Ndio, hakuna jipya, lakini bado unahitaji kujifunza “KILA SIKU”.

By | November 3, 2015

Habari za leo rafiki? Naamini uko poa sana, rafiki yako niko vizuri sana. Karibu tena kwenye mazungumzo yetu haya muhimu sana kama marafiki. Karibu tushirikishane yale muhimu katika safari yetu hii tuliyochagua, safari ya kuwa tofauti na kuwa bora sana kila siku. Leo nataka tushirikishane jambo moja muhimu ambalo limekuwa (more…)

Sababu za biashara kushindwa ni za ndani na sio nje ya biashara.

By | November 2, 2015

Karibu tena kwenye kona yetu hii ya mjasiriamali ambapo tunajifunza mambo muhimu kuhusu biashara na ujasiriamali. Kupitia kona hii unapata mbinu mbalimbali za kuiwezesha biashara yako kwenda vizuri na wewe kufikia malengo yako ya kibiashara. Kama wote tunavyojua biashara zina changamoto nyingi. Kabla hujaingia kwenye biashara unaweza kuwa na mipango (more…)

UKURASA WA 306; Aina Mbili Za Kufanya Kazi….

By | November 2, 2015

Kuna aina mbili za kufanya kazi yoyote ile unayojishughulisha nayo. Iwe ni kazi ya kuajiriwa, ya kujiajiri, biashara au hata kazi ya sanaa kama muziki au uandishi. Aina ya kwanza tayari unaijua kwa sababu tumekuwa tunaijadili sana. Aina hii ni kufanya kazi iliyo bora, kuboresha kila siku, kufanya kwa utofauti, (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Hakuna Anayejua Kwa Hakika Kile Anachofanya, Na Jinsi Unavyoweza Kutumia Hali Hiyo Vizuri.

By | November 1, 2015

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Karibu tena jumapili ya leo tuendelee kushirikishana misingi muhimu kwenye falsafa yetu hii mpya ya maisha. Kupitia falsafa hii tunaishi yale maisha ambayo tunayapenda na hivyo kuwa bora kwetu bila ya kujali wengine wanachukuliaje. Kuna changamoto moja kubwa sana ya maisha ya kila mtu, na (more…)

UKURASA WA 305; Njia Bora Ni Kufanya….

By | November 1, 2015

Watu wengi wamekuwa wakifikiria njia bora ya kuwa kile wanachotaka kuwa. Njia bora ya kuingia kwenye biashara, njia bora ya kufanya kazi, njia bora ya kusoma, njia bora ya kuwa na maisha bora. Unaweza kufikiri sana hili, unaweza kujifunza sana, unaweza kuweka malengo na mipango mizuri. Lakini haya yote hayatakuletea (more…)

UKURASA WA 304; Unayaweka Wapi Mawazo Yako Kati Ya Sehemu Hizi Mbili?

By | October 31, 2015

Unapofanya jambo lolote la kukufikisha kwenye mafanikio makubwa, maana yake hili ni jambo kubwa na ambalo huenda hujawahi kufanya, mawazo yako yanaweza kuwa sehemu moja kati ya hizi mbili. Sehemu ya kwanza ni kufikiria yale matokeo unayotaka kuyapata, kufikiria kile kitakachotokea baada ya wewe kukamilisha hilo. Hapa unaiona picha ya (more…)

UKURASA WA 303; Unapoamua Kile Unachotaka…

By | October 30, 2015

Maana yake unajua kabisa ya kwamba kuna vitu vingine vingi unataka, lakini hiki ni muhimu zaidi. Unajua ya kwamba kuna vingi vitakuja njiani lakini hutaacha hiki ulichoamua kwa sababu ya vitu hivyo. Unajua ya kwamba utakutana na changamoto nyingi lakini hutakubali zikurudishe nyuma. Unajua kabisa ya kwamba kuna wengi watakukatisha (more…)

MABORESHO ZAIDI KWENYE KISIMA CHA MAARIFA KUANZIA NOVEMBER 2015.

By | October 29, 2015

Kuanzia mwezi november mwaka huu 2015 kutafanyika maboresho zaidi kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Maboresho haya ni kuhakikisha wewe unapata maarifa bora zaidi yatakayokuwezesha wewe kuchukua hatua ya kuboresha kazi zako, biashara zako na hata maisha yako kwa ujumla. Kumbuka maarifa ni muhimu sana kwako kama unataka kufikia mafanikio makubwa kwenye (more…)

UKURASA WA 302; Kushindwa Kunapatikana Sehemu Moja Tu, Na Kwa Bahati Nzuri Haupo Sehemu Hiyo.

By | October 29, 2015

Kuna sehemu moja tu ambayo kushindwa kunapatikana na sehemu hiyo ni kaburini. Ndiyo ni kaburini pekee ambapo kushindwa ndio kunapatikana. Kwa sababu unasoma hapa, naamini hujafika kaburini na hivyo hii ni habari njema kwamba bado hujashindwa. Mtu pekee ambaye tayari ameshashindwa ni yule ambaye ameshakufa, maana huyu hana njia yoyote (more…)