya kile ambacho unapenda, kuchagua kuishi maisha ambayo yana maana kwako na (more…)

UKURASA WA 419; Unachokijua Ndio Kinachokupoteza…

By | February 23, 2016

Ukilinganisha na vitu ambavyo tunatakiwa kujua, tunavyojua mkapa sasa ni vichache sana. Yaani ni sehemu ndogo sana ambayo kila mmoja wetu mpaka sasa anajua. Ukiangalia kuhusu maisha, ambayo ndiyo biashara inayomhusu kila mmoja wetu, tunajua kidogo sana, bado kuna mengi ambayo ni muhimu lakini bado hatujayajua. Tatizo sio kujua kidogo, (more…)

UKURASA WA 418; Maandalizi Na Kufanya.

By | February 22, 2016

Kuna wakati tunasahau ni kipi muhimu sana kwenye kufikia malengo yetu na mafanikio pia. Tunaweka juhudi zetu kwenye mambo ambayo yanaweza kuonekana ni muhimu lakini kwa uhalisia sio muhimu. Kwa mfamo, tunapoweka malengo na mipango, kuna maandalizi na kufanyia kazi malengo na mipango hiyo. Lakini watu wengi wamekuwa wakiweka muda (more…)

Zingatia haya unapopeleka biashara yako sehemu mpya.

By | February 22, 2016

Pale biashara yako inapokua, unaanza kuona fursa nyingi zaidi za kukuza biashara hiyo. Haya ndiyo madhara mazuri ya kuendesha biashara yako kitaalamu. Na unapofika wakati wa kuikuza zaidi biashara yako, kufungua matawi sehemu mpya ni moja ya sehemu za ukuaji wa biashara yako. pamoja na kufanikiwa sana kwa biashara kwenye (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Mtu Pekee Unayeweza Kumpa Furaha Kwenye Maisha Ni Huyu Hapa.

By | February 21, 2016

Karibu mwanafalsafa mwenzangu kwenye siku hii nyingine ambapo tunakutana pamoja katika kujenga falsafa bora sana itakayoongoza maisha yetu. Kupitia falsafa hii mpya tunapata mwongozo wa maisha bora, yenye furaha na mafanikio makubwa sana. Leo katika falsafa tutachimba ndani kuhusu furaha ya kweli kwenye maisha. Kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana kwenye (more…)